Kupima DNA kwa lengo la kujua uhalali wa mtoto kunatoa majibu sahihi?

Matokeo ya DNA ni 100% sahihi. Ni matokeo ya Maabara sio ya Ustawi wa Jamii.

Nimeshasimamia zaidi ya vipimo 30, vipo vilivyoleta majibu 99.99% na 0.00%.

Wengi wa wateja hufuata hatua za upimaji wakiwa tayari na imani kuwa majibu yatakuwa (-). Na hushtushwa na kuwa (+). Hii ni kutokana na tabia binafsi za wenzi wao au historia ya mahusiano yao.

Mshauri jamaa alee mtoto tu.
Huwa mnatabia za kuchakachua majibu wala si uongo yaani bora kupima nje ya nchi
 
Huwa mnatabia za kuchakachua majibu wala si uongo yaani bora kupima nje ya nchi
Mimi sio Mkemia. Ni Mwanasheria.

Matokeo ya DNA huthibitishwa/hukikiwa/hutazamwa na watu watatu tofauti.

Haina kuchakachua.

Kulikuwa na kesi ambayo mteja alikaaa matokeo ya DNA ya Tanzania na alienda kurudia vipimo Kenya. Majibu yakawa vile vile.
Akaanza kunishawishi kuwa tuwasilishe majibu tofaiti kwa Mwezi wake-nikakataa.

Tuwajibike kwa matendo yetu. Tuamini Sayansi.
 
Halafu mimba huwa Ni wiki 36 hesabu yake sio miezi 9 ya huku kitaa Kuna uwezekano kujifungua wiki ya 34 au 35,

Alipomuingilia baada ya kutoka safari yawezekana mwanamke alikuwa siku za joto ndo maana alihisi utofauti na ukitegemea hasa km alikuwa na muda mrefu hajakutana na mwanaume
 
Majibu ya DNA ya watoto ya kweli ni yale ya kwenye kesi labda za wanafunzi kupewa mimba ila hizo kesi kama za kwenye ndoa mara nyingi wanalinda ndoa zisivunjike.
Niliwahi sikia afisa mmoja wa ustawi wa jamii anasema hawapendi kuona ndoa inavunjika.
 
Back
Top Bottom