Kupendana kupindukia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupendana kupindukia

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by BAK, Oct 30, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,791
  Likes Received: 83,168
  Trophy Points: 280

  Kuna hili swala la Wanaume na Wanawake ambao wako kwenye mapenzi mazito ndani ya ndoa au katika uBF na uGF wanampenda sana mwenzi wao katika mapenzi kwa kupindukia lakini hawako tayari kumwambia hivyo muhusika ili ajue anapendwa kupindukia badala yake wapo radhi wawaambie ndugu, jamaa na hata marafiki wa muhusika au ndugu, jamaa na marafiki zao. Wengine hudai kwamba muhusika akitamkiwa hivyo kwamba anapendwa kupindukia basi ataanza “kuleta za kuleta”. Hili Waungwana limekaaje? Kwanini kusiwe na uwazi wa kumwambia mpenzi wako kwamba unampenda kupindukia na penzi lake kwako linakufanya ujisike na furaha kupita kiasi? Kwanini akayasikie maneno haya kwamba “Mumeo/Mkeo au BF/GF anakupenda kupindukia” kutoka midomoni kwa ndugu, jamaa na marafiki badala ya wewe muhusika mkuu!? Kulikoni?
   
 2. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hii haijatulia, nadhani haiwezekani; yaani wewe umpende mtu kupindukia tena ni mkeo ama gelifrendi halafu usimwambie uanze kusimulia watu wengine?! Itakuwa ni akili au matope?
  Labda wakati wa kumtokea bado unaona noma kwamba atajua unamzuga, vinginevyo mi siamini kama kuna kityu kama hicho.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Imani hiyo ipo kabisa, si Imani tu, lakini pia na matendo ya watu wengi yanalenga huko, kwamba huwezi kumwambia mke/mume,b/f, g/f kuwa unampenda kupindukia...ukweli kabisa ni kwamba kuna madhara ya kuweka hadharani hali hiyo!

  Watu wengi kabisa tushaona live! Mimi mwenyewe nikiambiwa na Mrembo kwamba ananipenda kuzidi kipimo, basi lazima nimfanyie pozi ili kutikisa kiberiti
  KUMWONYESHA KWAMBA MI NI MZURI, NA MUDA WOWOTE ANAWEZA KUNIKOSA AKINI`MISS-TREAT, hope this is kinda Natural!

  Usipoweka wazi suala hilo kwa mwenza wako, atajua mnapendana kawaida tu, hivyomambo yataenda, japo mioyoni kila mmoja analiwa na penzi la juu mno na lisilopimika!...

  After-all penzi liko moyoni bana, mdomo huweza kudanganya anytime...lol!
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...bi nafsi sikubaliani na msemo huo.

  Kuna mwanadada alikuwa "anasema" anampenda mchumba wake kupita kupindukia kiasi kwamba hata alipo cheat mara nne na wanaume tofauti, na hata pale alipopatwa na ujauzito wa njemba mojawapo kati ya hizo nne, alimsingizia shetani kwa kumpotosha upendo wake wa ukweli kwa yule mchumba wake... yaani si yeye wa kulaumiwa!

  Hakuna kupenda kupita kupindukia bana... usanii tu!
  Sidanganyiki hata akijichora tatoo yangu mwilini mwake!
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Ni bora ubaki kimyaa ukimwambia na yeye akabaini basi anaanza kuusumbua mtima wako.
   
 6. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hapana! ni vyema tena ukasema mpenzi wako aelewe. Hata ,mnapoongea kwenye simu ukimaliza unamalizia na neno "nakupenda" siyo "kwaheri" au "baadaye basi" kama tulivyozowea kiswahili swahili. Ni lazima tuendelee na polite language yetu wa TZ siyo tuogope kusema kinachoufurahisha moyo wetu. Acha kila mmoja akiri sababu ya kuwa na mwenziye. Ili hilo alikumbuke wakati wote na lisiwe neno la kumwambia kila mtu bali mmoja tu! Umpendaye! Bahati mbaya zinapotokea zisiharibu maana ya jambo zuri.
  Ila angalia bill za simu huwa zinaongezeka kidogo maana mwenziyo huwa anataka kukusikia ukilirudia mara kwa mara, hasa unapomalizia kwa sauti ya yenye pozi maalam, ya " asante nakupenda"
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,791
  Likes Received: 83,168
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mbu kupenda kupindukia kupo sana tu pamoja na watu kuzidiwa na mapungufu yao kama binadamu na kutembea nje ya ndoa.

  Mapungufu hayo tuliyonayo kama binadamu ndiyo yaliyomfanya Bill Clinton kusahau cheo chake Kikubwa cha Urais katika Taifa kubwa na kukaribia kupoteza cheo kile baada ya kucheza na Monica Lewinsky. Mapungufu hayo pia ndiyo yanayosababisha idadi kubwa ya mapadri ambao ni watu wenye nafazi za juu kabisa katika jamii zetu kujihusisha na matendo ya kuwalawiti wavulana wadogo au kutembea na wake za watu miongoni mwa waumini wao.

  Miezi michache iliyopita nilisoma ujumbe wa binti mmoja hapa Jamii kwamba hajawahi hata siku moja kutamkiwa na mumewe kwamba "nakupenda sana" lakini alifahamu hivyo kupitia kwa wifi zake ambao walimwambia kwamba kaka yao anampenda sana mkewe. Binti huyo aliandika kwamba pamoja na kuwa alifurahia kusikia hilo lakini angependa kulisikia toka mdomoni mwa mume wake badala ya mawifi zake.

  Kwa maoni yangu kama umo kwenye mapenzi mazito katika ndoa au uBF na uGF hakuna ubaya wowote ule kumfahamisha mwenzio kwamba unampenda sana. Sina uhakika na hili lakini nadhani watu wengi waliokuwa kwenye mapenzi wakiulizwa je mumeo/mkeo/BF/GF unajua anakupenda kiasi gani? Nadhani wengi watajibu kwamba najua ananipenda lakini sijui kiasi gani. Kwa wale ambao wanapendana sana ni vizuri kufahamisha badala ya kusema I love you basi iwe I love you so much au badala ya nakupenda basi iwe nakupenda sana.


  Kumbuka kuchora Tattoo mwilini haina maana mapenzi yenu yatakuwa ni ya milele. Hata wale wanaopendana sana hutokea wakati wakahitilafiana na mapenzi yao yakanyauka lakini haiondoi ule kweli kwamba kuna wakati huyo mpenzi alikupenda sana. Hebu sikiliza maneno mazito haya hapa chini Mkuu.

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=H2BjzHWVFEg&feature=related[/ame]
   
 8. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145

  Nimbaya ati kuonyesha wampenda kupindukia kwa kuwa hujui naye yuko geji kiasi gani. Ni mtazamo tu!!
   
 9. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wasiwasi wangu ni kuwa tuna mapenzi ya kuunga unga sana kwahiyo ukianza kuambiwa nakupenda kupita maelezo unaanza kupata walakini inawezekana hapa wife/husband anaziba gaps nisijue kuwa uko nje anamegwa/anamega. Wakati mwingine kuogopa kuwa kumwambia mtu unampenda kupitiliza ataleta pozi ni kujiogopa mwenyewe tu hakuna uhakika kwa hilo ingawa exceptional ipo pia.
   
 10. M

  Msindima JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu umenena,naunga mkono hoja.
   
 11. GP

  GP JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  uko sawa kabisa mkuu kwa 200%, akijua anapendwa atakusumbua sanaaaaaa.
   
 12. M

  Msindima JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  No Fidel ni vizuri kumwambia,na si wote wenye hiyo tabia,yaani nijue unanipenda halafu nianze kukusumbua,na kwanza ninakusumbua ili nipate nini?
   
 13. M

  Msindima JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  No George,sio wote wasumbufu,ni baadhi tu,kwa hiyo kama unam-feel mtu mwambie tu.
   
 14. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  kimya kimya ndio mwendo.
  Ukisema kwanza utaonekana msanii tu huna lolote .na pia utakula vituko mpaka dunia yote itajuwa na mwisho wa yote unakuwa BUSHOKE,....!!
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Bora umzoesha mtu wako kumwambia...
  Bora azoee lugha hiyo kutoka kwako maana akija kuisikia kwingine utajuuuuuuta!
  Binafsi napenda sana kumwambia mtu wangu ninavyompenda.... napenda kumfanya ajisikie ni mtu muhimu sana kwenye maisha yangu.... na hata mie hufurahi kuliko kitu chochote nisikiapo akiniambia maneno hayo....Bahati nzuri tumezoea na tumezoeshana kuambiana.Hakuna anayeshikwa na wasiwasi ati mwenzie atamtesa kwa vile kajua anapendwa.

  Uwazi katika mapenzi ni silaha ya kulinda penzi lenu.
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Nov 5, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,791
  Likes Received: 83,168
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni bahati iliyoje kuwa katika mapenzi ya hali ya juu kiasi hicho Majina yenu ya kwanza au mama Fulani/Baba fulani hupotea na kuitana mpenzi, sweetlove, darling, honey, My Universe etc na wala msiwe na wasiwasi kwamba kuonyeshana mapenzi yenu kiasi hicho basi mmoja anaweza kutaka kumuumiza/kumtesa mwenzake kwa kujua anapendwa sana.

  Mnaambiana maneno matamu kama haya: Mpenzi unajisikia kula nini leo? Ohh! my darling we tengeneza chochote tu ambacho unaona hakitachukua muda mrefu maana najua umechoka, jamani sweetlove sijachoka kiasi hicho naweza kukutengenezea chapati nne, hapana mpenzi chapati tutakula weekend. Ni raha tupu kila siku mnakuwa kama mko peponi na matabasamu yenye nguvu na furaha tele moyoni. Hongera zenu! Mjitahidi mlitunze penzi lenu kwa kila hali maana katika dunia ya leo mapenzi ya juu kiasi hicho ni adimu mno kuyapata.

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=9CkKuA86Mis[/ame]
   
 17. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #17
  Nov 5, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Kama unampenda mwambie ukweli nakupenda hakuna haja ya kuficha, sema kitu ile roho inataka .
   
 18. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #18
  Nov 5, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ukiangalia mabandiko/mada nyingi zinazoletwa jamvini mara kwa mara, malalamiko mengi yanahusu jinsi uhusiano unavyozorota siku hadi siku .Mara ohh mtu wangu ananuna, hanisemeshi. Mara Ohh siku hizi hanipi nanihii... kwanini haya yote yasikupate ikiwa wewe una ububu kwa mwenzio?

  Upendo ulio nao umeuficha moyoni na kufanya siri yako.Mwenzio ataona ishara gani ya kumvuta kwako? Ni hizi tabia za kufichaficha zinazopelekea wajuzi wa mambo kucheza na weakness yako... watamwambia mtu wako "umependeza leo", mara "una tabasamu zuri"... mwishowe ataambiwa "NAKUPENDA"! Hili kwake litakuwa neno lenye miujiza... neno ambalo mara ya mwisho kulisikia ni mwaka 47!

  Jamani acheni kuathiriwa na maneno ya nyimbo za bongo fleva sijui mume *****... na nyingine.

  Halafu pia msisikilize maneno ya watu..mwenzio anakudanganya mimi simtamkii mtu wangu kuwa nampenda... kumbe kila dakika hayo ndio maneno yanayomtoka mdomoni.

  Kwenye mapenzi usimsikilize mtu bali moyo wako. AKILI KICHWANI MWAKO.
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Nov 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,791
  Likes Received: 83,168
  Trophy Points: 280
  Sema VeraCity Sema! Halafu ukishaporwa mtu wako ndiyo unaanza kuwaambia watu tena kwa majonzi nilimpenda sana mke/mume wangu sijui kwanini kanifanyia hivi.

  Ulikuwa wapi siku zote usimwambie maneno ya kumtoa nyoka pangoni mpaka umeshaporwa ndiyo unatamka hadharani ati ulimpenda mtu wako! Too little too late! wajanja wanaojua kupenda tena kwa maneno ya kumtoa nyoka pangoni wameshakuzidi kete! WE URIE TU!
   
 20. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #20
  Nov 13, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu BAK,
  Umeleta mada nzuri sana hapa jamvini. Nitawapa mfano wangu binafsi. Karibu kila siku tuinaambizana maneno - nakupenda, na yanatoka moyoni. Kila mtu anajua mwenzie anampenda, kwa sababu feedback hutolewa na kila mmoja na pia hisia za kupendwa unazipata. Hakuna anayemringia mwenzie hata siku moja, heshima iko pale pale siku zote. Na mkitaka mapenzi ni ya miaka mingapi - zaidid ya kumi.
  Waambieni wapenzi wenu mnawapenda, msiposema wataambiwa huko nje itakuwa balaa.
   
Loading...