Kupiga picha na watu maarufu, kunakuongezea vipi, unafuu katika maisha yako?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,270
40,087
Watu wengi hupenda, au kulazimisha kupiga picha na watu maarufu katika nyanja mbali mbali.

Leo tunataka tujiulize; zile picha huwa zinamanufaa gani katika maisha yako; hasa katika utafutaji wa kipato chako cha kila siku.
 
Kiuchumi huwa haziongezi Wala kupunguza kitu. Lakini kiroho unakua na amani Sana na kujiona umefanikiaa Jambo kubwa maishani mwako. Unajua sometimes unaweza kupigwa na maisha lakini ukiangalia picha enzi ukiwa njema unafarijika na kujiona utawini tu.
Nina picha nikiwa na J.M.Kikwete ilipigwa 2017 wakati wa graduation pale MUCE, Kila nikiiangalia huwa natamani nikamwambie unaiona hii picha tangu tupige Ile siku sijaajiriwa.
 
utapeli tu............................................oooooooh njoo nikufanyie connection si unacheki hii picha nipo na ummy mwalimu
 
Hutumika kujiliwaza kwamba katika maisha mpiga picha na kiongozi na yeye alifahamika.Pia hutumika kufanyia utapeli.Mtu anaonesha picha kwa "wakuja" na kumdamganya huyo kwenye picha ni rafiki yake mkubwa sana,bosi wake au mshirika katika biashara halafu anatumia kutapeli.Hata hivyo, wengine ni "ugonjwa" wao kupenda "selfies" na viongozi tu.Hahahahaaa
 
Hutumika kujiliwaza kwamba katika maisha mpiga picha na kiongozi na yeye alifahamika.Pia hutumika kufanyia utapeli.Mtu anaonesha pita kwa "wakuja" na kumdamganya huyo kwenye picha ni rafiki yake mkubwa sana,bosi wake au mshirika katika biashara halafu anatumia kutapeli.Hata hivyo, wengine ni "ugonjwa" wao kupenda "selfies" na viongozi tu.Hahahahaaa
Mi nilijua labda wanaenda kuchukulia mikopo kwa hizo picha
 
Kiuchumi huwa haziongezi Wala kupunguza kitu. Lakini kiroho unakua na amani Sana na kujiona umefanikiaa Jambo kubwa maishani mwako. Unajua sometimes unaweza kupigwa na maisha lakini ukiangalia picha enzi ukiwa njema unafaeijika na kujiona Imani.
hatari sana mkuu
 
Wengi wanapenda kuuza sura utakuta mtu kapishana hata na let's say TINO anaza kumshobokea picha ili aka post kwenye mitandao ya kijamii .... na wwngine ndo furaha zao ila mimi namini mwanaume kamili hawezi fanya kitu kama hicho hasa sisi tulio toka kanda ya kaskazini hatunaga shobo za dizain hiyo wala pigo hizo hatunaga
 
Inasaidia haswa kwenye social media, mtu akiingia kwenye profile yako na akaona unatembelea au una connection na watu maarufu au wenye pesa au mafanikio yoyote makubwa, automatically na wewe anakuweka kwenye hadhi ya kutokukuchukulia poa haswa kimaslahi

Ila kwa walio wengi ni kumuhusudu Tu celebrity au na yeye aonekane wa mjini...
 
Ni kumbukumbu katika maisha kwani ww unapiga picha ili ikusaidie nini kama hujapata nafasi ya kupiga na mtu maarufu siyo mbaya labda huna nafasi ya kukutana nawo
 
Watu wengi hupenda, au kulazimisha kupiga picha na watu maarufu katika nyanja mbali mbali.

Leo tunataka tujiulize; zile picha huwa zinamanufaa gani katika maisha yako; hasa katika utafutaji wa kipato chako cha kila siku.
1.Just to have memory to the person you love.

2. Creating trust to people in order to scam them easily take example if a scammer can take a picture with Bakhresa,then people will trust him/her and the last thing is to be scammed.

By the way some people don't only want to take pictures with famous people but others will go far to have something signed by them.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom