Kupigwa mnada kwa mali za kampuni ya udalali ya majembe kumenipa mafunzo haya

justin mwanshinga

Senior Member
May 22, 2014
146
500
MALIPO YA MUNGU NI TASLIMU

Ipo taarifa inayosambaa kuwa Oktoba 14, mwaka huu, mali za kampuni ya mnada ya Majembe zitanadiwa. Kwamba waliozoea kunadi mali za wenzao na zao zinaingia mnadani.

Watu wanashangilia. Wale ambao mali zao zimepata kunadiwa na Majembe wanafurahi kweli. Ukipita mitandaoni nayaona maandiko "muosha huoshwa". Kwamba Majembe walizoea kuosha wenzao, sasa nao wanaandaliwa maji na sabuni waoshwe.

Kwangu tukio la Majembe si shangwe, bali ndani yake ni elimu mbili. Ya kwanza ni athari ya kiuchumi. Hali ni mbaya, kampuni nyingi zinafilisiwa. Nyumba za watu zinauzwa kwa bei poa kwa sababu ya kushindwa marejesho mbalimbali kwenye taasisi za kifedha.

Mali za kampuni au za watu binafsi zinaponadiwa si jambo la kushangilia. Hicho ni kiashirio kibaya kiuchumi. Kwamba wenye mali zao mambo hayaendi sawa, hivyo wanashindwa kufikia malengo ya kiabishara, kwa hiyo hata mikopo wanashindwa kulipa.

Ukiwa Mtanzania mwenye kuiombea mema nchi yako, unapoona kuna wimbi kubwa la watu kufilisiwa mali zao, unatakiwa upate hofu, uionee huruma nchi yako na safari yake ya kiuchumi, maana hali ya mzunguko wa kifedha ni taabani.

Ukienda mbele ya hapo utaona kuna idadi kubwa ya watu wanapoteza ajira kwa sababu waajiri wao wanafilisiwa. Hapohapo unaona idadi ya watu ambao uwezo wao wa kuyamudu maisha yao na kuhudumia familia unavyoathirika. Unaona kuna watu ambao uwezo wao wa kununua unaporomoka. Yote hayo huzidi kuathiri uchumi. Mzunguko wa kifedha unaathirika.

Elimu ya pili ambayo inapatikana kutokana na tukio la Majembe mali zake kupigwa mnada ni matokeo yenye kudhihirika kuwa hakuna jambo ambalo unaweza kulifanya kwa mwenzako, likawa haiwezekani kufanyika kwako.

Majembe walinadi sana mali za watu, nao sasa hivi mali zao zipo kwenye matangazo ya mnada. Ni ukweli kuwa wao hupewa tu kazi ya kunadi. Hata hivyo ni wakati wao wa kuyahisi maumivu ya watu ambao walinadi mali zao.

Ni elimu kwa kampuni nyingine za mnada, kwamba mbwembwe na vishindo wakati wa kunadi mali za watu walioshindwa marejesho huongeza maumivu kwa wenye mali. Kuna yule mama wa Yono, hutangaza kwa mbwembwe kweli wakati mwenye mali analia.

SOMO PANA

Mali za Majembe kupigwa mnada ni mwendelezo wa utaratibu wa Mungu hapa duniani wa kurejesha maumivu upande wako ili uhisi sawasawa au zaidi ya vile ambavyo nawe umewahi kusababisha mwingine aumie.

Ni matokeo ya nadharia ya Karma ambayo inaelezwa vizuri katika nafundisho ya Burdha, kwamba ukifanya jambo leo, liwe jema au baya, utavuna matokeo yake. Utafaidi kwa wema uliotenda na utaumia kwa ubaya uliofanya.

Mungu ameweka utaratibu mzuri kabisa wa kudhihirisha machungu kwa binadamu ambao kwa namna moja au nyingine waliwaumiza wengine. Hudhihirisha machungu hayo kabla ya mtu husika hajatenganishwa na dunia.

Ukilitambua hilo utajua kuwa wanajidanganya wale waliopanga na kumshambulia kwa risasi Tundu Lissu, maana Mungu utaratibu wake ni uleule. Waliomjeruhi kwa risasi Lissu hawawezi kuwa salama, vinginevyo asiwe Mungu ninayemwabudu. Labda Mungu huyo awe mjomba wao.

Mungu ninayemwabudu ni yule aliyemwezesha mtoto mdogo Daud amuue jitu kubwa mno, Goliath. Aliyemwezesha mwanamke mjanja kumuua askari shupavu Sisera ambaye ndiye alikuwa kikwazo pekee cha wana wa Israel kuingia Canaan.

Mungu ninayemwabudu ni yule aliyeangamiza watu wa Nuhu walioidharau Safina. Aliyewageuza watu wa Luthu kuwa miamba ya chumvi kwa sababu ya dhambi kubwa waliyotenda pamoja na Mungu kujidhihirisha pachoni pao. Kama Huyo ndiye, basi waliomjeruhi Lissu watakuwa salama kwa muda tu. Muda utafika.

Umezaliwa kama mwenzako, umepewa fursa ya kuvuta pumzi ya uhai na kuishi kama mwenzako. Iweje umsababishie maumivu mwenzako? Unajaribu vipi kukatisha uhai wa mwenzako? Halafu uwe salama! Labda asiwe Mungu ninayemwabudu. Huyo atakuwa kaka wa mama yako!

Mungu ninayemwabudu ni yule aliyeyafanya maisha maisha ya Manuel Noriega yaishie jela na kufariki dunia akiwa mfungwa. Noriega wa Panama, 'mtoto' wa Marekani aliyeshirikiana na Mfalme wa Cocaine, Pablo Escobar kuuza dawa za kulevya ulimwenguni.

Noriega akawa muuza dawa za kulevya pekee anayependwa na kulindwa na Marekani. Noriega akawa tishio kwa Panama, akajisimika uongozi wa nchi kwa nguvu za kijeshi kwa jeuri ya fedha za unga kisha Marekani ikamuunga mkono.

Hata hivyo, muda ulipofika, ni Marekani waliomuondoa Noriega madarakani na kumfanya afie jela. Huyo ndiye Mungu nimjuaye. Mungu ninayemwabudu. Mungu ambaye hulipa kisasi akiwa haonekani.

Mungu ninayemwamini na kumwabudu, hahitaji kisomo cha Albadili ndipo afanye uamuzi wa kuwanyoosha wale wabaya wenye kukandamiza au kuwaumiza wenzao. Mwenyewe huona kisha huamua kushusha adhabu kwa anayemkusudia kwa wakati ambao huona unafaa.

MUNGU MKALI SANA

Mtazame Mungu na malipo yake. Ameishia wapi Dk Willibrod Slaa aliyedhihirisha chuki kwa Zitto Kabwe? Msaliti alimwita na kumfanya Zitto achafuke kwenye jamii iliyomheshimu na kumwamini, lakini muda ulipofika naye aliitwa msaliti na kwenye chama akakimbia.

Mkumbuke Nape Nnauye wa CCM ya Dk Jakaya Kikwete. Kijana pendwa na mwenye nguvu kweli. Aliwaandama watu wazito, Edward Lowassa na Rostam Aziz. Aliwatikisa kwa jina "fisadi", aliwafanya wakose raha ndani ya CCM.

Imefika leo, Nape hana furaha kwa sababu ya kijana Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kama ambavyo Nape alivyokingiwa kifua na JK dhidi ya akina Lowassa, ndivyo Makonda anavyolindwa na Rais John Magufuli.

Huyo ndiye Mungu nimjuaye mimi. Mungu asiyekopesha. Mungu ambaye hulipa taslimu. Mungu aliyewafanya Saddam Hussein na Ali Hassan Al-Majid 'Chemical Ali' waandamwe na damu ya Wakurdi waliowateketeza kwa kemikali miaka ya 1980. Nao uhai wao ukaondolewa kwa kitanzi.

Hivyo, aliyehusika na kupotea kwa Ben Saanane muda utafika na atalipa gharama. Mungu hajawahi kuwaacha watu wajichukulie sheria dhidi ya maisha ya wengine. Ukijipa kibali cha uhai wa wengine, Mungu ninayemwabudu hatakuacha salama.

Anajidanganya aliyewateka akina Roma Mkatoliki. Asije kukaa na kujipongeza kwamba anaweza kutesa watu kisha akabaki salama. Muda wake utafika. Dunia inaweza isijue, Tanzania isitambue chochote, hata mhusika akawa ameshajisahaulisha unyama wake, lakini Mungu atakuwa analipa kisasi.

Utawaongopea walimwengu lakini si Mungu juu ya unyama wa watu wanaouawa na kutupwa baharini kisha kukutwa kwenye mifuko ya sandarusi ufukweni Bahari ya Hindi. Walio nyuma ya unyama huo wanafanya utani na Mungu. Mimi nawaambia kuwa Mungu hana utani. Mungu ni mkali sana.

Kadhia za mauaji ya Kibiti na Mkuranga. Watu wasiojulikana na sinema zake. Hakuna asiyejulikana mbele ya Mungu. Watu waendelee kufanya mchezo na Mungu lakini wajiandae kwa kisasi. Mungu ninayemwabudu huwa hachekei unyama dhidi ya waja wake wasio na hatia.

Ni sawa kama unamaanisha kweli aliyemtishia bastola Nape hajulikani. Tambua kuwa waliomuona siku ya tukio walimtambua. Muhimu zaidi ni kuwa Mungu anamjua vizuri kabisa. Ikiwa alijituma au alitumwa, kama kweli hajulikani au analindwa, Mungu yupo atashughulika na kila anayehusika. Mungu si mjomba wao.

Unaweza kuwa na madaraka makubwa ukadhani umemamiliza, kumbe Mungu amekupa cheo ili kuudhihirisha uovu wako kwa watu. Kama alivyowadhihirisha Jean-Bédel Bokassa Afrika ya Kati, Mobutu Sese Seko DRC, Mengistu Haile Mariam Ethiopia na wengine.

Maana ya hapo ni kuwa cheo ni majaribu makubwa mno. Unakuwa na nguvu kuliko wengine. Ukizitumia kuonea watu na mwisho wako huwa mbaya. Ni kwa sababu Mungu hajawahi kuwa na utaratibu wa kuwachekea wenye kumwaga damu za watu. Mungu hulipa taslimu.

DHAMBI HAIKIMBIWI

Harrison ni jaji, usiku mmoja akiendesha gari, taa ilimulika gizani na kuwaona watu wakimuua mwenzao. Bahati nzuri aliwatambua wote. Aliyeuawa ni James, wauaji walikuwa watatu, Larry, Jaden na Chris.

Baada ya wiki moja Harrison akiwa kazini alipangiwa kusikiliza kesi ya mauji ya James. Mtuhumiwa aliyeletwa mbele yake ni Jorum. Kumbuka kuwa Harrison kama jaji aliwaona wauaji. Lakini maadili ya kazi yake hayamtaki kusema alichokiona, isipokuwa kutoa hukumu kutokana na matokeo ya mwenendo wa kesi.

Kesi ilipofika wakati wa ushahidi, vilitolewa vielelezo vyenye nguvu kabisa kuonesha wazi Jorum ndiye aliyehusika na mauji. Mpaka ushahidi unakamilika hakukuwa na namna yoyote ya kumuokoa Jorum na hukumu ya kifo kutokana na mauaji ya James.

Harrison akawa anaumia mno, maana yeye aliwaona wauaji na anawajua. Anafahamu fika kuwa James hakuhusika na mauaji yale. Kilichomuumiza Harrison ni kuona kuwa anakwenda kumpa mtu adhabu ambayo hakuwa na hatia nayo. Ushahidi ulitengenezwa na umethibitisha kuwa Jorum ndiye alimuua James.

Siku moja kabla ya hukumu, Harrison alikuwa mwenye mawazo mno. Hukumu ya Jorum ilimtesa hasa. Mwisho aliamua kwenda gerezani ambako Jorum alikuwa amewekwa mahabusu.

Harrison akamwambia Jorum: "Najua kabisa wewe siye uliyemuua James".

Jorum akajibu: "Ni kweli mheshimiwa, mimi naonewa. Hii kesi imetengenezwa".

Harrison aliwaza kisha akamuuliza Jorum: "Bila kunificha kabisa, kabla ya tukio hili, wewe huko nyuma umewahi kuua?"

Jorum: "Ni kweli niliwahi kuua zamani lakini hakuna aliyejua".

Harrison akasema:"Basi hukumu ya kesho nitaitoa kwa ajili ya yale mauaji ambayo uliua na hukujulikana. Nilikuwa napata shida kumhukumu mtu asiye na hatia, kumbe hatia unayo".

Ndimi Luqman MALOTO
 
Rooney

JF-Expert Member
Jan 16, 2015
3,709
2,000
Apo kwa Noriega...km usa ndo walsapot na aoao wakamtupa jela...vp malipo yao usa mbona wanapeta tu
 
AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
1,893
2,000
sawa,je kama kilichotokea kwa hao wahusika hapo juu,amin ,lissu,ben saanane na hao waliokufa kibiti na wanaookotwa bahaini wakiwa wamekuufa ni sehemu ya malipo yao kwa mungu,kuwa nao kuna mammbo ya sirini kama hayo waliyafanya au walishii sasa ni malipizo kwao ,hapo napo tunasemaje?

Nadhani muandishi pamoja na andiko zuri amejitahidi kuingilia uhuru na kazi ya mungu ya kuhukumu,(najua nitakuwa nimewaumiza mashabiki wa lissu,ila kumbuka nimeanza na neno KAMA coz hakuna ajuaye siri za mwingine )
 
sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,496

Ni somo zuri mno
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom