Kupiga kura ni dhihirisho la kujitolea kwetu, sisi kwa sisi, nchi hii na ulimwengu huu.

AbbasTwalb

Member
Oct 15, 2020
13
32
Kuelekea katika tarehe za kupiga kura mimi bado naendelea kuwashawishi vijana wenzangu wa kitanzania kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura ili tuweze kuchagua viongozi tunaowahitaji ili watufanyie mabadiliko katika maeneo yetu tunayoishi.

Kigezo cha kusema mshindi ameshapangwa na NEC sio jambo zuri kwani kufanya ni kuamini kwahiyo basi hata kupiga kura napo ni kuamini yakwamba kiongozi unayeenda kumpigia kura ndiye atakayeibuka mshindi.

Na niwaombe tu NEC pamoja na jeshi la polisi kupunguza kufanya maamuzi yasiyoyalazima au ambayo yatapelekea uvunjifu wa amani katika nchi yetu.

Na pia sisi wananchi tujiepushe na vurugu katika vyumba vya kupigia kura ama pembezoni mwa maeneo hayo kwani tufahamu yakwamba mazuri hayahitaji vurugu ama umwagaji damu na ndio maana hata Mwl Nyerere aliona ni fahari kubwa kwa nchi yetu kupata uhuru bila kumwaga damu.

@abbastwalb
 
Wasiwasi wangu mkubwa ni kuhusu utitiri wa vijana wengi walioandamana kwenye kampeni sina hakika kama wote wmejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi huu ambapo asilimia kubwa ni vijana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 40+
 
Back
Top Bottom