mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,763
- 35,201
Kumekua na ongezeko kubwa la wazazi kukupeleka watoto wadogo kuanzia chekechea. Kweli wazazi tumekua na majukumu mengi huku usaidizi katika malezi ukiwa changamoto kubwa sana.
Lakini kwa niliyoyaona na kuyasikia wazazi tujitafakari tena, watoto wengi wanaopelekwa bweni wanateseka mnoo. Wengine wanaishia kupata hadi ulemavu sababu ya kukosa malezi yanayoambatana na upendo toka kwa familia.
Matukio mengi yanayotokea kule yanaumiza ila kuna hili la mtoto ninayemjua kupelekwa bweni akiwa miaka3. Alipofika darasa la tano mtoto aligundulika kuwa na tatizo la kutoa haja kubwa bila kujijua. Kwanza kabisa tulijua mtoto keshaharibiwa, wazazi katika kuhangaika kumpeleka hospitali tofauti na kila wanasaikolojia na madaktari walivyokua wakimchunguza hawakuweza kupata ushahidi kwamba amewahi kufanyiwa kitendo chochote.
Baadae wakaambiwa wamepeleke muhimbili kwa matibabu zaidi na pale ndipo madaktari walipogundua kwamba mtoto katika umri wake mdogo alikua akiogopa kujisaidia either sababu ya kukaripiwa au kuona aibu kitu ambacho kilisababisha mfumo wa ufahamu ya utoaji haja kupoteza mawasliano na mtoto kupoteza uwezo wa kuhisi haja kabisa.
Kama sisi wazazi tunaona ni kazi kubwa sana kuwalea hawa malaika tuliowazaa kwa uchungu tunaonaje hili la kumpelekea matron mmoja watoto 10, 20, 30 na kuamini kwamba anawapa malezi bora kuliko sisi?
Watoto vinateseka jamani na kibaya kama mzazi unavyoamini kwamba shuleni ni bora kuliko nyumbani na matron na walimu ni bora kuliko wewe na mtoto anaamini hivyo, hadi uje ujue anachopitia mtoto anakua kashaumia sana