Kupewa mimba siyo yako au kudhulumiwa mimba kipi bora?

Dr criminal

JF-Expert Member
May 16, 2022
2,278
4,268
Out there wakuu,

Hivi kama mwanaume kipi bora, mwanamke apigwe mimba na jamaa huko halafu aje akubambakizie wewe au mimba yako, yani ni wewe umemjaza lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake akaamua akampe jamaa mwingine, kwa wewe kujua, kuhisi au kutokujua kabisa?

Binafsi kwangu yote heri tu, yaani uzito wa mambo hayo mawili kwangu ni sawa tu, mwanamke akinifata ana mimba akasema ni yangu na nililala naye na nilimwagia ndani sina haja ya kutafuta DNA ntalea mimba, akijifungua salama tutalea mtoto. Kwanini?

Kwasababu kwanza, mimi siwezi kushiriki tendo na mwanamke nisiyempenda, siwezi, na kwa kulala na mwanamke ninayempenda huwa sipendi twende kavu (sifurahii na lile limpira, nataka nihisi ngozi yake, lakini hapa lazma nijihakikishie yupo salama).

Huwa nahihikisha kila kitu kipo sawa hususani asiwe kwenye siku zake za hatari, kimsingi hatuna mpango wa mimba na kumwagia nje ikiwezekana. Sasa ikatokea kaniletea habari za mimba, kwanza nakapenda, pili nilikakula kavu , nini kinafuata? Mimba inalelewa bila ubishi.

Pili mwanamke wangu akaja akanambia "Criminal nna mimba yako", nitamwambia twende tukapime, tukienda tukaikuta ni hapo hapo matunzo yanaanza (nikiletewa mimba nahesabu ni yangu, sina muda wa kujipa fikra hasi kwamba huenda mimba siyo yangu).

Mimi nahesabu kama baraka tu, mimi nalea kiumbe cha Mungu kiroho safi tu, maana sijui mwanamke katumia vigezo vipi kunipatia mimi hiyo mimba (kama siyo yangu lakini akaniambia ni yangu), huenda hata ni malaika wamemuelekeza aje kwangu. Kwahiyo kwangu ni baraka kukuza kiumbe cha Mungu, Duniani tunapita tu (ikimbukwe Nabii Mussa alilelewa na farao).

Sasa ikatokea siku kaja mtu kudai mtoto ambaye nimemlea kuanzia mimba, anazaliwa mpaka anakuwa, nitamwambia twende tukapime DNA kwa gharama zake. Akifanana na wewe unasepa naye (sitoitaji hata gharama nilizotumia kumlea mtoto), zikifanana na zangu janja anabaki.

Suala la kudhulumiwa mimba pia nalichukulia tu kama la kupewa mimba siyo yangu (namaanisha ile nimedhulumiwa mimba mimi mwenyewe sijui, maana nikijua lazima nitapigania damu yangu).

Mwanamke kama ameona mimi sifai kuwa baba wa mwanawe au kuna baba bora zaidi yangu, ni sawa tu akampe huyo anayeona ni bora, mimi namtakia tu mwanangu kila la kheri katika malezi na makuzi yake.

Wakuu mi naamini baba na mama ni njia tu ambayo Mungu huitumia ili kiumbe chake kifike Duniani, kifanye alichotumwa kufanye halafu arudi kwa Mungu Baba. Kiufupi Mungu alikuwa na uwezo wa kumfanya yeyote miongoni mwa binadam awe mzazi wako, ila akawachugua hao wawili unaowaita baba na mama.

Kwahiyo tusiweke ugumu mambo, ukiletewa mimba we lea, mwanamke akipeleka mimba yako huko ushuani safi, ila haitobadilika kamwe kuwa wewe ni baba yake. Ile ni njia tu ambayo Mungu aliamua huyo mtoto apite (kwahiyo msilaumu wanawake siku zote).

Ukweli: Mama yako pekee ndiyo anamjua baba yako halisi.

Nikiingia kwenye ndoa tukadumu Kka muda wowote ule, halafu tukazaa watoto wa idadi yeyote ile, halafu baadaye akaja mke wangu kuniambia "Mume wangu, Abdul na Nurath siyo wanao, ni wa jamaa fulani", nitwambia twende tukapime DNA tukikuta kweli ni watoto wa jamaa.

Hapo nitawauliza watoto "Mnataka kwenda kwa baba yenu au mbaki hapa?" Wakisema wanabakii ni amani na upendo, kama hakuna kilichotokea, wakisema wanaenda kwa baba yao, ntawaambia "Kwaherini ila hapa ni nyumbani kwenu, muda wowote mnakaribishwa". Kuhusu mke wangu ntaendelea kumpenda labda yeye mwenyewe aamue kuondoka.

Mnajua kwanini wakuu, mwisho wa siku maisha ni mchezo wa muda, hata kama siutumii muda wangu vizuri basi nahakikisha nautumia kufurahi, hata kama kuna kosa nitafanya leo likija kunigharimu miaka kumi ijayo ntalipokea huku natabasamu, hata kama ukinikosea leo ukaja kuniomba msamaha baada ya miaka 20, wewe jua nilishakusame kitambo. Sina mda wa kujutia ni kujilaumu.

"Kulea mimba siyo mchezo, ba kijacho hujajipanga" -R.O.M.A MKATOLIKI

Kwangu ndiyo hivyo wakuu, niletewe mimba na mwanamke ninayempenda na niliichakata kavu, naihudumia, nidhulumiwe mimba sawa tu, wakelee wengine huko.

Kwako vipi?


#OneDayYouWillBeGone
Dr Criminal

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sex is a transaction, be careful one night sex can cost you to loose your empire or gain a life fortune. Bora kupata kuliko kukosa
 
Yote mabaya tu. Why nipewe mimba isiyo yangu? Na kwanini mimba yangu apewe mtu mwingine?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom