Kupima Ukimwi sasa ni nyumba kwa nyumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupima Ukimwi sasa ni nyumba kwa nyumba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ishuguy, Dec 5, 2009.

 1. i

  ishuguy Member

  #1
  Dec 5, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imeanzisha huduma mpya ya upimaji Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini itakayofanyika nyumba hadi nyumba.
  Waziri wa Wizara hiyo, Profesa David Mwakyusa, aliyasema hayo katika hotuba yake ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku Ukimwi Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani hapa.
  Hotuba ya Waziri Mwakyusa ilisomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Hawa Ghasia.
  Profesa Mwakyusa alisema wizara hiyo imeanzisha huduma hiyo baada ya kampeni ya kitaifa ya kupima virusi hivyo kwa hiari iliyozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam mwaka juzi.
  Alisema katika mpango huo mpya, wahudumu wa afya watatembelea kila mwananchi nyumbani kwake na kumshawishi kupima VVU kwa hiari.
  Alisema kwa kuanza huduma hiyo inatolewa wilaya za Bagamoyo mkoani Pwani, Mvomero (Morogoro), Kilolo (Iringa), Temeke (Dar es Salaam) na Arumeru (Arusha) na inatarajiwa kusambazwa wilaya zote nchini.
  Alifafanua kuwa lengo la kuanzisha mpango huo ni kuwezesha Watanzania wengi kupima virusi, hivyo kujua kiwango halisi cha maambukizi nchini.
  Alisema takwimu zinaonyesha kwamba kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka huu, idadi ya watu waliopimwa VVU kwa hiari nchini imefikia milioni 7.3 na kusisitiza kila Mtanzania bado anahitaji kupima aweze kujua hali yake na kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya yake.
  Akihutubia taifa katika kilele hicho, Pinda aliwatahadharisha wananchi kuwa Ukimwi bado ni tishio kutokana na takwimu kuonyesha unaua watu wengi.
  Pinda alisema hali hiyo inawatahadharisha Watanzania kutobweteka kwa kujipa matumaini kuwa maambukizi ya VVU yanazidi kushuka, bali wanapaswa kutambua kila mwaka unaua idadi kubwa ya watu.
  CHANZO: NIPASHE  hongera waziri na wizara yako kwa kijitihada hizo.
  hapo me naona inaweza kupunguza kasi ya maambukizo kama watu watajitambua kuwa wako salama au la.
  watanzania tuunge mkono jitihada hizi, kwani ni kwa manufaa yetu wananchi, itachekesha pale watu watakafuatwa makwao halafu wakagoma kupima..
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  kupima watapima then what next?
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  kinacho takiwa ni kujitahidi kupunguza umaskini. Akina dada zetu ambao wana opt kujihusisha na biashara ya miili yao wawezeshwe ili biashara hiyo itambulike na hapo wataweza kuwa na maamuzi na miili yao kuliko ilivyo sasa.

  Wenye mabaa na mahoteli wawalipe vizuri wahudumu wao ili wasijiingize kwenye uzinzi ili kujiongezea kipato.
   
 4. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  kwa kuanzia, bora waanze kupima nyumba ya huyo waziri.
   
 5. c

  chelsea Member

  #5
  Dec 5, 2009
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wenye mabaa na wamiliki wa biashara nyingine waache kutumia mapenzi kama kigezo cha kuwapa kazi wadada zetu
   
 6. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Waste of time, energy and money! Mi naamini kila mtu anakwenda hospitali at some point, kwanini huo ushawishi usifanyike nyakati hizo? Au mtu akienda kucheck malaria au typhod- si inawezekana akatolewa damu ya kutosha kufanya test zote kwa pamoja? Na mbona hii habari haituambii utaratibu mzima wa kasheshe la kupeana majibu utakuwa vipi?
   
 7. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,054
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 280
  Hiyo nyumba kwa nyumba waanzie kupima Magogoni,Oysterbay,Masaki,mbezi beach ndo wamalizie huku kwetu Uswazi.
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ni vilevile tu.
  Ni kupima kwa hiari, tofauti ni kwamba wapimaji wanakuja nyumbani.

  Kwa mtu asiyetaka, then anaacha, na hakuna tatizo!
   
 9. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #9
  Dec 5, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mi simo tusubiri vituko
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Dec 5, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mimi nasema wazi nyumbani kwanguasije mtu......la sivyo tusilaumiane.
   
 11. M

  Magezi JF-Expert Member

  #11
  Dec 5, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Huu wote ni usanii tu wa CCM ili wale pesa. Kwa nini vifaa vya kupimia HIV visiwekwe kwenye kila zahanati, vituo vya afya, mahospitali yote n.k. ili kila mgonjwa au mtu yeyote anayefika pale anapimwa na iwe ni lazima bila hivyo hakuna huduma.
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Its a good move, lakini tujijulize utayari wetu kwenye
  ikiwa watu wanatest positive, tupo tayari kuwasajili wakati donors tayari wanakata funds?
  Je tumeshaandaa dawa na diagnostics za kutosha for pateints enrolment an follow-up?
  kupima ni hiyari sasa je wakija nyumbani si watapima kila mtu au at least majibu itabidi yawe yanafahamika, hii haiwezi kuongeza stigma?
  Tuna enough washauri nasaha for to course?
  Maunga mkono hoja nikitegemea kwamba wfnyakazi wa wizara ya afya watakuwa wa kwanza kujaribiwa

  tena tusifanye majumbani tu!! bali tuanzie maofisini, na pale wizarani ndio patamu kuanzia, kisha mahospitali ya rufaa, mikoa na wilaya

  halafu kwingine!!
   
 13. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #13
  Dec 5, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  I concur with you MTM. Good comment
   
 14. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ah!! nyumba yangu asije mtu labda kwanza ajipime yeye kisha nione majibu yake ndo na mimi nitaamua kupima au la! ok. this is Conf bwana hayo majibu tutapeana vipi siitakuwa Kasheshe.
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mchungaji kwani tatizo liko wapi, mbona umekataa hata kabla ya ushauri nasaha?
   
 16. M

  Matarese JF-Expert Member

  #16
  Dec 5, 2009
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mkuu kula tano! hilo ni swali muhimu kweli kweli, sijui kama wanaoanzisha huu "mradi" wana jibu. Inawezekana kabisa kuna mtu kaleta container la mashine za kupimia au chemicals zake.

  Lakini pia kuna upotoshaji mkubwa katika jambo hili. Ukimwi(AIDS) sio ugonjwa as such,ni syndrome. Ina maana hata mtu asiye pata chakula bora aweza kuwa na hii syndrome. Tatizo letu kubwa tatizo ni UMASKINI uliokithiri. Watu wanakufa kwa ajili ya hilo.Kwa bahati mbaya sana, people are mislead, na mostly mipango na mikakati mingi kuhusu HIV(AIDS) Tanzania imekuwa ni miradi ya watu kujinufaisha. Ili tuweze kutatua tatizo hili, kwanza tutatue tatizo la UMASKINI ULIOKITHIRI kwa watanzania, na sio kwenda kupima nyumba hadi nyumba.
   
 17. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #17
  Dec 6, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Na wanaume wanashawishiwa na kitu gani? nao wanalipwa pesa?
   
 18. i

  ishuguy Member

  #18
  Dec 6, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15

  tatizo kuna baadhi ya watanzania bado wanategemea mitishamba hawakanyagi kabisa hospitalini.. sasa huduma itawafiakiaje?
   
 19. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #19
  Dec 6, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Suala la kupimwa UKIMWI ni suala la HIARI na sio la lazima kisheria.

  Sasa kama watalazimisha watu wapime kwa lazima basi watakuwa wanavunja sheria.
   
 20. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #20
  Dec 6, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wanataka kufahamu soko la bidhaa zao (drugs) duh!

  Kupima vs kupungua uambukizi..kuna uhusiano wowote au wanataka kujua ni kiwango gani cha madawa kinahitaji (market size) maana ukimwi umeshakuwa biashara kubwa kwa makampuni ya madawa..etc..lol
   
Loading...