Kupiga picha/kusambaza picha za majeruhi/Maiti

raia_mwema

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
479
313
Ni jambo la ajabu sana unakuta imetokea ajali au janga ambalo msaada unahitajika lakini unakuta watu waliopo jirani wenye kuweza kutoa msaada wapo busy na simu zao wakichukua picha ili tu wazipeleke katika mitandao ya kijamii.
Pia tabia ya kusambaza picha za majeruhi au maiti sidhani kama lipo sahihi kimaadili.
Ukiingia facebook au status na dp za wasap zinawekwa picha za majeruhi.

Watanzania wenzangu hebu tuache kutumia vibaya sayansi na teknolojia. Linapotokea janga kinachohitajika ni msaada na sio picha..
 
Aisee ni mambo kijinga kwelikweli, kupiga picha maiti au majeruhi bila hata ruhusa maalumu ni ukatili mkubwa wa kijamii na utu, badala ya kutoa msaada unapiga selfie na maiti, ndiyo maana baadhi ya watu huona sheria ya kimtandao ( cyber crime act) ya Tanzania ni kandamizi kwa sababu mambo kama haya ya kupiga na kusambaza picha za watu, maiti, majeruhi n.k hayaruhusiwi kisheria,
jana kuna ajali ilitokea msalala Shinyanga, mijitu mingine inapiga selfie kwenye ajali..ujinga.
 
fece339cba74b9d58bb9dc452d4a256c.jpg
 
Back
Top Bottom