Kupigwa Dr Ulimboka. Kwa nini polisi mnang'ang'ana na tume yenu? Kuna kitu mnataka kufunika. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupigwa Dr Ulimboka. Kwa nini polisi mnang'ang'ana na tume yenu? Kuna kitu mnataka kufunika.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jun 30, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Watanzania wapenda haki ambayo ni rutubisho la amani - tupinge kwa nguvu zote ile tume ya akina Kova. Kwa kuwa kumeisha ingia doa la kwa polisi kushukiwa mkono wake, basi ni bora wajiondoe kupisha tume huru iundwe. Wakikataa tupeleke petition mahakamani ili izuiwe.

  Sababu yao ya kung'ang'ania ni nini?
   
 2. Root

  Root JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,319
  Likes Received: 13,025
  Trophy Points: 280
  wanang'ang'ania ili wafunike
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Waziri wa ulinzi ajiuzuru kwanza kwa wananchi kukosa imani na watu wake
   
 4. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Mikono ya sakari wa jeshi la polisi pamoja na vitengo vingine vya dola (mihimili mikuu) ni michafu. Sakata zima la mgomo wa madaktari vinaonyesha udhaifu wa kiasi kikubwa wa watendaji wakuu wa serikali. Kukosekana kwa huduma muhimu kwenye hospitaliu zetu ni ukweli usiofichika, na ndiyo mahali wakubwa wanapopatia ulaji wao. Ieleweke ya kwamba wao wakiugua hupelekwa nje ya nchi, kwa hiyo hawajali kabisa wala hawana nia ya kutaka kujua mtanzania wa kawaida anaishi vipi na huduma za afya anazipataje. Hapo hapo, watanzania wachache wenye 'uwezo' wa kwenda India kwa matibabu, wanakwenda huko kupitia migongo ya viongozi hao hao. Kuna vibali kadhaa ambavyo mtu anatakiwa avipate kabla hajaweza kusafiri kwenda kutibiwa huko. Na hivyo vibali havitoki bure. Kwa mantiki hii kuboresha huduma za afya nchini kutaathiri ulaji na maslahi ambayo wanayapata kutokana na hali mbaya za huduma za afya.

  Mgomo wa madaktari ulipokuwa unapoendelea watu wa kawaida wakaanza kuelewa ukweli wa mambo, na kuibana serikali itafute ufumbuzi. Dola ilibidi iingilie kati ili kujilinda na kulinda maslahi ya viongozi. Vyombo vyote vya dola kama jeshi la polisi, mahakama, usalama wa Taifa vimeshirikiana ili kuwafumba midomo watu wote wanaopiga kelele. Dr. Ulimboka alionekana kuwa sauti ya wanyonge, na walitaka kumnyamazisha kwa njia yoyote ile. Sasa kwa kuwa azma yao haijatimia, wanajaribu kufunika ili kile kinachojulikana waweze kukigeuza na kutoa tamko lao kama walivyopanga wenyewe.

  Inasikitisha sana lakini ukweli ni kwamba tumefika pabaya sana! Ila wafahamu ya kwamba wamelikoroga, na sasa KIMENUKA!!!
   
Loading...