Kupigwa na mwekezaji kisa kutofika kazini, ni halali?

kisute

Member
Oct 6, 2010
54
3
Wana jamvi nahitaji msaada wenu kwa hili.
Jamaa yetu mmoja (mtingaji mgodini) leo hii kapata kisago kisa hakufika kazini kwa siku mbili.
Kabla ya kujitetea alipigwa na kiongozi wake ambae ni kaburu hadi kuzirai. Alipopata fahamu alijikuta yuko clinic kaumia mbavu na mkono mmoja. Je, kwa kosa la kutofika kazini adhabu yake ni kipigo? Hii sheria ni ya nchi gani. Nini afanye huyu ndugu yangu.:shetani:
 
khaa hivi hawa wageni hua wanajiamini nini humu nchini kwetu? Nani anawapa viburi? Au wuamegundua sisi watanzania ni wakarimu na wapole hasa kwa wageni wanaokuja inchini kwetu?:A S angry:

Nakumbuka niliwahi shuhudia raia mwenye asili ya ki-Asia akimtishia kumgonga na gari kijana muosha vioo kwenye foleni ya traffic lights pale Magomeni. Kama haitoshi akashuka chini na kumfuata kumpiga mateke, huku walio jirani pamoja na wenzie wakiwa wanaangalia tu wasijue cha kufanya.

Nilikereka zaidi baada ya kugundua pembeni kuna bus la Mbagala-Mwenge na kuna askari (polisi-usalama wa raia na mali zao) akiwa anashuhudia hizo fujo kupitia dirishani kama vile anaangalia mieleka ya John Cena.

Ipo siku historia ya sehemu fulani ulimwenguni itajirudia hapa Tanzania.
 
Wana jamvi nahitaji msaada wenu kwa hili.
Jamaa yetu mmoja (mtingaji mgodini) leo hii kapata kisago kisa hakufika kazini kwa siku mbili.
Kabla ya kujitetea alipigwa na kiongozi wake ambae ni kaburu hadi kuzirai. Alipopata fahamu alijikuta yuko clinic kaumia mbavu na mkono mmoja. Je, kwa kosa la kutofika kazini adhabu yake ni kipigo? Hii sheria ni ya nchi gani. Nini afanye huyu ndugu yangu.:shetani:

Mkuu katika hali yoyote ile kumtusi ,kumpiga au hata kumsukuma tu kisheria ni kosa na kama utafanikiwa kuishawishi mahakama na ikaridhika na ushahidi mtuhumiwa lazima atapewa adhabu.
Katika tukio hilo la mwajiri kumpiga mfanyakazi wake kuna uwezekana wa Kesi ya jinai au kufungua kesi ya mgogoro wa kiajira ambayo kwa mujibu wa sheria ya ajira 2004 inaweza kuangukia kwenye kipengele cha sita(6)Forced labour.
Ningekushauri ndugu yako atafute mwanasheria amsaidie lakini inaonekana pesa inaweza kutumika kuzima kesi hiyo.
Nakushauri pia usome ambatanisho hili ili uongeze ufahamu juu ya sheria ya kazi.
View attachment 65813View attachment 65815
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom