Jinsi ya kupika maharage kwa njia rahisi bila kutumia gharama kubwa

elwiza

Member
Dec 9, 2011
14
3
1600609047491.png

1600609126345.png


Wadau wanao hitaji kujua jinsi ya kupika maharage
Wadau samahani, Yani kila siku napojaribu kupika maharage ile natoka na kurudi ndani nakuta nyumba imejaa moshi vitu vimeungua sana. Yani hivi mnafanyaje fanyaje wakuu!

Nimechoka kula mama ntilie aisee.
----
Napenda maharage na wali au na ugali au na chapati kuliko hata navyopenda nyama au samaki, ila issue ni kuyapika huku mjini ni gharama sana mpaka uwe na mkaa.

Hivi kwa mtu aliye bachelor ni bora kununua maharage yaliyopikwa mgahawani au bora kununua maharage na mkaa na kupika? Kipi nafuu?

Sent using Jamii Forums mobile app


Jinsi ya kupika maharage
Kuna njia mbali mbali za kupika maharage lakini kuna moja haitambuliki sana na watu wengi ingawa inahitajika mpishi awe na subira pale anapotumia mbinu hiyo.

Unachohitaji kuwa nacho ni 'Chupa ya chai au Thermos Flask' pekee na utapika maharage mpaka yaive kwa njia nyepesi na bora zaidi.

Mbinu hii wengi wetu hatuitumii na sio maarufu kwa mapishi ya maharage kama njia nyingine zilizozoeleka ijapokuwa ni bora zaidi na inapunguza gharama za mkaa, gesi, umeme na mafuta ya taa kama nishati za kupikia.

Hatua zifuatazo ni muhimu kwa mapishi ya maharage:-

1. Kwanza, tafuta chupa ya chai (Thermos Flask) ambayo itakuwa na ukubwa sawa na maharage unayotaka kupika.

2. Pima kiwango cha maharage unachohitaji kwa kutumia kikombe.

3. Chemsha maharage hayo kwa muda mfupi kwenye sufuria.

4. Yaweke maharage hayo kwenye chupa hiyo ya chai kisha ufunge kwa nguvu kuzuia hewa kuingia.

5. Yaache kwa muda wa masaa sita kama ni usiku yaache yalale ndani ya chupa hiyo.

6. Baada ya hapo, maharage yako yatakuwa yanafaa kupikwa vizuri kwa viungo kwa ajili ya kula na wali, ugali, maandazi au kama futari.

1600609722724.png


Maoni na michango ya wadau kuhusu aina hii ya upishi wa maharage
Hatua ya kupika maharage kutumia chupa ya chai.

1. Tayarisha maharage yako vizuri
2.Chemsha maharage yako kwa dk kumi kwenye gesi au jiko la umeme
3. Hamishia maharage yako kwenye chupa ya chai ambayo unauhakika inafanyakazi vizuri. Hakikisha unaacha nafasi kidogo maana kuruhusu expansion.
4. Funga vizuri chupa yako na mfuniko.
5. Maharage yako yatakuwa yameiva baada ya masaa 12.

Njia hii nizuri jioni kwa maharage ya kesho yake asubuhi na jioni.

----
Habari za mapumziko ya mwisho wa wiki,

Leo nimeona bora niwashirikishe jambo moja hasa wale wanaoishi single a.k.a bachelor.

Mara nyingi nimeona watu wa kada hii husumbuka sana katika maandalizi ya chakula na kupelakea kuwa na mahusiano mazuri na wauza chips au Mama lishe ili angalau kuitendea haki miili yao, na mara nyingine wanabuni mboga rahisi kama mayai, dagaa wa kukaanga na mtindi ili kukamilisha zoezi. Lakini napenda kuwajulisha sasa unaweza kupika maharage kwa dk 10 na ukafurahia maisha, fuata maelekezo haya;

1. Andaa maharage yako tayari kwa kupikwa,

2. Washa jiko lako kisha tenga maharage yako, subiri mpaka yachemke kabisa (boiling point)

3. Mimina maharage na maji yake kwenye Thermos (chupa ya chai) hakikisa chupa yako haipozi, na pia hakikisha maji yanajaa mpaka juu.

4. Funika chupa yako vizuri kisha ondoka nenda kazini.

5. Ukirudi toka kazini njoo na nyanya,vitunguu,karoti nk tayari kuunga maharage yako tayari kwa kuliwa.

Nawatakia Siku njema, nasubiri mrejesho.

Stay blessed
----
Nunua thermos zile kubwa za lita 2.5 au zaidi but siyo lazima ila thermos kubwa inakuwasaidia kwa mambo mengi.

Ukiwa umeshanunua maharagwe yako na kuyasafisha, chemsha maji kulingana na maharagwe yako, maji yakichemka nyuzi joto zinazotakiwa mimina kwenye thermos na yale maharagwe.

Zoezi hili lifanyike masaa 5-8 kabla ya muda unaotaka kuyaunga, njia hii niliitumia sana miaka ya ubachera nikiwa na jiko la mchina lile la mafuta, ambalo likiingiza hewa linalipuka.
----
Umewazungusha sana, njia rahisi ni chukua maharage yako, yaloeke kwenye maji ya baridi tuu kwa masaa 6-7 yatakuwa yashavimba=kulainika.

Then baada ya hapo unayainjika kwa dakika 20-30, yanakuwa tayari kwa kuliwa. Na quality yake inabaki palepale.

NB: Ukiyaloeka kwa masaa zaidi ya 24, utakuta yashaota. Hizi techniques tunaiga toka vijijini tulikotokea ambapo mvua ikiwahi kunyesha na ikakukuta hujapanda, basi unachofanya unaloeka mbegu zako kwa siku moja, baada ya saa 24 zinakuwa zishaota ndio unazipanda. Ukipanda leo kesho yake unakuta zimeshachomoza.


Unforgetable
 

Attachments

  • 1600609723705.png
    1600609723705.png
    270.6 KB · Views: 26
  • 1600609724552.png
    1600609724552.png
    270.6 KB · Views: 25
Hatua ya kupika maharage kutumia chupa ya chair.
1. Tayarisha maharage yako vizuri
2.Chemsha maharage yako kwa dk kumi kwenye gesi au jiko la umeme
3.hamishia maharage yako kwenye chupa ya chai ambayo unauhakika inafanyakazi vizuri. Hakikisha unaacha nafasi kidogo maana kuruhusu expansion
4. Funga vizuri chupa yako na mfuniko
5. Maharage yatako yatakuwa yameiva baada ya masaa 12.

Njia hii nizuri jioni kwa maharage ya kesho yake asubuh na jioni.
Nitaijaribu leo nione matokeo yake... ahsante sana.
 
Hatua ya kupika maharage kutumia chupa ya chair.
1. Tayarisha maharage yako vizuri
2.Chemsha maharage yako kwa dk kumi kwenye gesi au jiko la umeme
3.hamishia maharage yako kwenye chupa ya chai ambayo unauhakika inafanyakazi vizuri. Hakikisha unaacha nafasi kidogo maana kuruhusu expansion
4. Funga vizuri chupa yako na mfuniko
5. Maharage yatako yatakuwa yameiva baada ya masaa 12.

Njia hii nizuri jioni kwa maharage ya kesho yake asubuh na jioni.
True! nimeshajaribu hiyo kitu.
 
iyo nafasi naicha vip, pia hiyo chupa ndan kusiwe na maji kabsaaa??
Chupa ya chai inatunza joto.
Ukiweka maji yatendelea kuwa na joto. So maharage yataendelea kuwa na constant supply ya joto.

Maji yawepo
 
Wadau samahani, Yani kila siku napojaribu kupika maharage ile natoka na kurudi ndani nakuta nyumba imejaa moshi vitu vimeungua sana. Yani hivi mnafanyaje fanyaje wakuu!

Nimechoka kula mama ntilie aisee.
 
Hewaaaa maharage nazi nilikula Zanzibar ndiyo nikawa natamani nijaribu kuyapika.
Ngoja nijaribu Mkuu nione kama nitafanikiwa.
Changanya pia na brocoli, pilipili hoho, carrot na maharage machanga,hapo utazidi kuyapenda maharage, hizo mboga nilizozitaja una zi steam halafu wakati wa kuunga maharage ndio unachanganya pamoja
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom