Kupika. . . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupika. . .

Discussion in 'JF Chef' started by Lizzy, Feb 5, 2012.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  . . .What are you Great at?!!

  Nini ukipika watu wengine wanaomba kuongeza chakula kama hawana akili nzuri? Au hawaachi kuomba uwaambie ulichoweka? Au hawaachi kutania kwamba lazima umeweka dawa au 'umepika bila nguo' lolz. . .ama wengine unashangaa wanaishia kupenda chakula ambacho hawakuwahi kukipenda mwanzo.

  Mimi . . .
  1. Maharage/makande, ya nazi au bila nazi. Nimefanya watu wasiopenda wananiuliza kila siku ntapika lini tena.
  2. Ndizi na viazi, za nazi, mchemsho, samaki n.k. . ."lini tena nije kula" na "ntapata cha kuondokea ehhhhh?!" hua nyingi.
  3. Cabbage ya nyama, na kachumbari za aina mbili hua hazikosi kuuliziwa.
  4. Chapati. . . hehehe hizi hua zinanipa mtu wa kunisaidia kazi zangu kabisa. Nasema tu nnatamani kupika chapati ila sina nafasi mtu anajitoa mzima mzima.
  5. Wali. . kwanzia pilau tulozoea, pilau ya mautundu binafsi, wali mweupe wa namna tofauti tofauti.
  6. Kuku haswa wa kuoka. . hua nakua kichaa na spices and it always pay off.
  7. Kitoweo (mchuzi) cha nyama au samaki. Wakati naanza kupika back in the days nilikua napata malalamiko sana wakati wa kula. . mchuzi ni mdogo. Kuna watoto tulikua tunaishi nao wenyewe walikua wanapenda wakidumbukiza tonge la ugali kwenye mchuzi ile kupeleka mdomoni mchuzi utiririke mkononi (I HATE THAT). . na kwenye wali waone punje zinaelea, but they eventually got over it.
  8. Lasagne & pizza japo mimi silagi.
  9. Samaki na nyama ya kuoka. . .lazima watu walambe vidole na kuuliza kama kuna iliyobaki.
  10. Pork chops. . . nilimfundisha mtu miaka mitatu iliyopita mpaka leo haachi kunifagilia yeye akifagiliwa.
  11. Chips . . . sikua najua ni nzuri kiviiiiile mpaka nilipoanza kuulizwa huwa nazifanyaje.
  12. Na ya mwisho nnayokumbuka (samahanini msiopenda) KITIFAYA. . . yani hapo ndipo moto unapozimika.
   
 2. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wali nazi maharage!!
   
 3. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Denda lan'tiririkaje ! Hadi kuskirini ! Huko mbeleni napendekeza Ban kwa watamanishao wenzao aninesale!
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hhmmm unakaribisha wageni nije kujihakikishia?
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ohhh pole J. . .
  Weekend hii, hujaenda kudoea sehemu?
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Wali na kisamvu cha Karanga + nazi ..oops
   
 7. N

  Nehondo JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Chapatiiiii, njegere, nyama
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Hapo add samaki mkavu na kachumbari mmh yum yum!
   
 9. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  wee njoo tu, ila usije na Hot pot, njoo na rambo yako na ndizi mkononi!!
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  jamani nachukia kupika???
  i would rather do additional maths kuliko kupika.

  Big up kwa mnaopenda kupika, i real envy you guys.
   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Wifi tukubaliane hapa kuwa bragging a bit inakubalika. Mimi napenda kupika coz napenda chakula kizuri. Nikiingia kwa watu nikafunua bakuli nikaona hakuna mvuto, naanza kutangaza diet manake ntagusa tu! I can't stand bad food, that is it!
  Ila ukiachia vitumbua ambavyo sijawahi jaribu kupika, nadhani I a good cook. Ila my killer chapattis ndo funga kazi. My mom's family secret recipe, kama ushawahi ona chapati inanyambuka kama croissant, lainii afu not greasy,lol
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mama wa kwanza itabidi unifundishe.. . .kisamvu sijala nna miaka ,na huko nyuma wala sikuwahi kupika mimi.
   
 13. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sasa upate chapati na chai ya maziwa iliyoungwa hiliki au chai rangi iliyotiwa karafuu, ni balaa! Kitambo kidogo pale Kariakoo kwa wale Wasomali wa hoteli ya Al Uruba nilikuwa napiga Chapati na Roast ya nyama ng'ombe!!
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ahhh njegere na wali ni mwisho wa matatizo.

  Samaki mkavu na wali?
  Mi napenda na ugali, tena awe perege. Yani ntatafuna mpaka mifupa.
  Hehehe nije na ndizi kwani ni ubwabwa wa shughuli?
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kula je. . . Unapenda na kufurahia?
   
 16. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #16
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Afadhali hata additional na basic applied maths unazijua! Manake wewe hukawii kusema afadhali upewe adhabu ya kuangalia tv kuliko kupika!
  Haya, here is how to entice ur cooking hobby: invest in a good kitchen, gadgets za kurahisisha maisha na sink zuri la kuoshea vyombo na convenient dustbin. In 20 mins, with a 4 stoves cooker ngoma iko mezani kitu cha 3 course!
   
 17. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #17
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Kama ulikuwepo hapo kwenye chai nzito ya maziwa, yenye iliki na tangawizi mbichi! Afu kuwe na maharagwe na nyama, lol salaaale!
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Feb 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hahaha wifi we mbona ni miss 'brag much'. . lolz

  Duh. . .yani kama mimi. Sehemu ambazo najua msosi wao sio mi hua nasema sina njaa hata kama tumbo linanguruma. Na kama kulala kunanihusu ntajitolea kupika ili nijue angalau dinner hainipiti.

  Mi vitumbua hua napika sema hua nasumbuka sana na zile chapati zake (sijui wanaziiitaje vile ). . .otherwise filling hua inakua mwake sana. Yani hapo hata nikifunga macho hamna kufeli.

  Hahahaha unaringia chapati za kuchambuka ehhh? Embu tushindane siku moja . . . lolz. . .maana siri naijua sana!!
   
 19. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #19
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Yah, wali maharage nazi, na samaki mkavu kwa pembeni, nina tatizo la nyama kwenye meal yangu, i gotta have it, i gotta have some meat.lol
   
 20. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #20
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sasa hao wanaosema hawawezi kupika si ndiyo wanatukimbiza kabisa!! Misosi ya kupikiwa home ndiyo delicious lakini vya hotel ni vicious ila vinapambwa na matukio maalum
   
Loading...