Kupigwa marufuku mazao kwenda nchi jirani

gmail mkulima

Senior Member
Jun 11, 2017
187
250
Wakuu naomba kuliza hii marufuku iliyopigwa mazao kwenda nchi jirani imekaaje, je ni mazao aina yote au ni badhi.
 

Goldman

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
1,831
2,000
Yaani kulima nilime mimi, mbolea ninunue mimi shamba ninunue mimi, halafu wakati navuna ili niuze mnanipangia! Kweli mkulima hawezi toboa maisha haya!
 

Kingdavi.ii

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,182
2,000
Kama ni kweli badi wakulima watakuwa wanageuzwa watumwa wa serikali sababu
Hawapewi ruzuku za kutisha na zinazotolewa wanafaidi viongozi wahalmashauri na seikali kwa ujumla pia viongozi wa ccm na naafisa watendaji.

Gharama za viwatilifu , mbolea na dhana za kilimo ni ghali sana hibyo mkulima kubebeshwa mzigo mkubwa sana.

Wakulima kupangiwa bei za mazao kama mahindi, kahawa , pamba na tumbaku ni jambo baya sana , na hii inatokana na watu wenye mitaji mikubwa ni viongozi wa serikali na wafanya biashara ndani ya serikali nfiyo wanasababisha haya yote.
Ni vyema mkulima awe huru kuuza mazao popote ili aweze kupata faida na hii itawavutia wengi kujiingiza kwenye kilimo la sivyo vijana wataendele kukimnia kilimo mfano bei ya mahindi DRC ni 3times ya tz kwanini wakulima wasipewe haki yao.
Pia srrjali iwe mfanomzuri kernye kilimo kwa kuacha kuingiza siasa za kibaguzi mfano kubomoa shamba la bwana Mbowe hii haileti piha nzuri kwa jamii ambayo inaaminishwa kilimo ni uti wa mgongo.
Kilimo kianze kufundishwa kuanzia ptimary kama zamani ili kuwaandaa mindset za watoto kuwa kilimo ni kazi inayolipa kwa 100% kwani wengi wanaamini kilimo kama ni adhabu na siyo kazi

Sera ya ardhi inamapungufu makubwa kwani hakuna mipango ardhi mizuri.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
81,993
2,000
Hawana haki ya kuzuia mazao ya mtu yeyote kwenda popote , serikali ilishasema hakuna chakula cha bure kwa mtanzania yeyote , sasa wasiwasi unatoka wapi ?

Serikali ambayo imeshindwa kulipia karo za watoto wetu wa vyuo inatuzuia kutafuta ada za wanetu ili iweje ?

Shamba likiwa na bangi ni lako lakini likiwa na dhahabu au mahindi serikali inaingilia ili iweje ?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom