Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Tumeshuhudia Serikali zetu zinavyoendesha vita dhidi ya madawa ya kulevya ili kunusuru nguvu kazi ya Taifa. Lakini kwa bahati mbaya tumelipa kisogo tatizo na adui mkubwa wa afya kwa jamii yetu linalotokana na Tumbaku.
Hata kitakwimu,Tanzania kuna watumiaji wengi wa Tumbaku kuliko madawa ya Kulevya; kwa nini basi tupoteze nguvu nyingi kwa madawa haya ya kulevya tuka acha adui mkubwa wa afya zetu Tumbaku azidi " kutanua"
Hivi kama Tanzania ingelikuwa inazalisha Cocaine, je vita hivi ingekuwepo? Nini maudhui hasa ya kupiga marufuku madawa ya kulevya huku tunaongeza pembejeo, motisha na kila msaada kuongeza mavuno ya zao hili hatari kwa afya kwa binadamu?
Tusijjifanye kama Tembo, kuwaonesha umma kuwa tunajisafisha kumbe tunazidi kujipaka matope! Tutafakari na tuchukue hatua.