Kupenda Kutukuzwa ni laana, na kupenda kutukuza ni unafiki

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Mwalimu Nyerere, wakati wa Urais wake, kati ya vitu alivyowahi kukemea kabisa ni kumtukuza. Alikataa kuitwa MTUKUFU RAIS, alikataa kuitwa MHESHIMIWA.

Mwalimu wakati wote wa uhai wake, na wakati wa Urais wake, aliitwa NDUGU RAIS. Kutokana na yeye kukataa kuitwa MTUKUFU au MHESHIMIWA, hakuna Waziri au Mbunge, DC au RC aliyeitwa MHESHIMIWA. Mwalimu daima alisimama kwenye kauli ya TANU, sisi sote ni NDUGU na AFRIKA NI MOJA.

Shetani wa kupenda kutukuza na kutukuzwa aliingia kipinda cha Rais Mwinyi, na sisi tukamkubali, tukampokea na tukaamua kuishi naye.

Wakati wa Mwinyi, ndipo wabunge wakiwa wamekaa Dodoma, wakapitisha neno "MHESHIMIWA" kwa wabunge, na "MTUKUFU", kwa Rais. Wananchi walishangaa sana, na minong'ono ikawa mingi dhidi ya wabunge. Nao kwa hila, wakajitahidi kufafanua kuwa kinachoitwa MHESHIMIWA, siyo mtu bali ni nafasi ile ya kuwawakilisha wananchi, kwa hiyo UHESHIMIWA ule ulikuwa ni wa wananchi. Wakatoa maelezo ya namna ile ile tukwa neno MTUKUFU RAIS. Lakini ulikuwa ni uwongo. Sababu kubwa ilikuwa ni kutafuta namna ya kusifiwa, wakidai kuwa wenzao wa KENYA wanaitwa WAHESHIMIWA WABUNGE, na Rais wa Kenya anaitwa MTUKUFU RAIS DANIEL ARAP MOI.

Siku zote, kwa wale wote tunaomwamini Mungu, ukiwa na cheo, utajiri au umaarufu fulani, shetani anapokuingia, anatumia nafasi yako, upende kusifiwa na kuabudiwa, ili uanguke katika dhambi iliyo kuu.

Shetani alitupwa jehanamu baada ya yeye kutaka kusifiwa kama anavyosifiwa Mungu. Kwa hiyo shetani kwa kuwatumia mawakala wake waliopo Duniani watamwangusha katika dhambi iliyo kuu kiongozi au tajiri kwa kumsifia ili na yeye aone anakaribia utukufu alio nao Mungu.

Jambo hili tulilishuhudia wakati wa utawala wa Hayati Rais Magufuli. Mawakala wa shetani walimpamba, wengine wakamwita ni Mungu (ref. Kabudi), wengine walimfanisha na Yesu (Lugola), wengine walitamka kuwa Mungu anatakiwa kumshukuru Magufuli (Mwanri). Hii ilikuwa ni kufuru kubwa. Bahati mbaya Rais Magufuli hakuwahi kukemea maajenti hawa wa shetani, akakubali kufanishwa na Mungu. Hii ilikuwa ni bahati mbaya sana kwake. Mungu hakumtupa jehanamu Lucifer kwa koísa jingine lolote, bali kwa kutaka kusifiwa na kufananishwa na Mungu.

Mawakala hawa wa shetani wapo kazini, maana shetani halali usiku wala mchana, yupo kazini. Kama walivyofanikiwa kumdondosha katika laana iliyokuwa kuu Rais Magufuli, ndivyo wanavyofanya kwa Samia. Je, Samia ataanguka katika kufuru au atajitenga, mimi sijui. Lakini dalili za mwanzo, naye inaonekana anakubali kutukuzwa. Leo kila kitu kinachofanywa na Serikali, kinatajwa kuwa Rais Samia amefanya. Naye anaona ni sawa. Akumbuke, shetani huanzia mbali ili anapokufikia awe amemaliza kazi.

Rais Samia, jitenge na laana, jitenge na kufuru dhidi ya Mungu. Wewe ni mwanadamu, na wala Urais wako haujakuongezea hata nukta moja katika ubinadamu wako. Ujawa mtakatifu, bali uutafute utakatifu kupitia nafasi uliyoipata. Ujitahidi kuitafuta iliyo haki. Mpaka sasa, hata kwa jicho la kibinadamu, upo katika laana. Maana dhuluma dhidi ya yeyote asiye na hatia, nawe ukamtengenezea hatia, ili umtende kama vile utakavyo, unabeba laana. Laana hizi zitakuandama kwa namna uijuayo na usiyo ijuo.

Uombe kujaliwa hata chhe ndogo ya hekima ili upate kufunuliwa juu ya yaliyofichika mbeleni pako.

Maana siku zote, kimwangushacho mtu ni mazingira yake. Wanaokuzunguka ndio watakaokutia aibu au kukung'arisha. Watakaokudondosha ni wanaokutafutia sifa za kukutukuza wakati huna utukufu. Watakaokung'arisha ni wale waunenao ukweli, wanaokukumbusha daima kuwa wewe ni mwanadamu, wewe ni mavumbi, huna ubinadamu wowote zaidi ya wengine, hata kama wewe ni Rais.

Shetani alifurahi kwa kuwa mawakala wake walifanikiwa kumwangusha kiongozi wetu aliyepita maana aangukapo mtawala, huanguka na kundi kubwa.
 
Hakuna binadamu asiyependa kutukuzwa awe mbunge au mchungaji,padre ,askofu ,mbunge,shehe nk au mtu wa kawaida ndio maana hata maaskofu husujudiwa watu wanapobusu Pete yake hupiga magoti kuibusu

Na hupenda kuitwa Baba Askofu,baba padre au Baba mchungaji wakati hawakuwazaa
 
...kubudi aliwahi kumuita jiwe mungu
Hayo yake ni imani yake

Kuna watu imani zao huabudu miti,mawe,mito nk wahindi huabudu ngombe huwezi zuia mtu mwenye imani ya kuabudu mawe asiite jiwe Mungu !!
 
Mawakala wa Shetani bado hamjaisha tu,NA ALAANIWE MTU AMTEGEMEAYE MWANADAMU.
Viongozi wa dini pia hutegemea wanadamu Kwa sadaka ili waishi makanisa mengine kama hutoi sadaka au mafungu ya Kumi wanakutimua au hupati huduma za kikanisa!!

Watoao sadaka sana huheshimika mno hata kama ni wadhambi wakubwa je huko sio kutegemea wanadamu huko? Basi kama kulaaniwa viongozi wengi wa dini watakuwa wanaongoza kwa kulaaniwa sababu waumini hutegemea Ajira,biashara zao ,kilimo nk ila wao viongozi wa dini ndio hutegemea wanadamu hugo mstari wa walaaniwa wategemea binadamu wapekee viongozi wa dini ndio unawahusu kwa asilimia kubwa

Ahame hata muumini tu mwenye uwezo aende kwingine au imani ingine uone wanavyobweka kuchukuliwa kondoo wao aliyekuwa akiwapa kipato!!! Tegemeo Lao la kibinadamu!!!
 
Kuna uzu hivi ulianzishwa na chawa wa huyu Mama basi ID za hyo mtu nduo zilikua zinachangia uzi ule.

Ila machawa wa huyu mama nao wapo wengi kama enzi zile nchi iko mateka.
 
Hayo yake ni imani yake

Kuna watu imani zao huabudu miti,mawe,mito nk wahindi huabudu ngombe huwezi zuia mtu mwenye imani ya kuabudu mawe asiite jiwe Mungu !!
Hueleweki unatetea nini, unapuyanga tu. Hapa unasema hivi pale unasema vile
 
Kuna uzu hivi ulianzishwa na chawa wa huyu Mama basi ID za hyo mtu nduo zilikua zinachangia uzi ule.

Ila machawa wa huyu mama nao wapo wengi kama enzi zile nchi iko mateka.
Hawa wanaoitwa machawa, wengine hawajitambui. Wanadhani kuwa kwa kumtukuza Rais wanakuwa wafuasi waaminifu wa mtawala, lakini ukweli ni kwamba wamekuwa maajenti waaminifu wa shetani. Wamekuwa waaminifu kwa shetani, na wamekuwa wanajitahidi kuwapeleka watawala wanaowatukuza kwa ibilisi.
 
Ulikuwa mwendo wa mapambio!
1645551285397.png

(Cartoonist: Marco Tibasima)
 
Hakuna binadamu asiyependa kutukuzwa awe mbunge au mchungaji,padre ,askofu ,mbunge,shehe nk au mtu wa kawaida ndio maana hata maaskofu husujudiwa watu wanapobusu Pete yake hupiga magoti kuibusu

Na hupenda kuitwa Baba Askofu,baba padre au Baba mchungaji wakati hawakuwazaa
MWANRI: Mungu amshukuru Rais Magufuli.....jamani kufuru ya karne.
 
Sikujua kumuita Rais mtukufu ilipitishwa na Bunge. Nimejifunza hulka hii ya ajabu tuliyonayo watanzania haikuanza juzi.
 
Hakuna binadamu asiyependa kutukuzwa awe mbunge au mchungaji,padre ,askofu ,mbunge,shehe nk au mtu wa kawaida ndio maana hata maaskofu husujudiwa watu wanapobusu Pete yake hupiga magoti kuibusu

Na hupenda kuitwa Baba Askofu,baba padre au Baba mchungaji wakati hawakuwazaa
Mtu yoyote anaweza kuitwa baba, je mtu yoyote anaweza kuitwa mheshimiwa? tumia akili kidogo
 
Back
Top Bottom