Kupiga Marufuku Kujenga au kuishi Mabondeni siyo Uamuzi Mgumu

spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,599
3,220
GreatThinkers,

Ni katika kusaidia kuwapa fikra hawa wazee wetu, kila kitu wanaogopa hata kutoa tamko na kutekeleza.

Sasa fanyeni yafuatayo.
1.Majengo yote yaliyo bondeni yabomolewe, kipimo kiwe ni pale mafuriko yalipoishia.
2. Serikali iwape viwanja na mahema watu wote walioathirika na kuwapatia chakula cha kuwatosha miezi isiyopungua mitatu(Mfano. Gunia 2 za Mahindi, Gunia 1 Mchele,Gunia 1Maharage, Sukari kilo 50 mali yote hii kutoka chakula cha hifadhi kilichopo)
3. Serikali iwajengee vyoo na kupeleka huduma ya maji
4. Serikali iweke nguzo kama za Road reserve-ziandikwe End of Valley Reserve

Historia.
Mwalimu Nyerere alifanya kitu kama hiki wakati watu wanahamishiwa Mji mwema,Maweni na Gezaulole.
Yule mzee alikuwa si mtu wa porojo bali mtendeji kwa masuala Serious kama haya.

Nawakilisha
 
Umejenga hoja vizuri sana lakini ulivyofika mwisho umechanganya habari kumuweka Nyerere!
 
Kupiga marufuku tu haitatusaidia kama ufuatiliaji na utekelezaji hautafanyika! Magufuli alijitutumua hapa kupambana na ujenzi holela akazodolewa na boss wake mbele ya kadamnasi kuwa apunguze kasi! Unategemea Tibaijuka aseme neno aharibu lipstick yake? Kila mwaka wanajisemesha, yametokea saa hizi wanakunywa kahawa wapi sijui!
 
Mku vema na haki. lakini nakumbuka wakati wa bunge la bajeti kuna mbunge aliongea hadi mapovu yakamtoka kinywani wakati waziri Tibaijuka aliposema kuna mpango wa kuwaondoa watu jangwani! Mbunge akasema hakuna mtu kuondoka wao watabaki hapohapo wakola mihogo ili watu wasiyoke masaki kwenda kujo.pimzisha jangwani huki wakila Ice cream! Sijui sasa.huyo mbunge yuko wapi manake sijasikia kaili yake
 
Tunahitaji serious MEGA-MILIONS TZS worth construction projects kwa ajili ya kuwapa watu ajira, makazi bora, miundo mbinu iliyo imara na inayoendana na kasi ya maendeleo. Hapo jangwani ilitakiwa kuwepo na Highway zinazopishana juu kwa juu na hayo maji yangekuwa yanaonekana kwa chini tena mbali.
 
GreatThinkers,

Kuna mda wa kushauriana na wasaa wa kuamua,

kwa maoni ya ngu huu ni wasaa wa kuamua na kutenda.
 
Mawazo yenu wooote mazuri lakini yanaonekana hayawezi wasaaidia wananchi kwa sasa kwani wakati mkiwaza hamkuwashirikisha.
Maamuzi yao sasa wanafua nguo, kufanya usafi na kuanika magodoro yaani wanarudi makwao. Nyie muendelee na mipango yenu endelevu.
 
Back
Top Bottom