Kupigwa, kudhalilishwa na Kunyanyasika kwenye Mahusiano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupigwa, kudhalilishwa na Kunyanyasika kwenye Mahusiano

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Serenity, Aug 7, 2012.

 1. S

  Serenity New Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jambo Wanajamii. Ninaandika kwa masikitiko makubwa na majonzi, na stori yangu ni ya manyanyasiko makubwa.

  Nimekuwa kwenye relationship huu mwaka wa 5 na huu mwaka wa pili nimekaa na huyu mwanamume as wife. Tuna watoto 2. Jamani nimepitia matatizo meeeeeeeeeengi na nimekuwa navumilia tu. Na mimi ndo nimekuwa nahangaika na kibarua changu kusupport familia. Amenipiga mara mbili vibaya tu, na hata mtoto wangu mkubwa akishuhudia.

  Mara ya pili akamwita mama yake ambaye alinisimanga na kunitolea maneno machafu na hata kunivua kanga mbele za wadogo zangu,mwanangu na mkwelima wake. Mwisho walinifukuza na watoto usiku. Hata ninapoandika hapa sina sehemu ya kukaa naomba kujiegesha tu kwa ndugu. Baada ya siku moja akanifuata kuomba msamaha, mimi roho bado nzito. Siku 2 hazijapita akanitumia matusi ambayo si heshima kuandika hapa jamvini na hata kunionesha jinsi anavyobadilisha wanawake na kwamba nisipige jungu atamchukua mwanamke mwingine.

  Jamani sina amani na nimekuja kuwachukia saaaaaaaaaaaana wanaume. Nimeondoka na wanangu na sitaki hata wamjue baba yao maana kanifanyia unyama. Wadau naombeni ushauri. Mdogo ana miezi 5 na wamenifukuza usiku.

  Natanguliza shukrani.
   
 2. Nambe

  Nambe JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 1,455
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  pole dada.................
   
 3. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Pole sana Serenity.
  Kukunyanyasa kote huko na kukufukuza usiku pamoja na watoto ni kwa sababu ya wanawake au kuna la zaidi?
  Kweli kama kuna mbingu baadhi ya wanaume hawataiona!!!!
  Hivi inakuwaje mke uoe mwenyewe kwa hiari yako halafu baada ya muda unamnyanyasa na kumsimanga??!
  Yaliyokukuta Serenity pia yalimkuta dada angu mkubwa! Dada ndio sole bread winner, ada za shule, matibabu n.k. Mume yeye busy na vimada maswala ya familia hayakumuhusu kabisa. Kilichotuumiza zaidi kama familia ni vipigo vya mbwa mwizi kwa dada yetu. Kwa sasa dada yuko nyumbani na anaendelea kutunza familia yake ilhali mumewe hana hajualo!
  Sikutegemea kuleta hii stori hapa ila nimeguswa sana na masaibu ya dada Serenity.
  Mungu akupe nguvu pia sikiliza zaidi moyo wako. Mateso unayoyapata mwenyewe ndio wayajua hivyo uamuzi ni juu yako either ku-settle the matter au kuchapa lapa.
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Huyo ni wife beater na hata acha na ipo siku atakuumiza uwe kilema au hata mauti yakukute. Kaa mbali sana nae, mwanaume anayepiga mke wake mbele ya watoto au ndugu huyo sio mwanaume.
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Pole sana ila wewe unaonekana ni mkongwe humu jamvini ila umeamua kufungua ID nyingine kwa manufaa yako
  Join Date : 7th August 2012
  Posts : 1
  Rep Power : 0
  Likes Received 0
  Likes Given 0

  Usiwachukie wanaume maana huenda ndo wakakusaidia pia
  Sasa Mnaanzaje kuzaa na hamjafunga ndoa?
  Tena watoto wawili , je sababu gani anakubonda huenda nawe una tabia inayomkera?
  Sema tatizo maana hapo umeeleza matokeao baada ya tatizo, Eleza tatizo linayosababisha ugomvi!!
   
 6. sakapal

  sakapal JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,824
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Pole sana dada lol! kwa hapa lazima uone wanaume kama wanyama wasiohitaji kuhurumiwa hata, lol pole sana.
  Kwanza source ya ugomvi wenu ni nn? hadi hapo ulipo una amani au bado unatamani kurudi kwenye mahusiano yako?
  Je unafikiri unaweza kuyamudu maisha yako mwenyewe na kuwatunza watoto wako mwenyewe ukiwa kama baba na mama?
  Kama ndivyo basi vumilia tu huu mpito na tafuta mahali pa kupanga chumba kimoja kinakutosha, uwe na mfanyakazi ambaye ataangalia watoto wako wakati unatafuta shekeli na usiyumbishwe na wanaume kwa kipindi hiki hadi uwe stable especially kwa watoto wako.
  Hapa jamvini tafuta ushauri tuu ila ukitafuta hifadhi ya kukaa unatafuta mimba nyingine au kadhaa, aidha waweza tafuta vikundi vya mikopo uanze maisha mapya.
  Ni ngumu kuanza ila ukifanikiwa belive me hamna mtu atakusumbua maishani na utaweza kuishi maisha yoyote yale ya hali ya chini hata ya juu.
  Kama unawazazi na uko nao vizuri waweza omba msaada wao au ndugu au jamaa watakusaidia vizuri kwa ukaribu na upendo wa kweli kuliko marafiki watakao taka kufaidika na shida zako.
   
 7. Gold

  Gold Member

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana,jipe moyo bt huyo c wako jitahd umsahau na uendelee na maisha yako kwn Mungu hamtup mja wake atakuafu 2 jipe moyo
   
 8. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Kila mara huwa nawaambia dada zangu mapenzi yawe kitu cha mwisho. Yaani, elimu, uchumi halafu mapenzi, ukiwa na elimu na uchumi bora huwezi kamwe kunyanyasika ktk mahusiano. Kama hisia za ngono zinajaa mwilini unatafuta msela anazipunguza kama tunavyofanya sisi wanaume wakati tukiwa tunasubiri mambo yawe safi. Maisha ni mahesabu.
   
 9. salito

  salito JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  Ebo?acha nishangae kwanza na kutafuta cha kusema
   
 10. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Pole dada.

  Katika maisha ya ndoa mambo hayo ni mapito na sio wewe tu unayepitia majaribu hayo. Jipe moyo, achana na huyo mwanaume na pigania future ya watoto wako. Tambua kwamba hapa duniani binaadamu wanaweza kukudhalilisha na kukuchukia as much as they can ila NI MUNGU PEKEE AMBAYE KAMWE HAWEZI KUKUCHUKIA, KUKUDHALILISHA NA KUKUDHARAU! Mtazame yeye na mtegemee yeye na hakika atakuinua.
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  Tukushauri nini dada?
  Umefanya uamuzi wa busaara wa kuondoka, mali na pesa zinatafutwa lakini maisha hayatafutwi.....

  Nenda kaanze upya maisha yako, mwanaume ambaye ni abusive huwa haachi, mbaya zaidi mkweo nae mkorofi, hutopata amani kwenye hiyo ndoa/nyumba.

  Huyo mwanaume hafai, hafai usirudi nyumba, mwanaume anapiga, anakudharau na kukutukana wa nini? Heri uwe single....

  Mungu amemuumba binbadamu na moyo wa kusamehe, in time utasahau na utafungua moyo wako....in time utapenda tena, kwa sasa songa mbele na wanao na maisha yako........
   
 12. Arabela

  Arabela JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 3,253
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Pole sn kwa matatizo.. Kama nyumbani kuna nafasi ya kurudi bora urudi na kama wazazi hawakuridhia kuwa na huyo baba watoto hilo litakuwa tatizo.. Ila me mwanamke mwinzio nkuhakikishie sio wanaume wote wabaya. Pole sana amini Mungu yupo nawe anza maisha yako na utasimama tu
   
 13. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #13
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Umenikumbusha utoto wangu .. Samahani sintoweza
  Kuchangia zaidi.. Very sensitive topic .
   
 14. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #14
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Pole sana dada.
  Aksante Badili Tabia, I couldn't say more.
   
 15. Little Angel

  Little Angel JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Pole sana dada. for five years uliishi uki hope kuwa atachange au? as loong as unaweza kulea watoto wako songa mbele mama. maisha ni mafupi sana kwann upate shida hivyo. sali sana MUNGU atakupa njia.
   
 16. LD

  LD JF-Expert Member

  #16
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Labda nitajitahidi kuvumilia manyanyaso ya huko kwenye ndoa...lakini SIO KUPIGWA!! kUPIGWA? UNANIPIGA kwa kipi HASA? UMEONGEA KWA MDOMO UMESHINDWA UNAONA UNIBONDE? Kulaaaleki siku mtu ananyanyua Mkono wake ana anipiga NI KWAHERI. HATA KAMA NINA WATOTO KUMI.

  Weeeeeeh...............Kupigwa? Upo tu, unasubiri akuue? Siku atakubonda shoka kichwani mbele ya watoto wako UNAKUFA hapo hapo. STAKI JITU LA JINSI HIYO..................LISHINDWE NA LILEGEEEEEEE KATIKA JINA LA MITUME WOTE WA MUNGU.....Mi sijui Ashindweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 17. LD

  LD JF-Expert Member

  #17
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kilimanjaro Revival Choir - Upendo Wa Mungu - Agape (OFFICIAL VIDEO) - YouTube
   
 18. S

  Starn JF-Expert Member

  #18
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 400
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Pole sana dada, ila inakubidi usiwachuke wanaume kwani mtu mmoja wapo aliyechangia mwanaume huyu kukuchukia ni mama wa mwanaume ambaye umekuwa ukilalamika kwamba amekuwa anakunyanyasa pia kwa mujibu wako mama wa mwanaume alikuwa ni mmoja wa mtu ambaye alikufukuza usiku.

  Kuwaondoa watoto maishani baba yao ni kuwaadhibu kupitia makosa ya baba yao, kwa ushauri wangu waruhusu watoto wamjue baba yao kama akiwakubali kuwakataa hiyo ni juu yake, watoto watamuhukumu wenyewe badala ya kuja kukuhukumu wewe kwasababu ya kuwaweka mbali na baba yao.
   
 19. felinda

  felinda JF-Expert Member

  #19
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 351
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  pole dia kwa hivyo vipigo,,,,,,,kama unaweza kuwalea wanao better uendelee na maisha yako achana nae wanaume sio watu ma dia,
   
 20. Bushloiaz

  Bushloiaz JF-Expert Member

  #20
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kuna wanaume huku duniani wanafanya wanaume tuonekane kama mashetani vile,hivi nakuwaje mtu anakuzalia watoto,anakutreat vizuri then unamfanyia vituko?
   
Loading...