Kupekuliwa kwa askari polisi, punde waingiapo na kutoka mgodini

ntugwa12

Member
Aug 7, 2016
85
34
Habari wadau, hivi karibuni nimeshangazwa na utaratibu mpya wa kupekuliwa kwa askari wetu (polisi) mara tu wanapoingia kwenye maeneo ya mgodi fulani hapa Tanzania, sio wanaingia kwa minajili yao, lah hasha, wameombwa na kampuni hii ili kuimarisha ulinzi na usalama wa mwekezaji huu, hofu hivi sasa imetenda.

Je, raia anaruhusiwa kumpekuwa askari mwenye silaha ya moto?
Je, sheria inamtambuaje askari anapokuwa kwenye majukumu yake?

Naomba maelezo kwa wataalamu humu ndani!

Nawasilisha.
 
We unashangaa askari polisi kupekuliwa?, nasikia alivyokuja Obama tz,Afrika yote ilirambwa na mbwa.
 
Iko sawa kabisa. Hiyo sheria haibagui mtu. Halafu fahumu kuwa polisi siyo malaika au wana wafalme fulani.
 
Chakufanya mshauri kamanda weni, wakati maaskari mnatoka mgodi (underground) mmoja wenu ambaye hajazama awepo juu kwa ajili ya searching. Nadhani umenisoma, wakati wa kutoka mgodini askari polisi apekuliwe na askari polisi aliyepo kituoni, yule askari/ mlinzi wa kampuni awe observer tu. NB: nimekujibu kiutaratibu sijakujibu kisheria
 
Waambie mapoti wakaze, magonga yasiwa sababishe hadi kutokujua thamani yao, ................nguo na raia!!!!!!
 
Yaani sijaielewa hii, maana ya search ni kuchunguza . Sasa wao kwa wao wachunguzane patamu hapo Polisi atapachika bonge la jiwe kwenye chupi,fedha tamu
 
Askari ana madhaifu kama watu wengine na linapokuja suala la searching raia yoyote anayo haki ya kumkagua askari ili mradi asivunje sheria ndo maana hata ikitokea askari anataka kukukagua unayo haki ya kumkagua yeye kwanza ili asije akakuchomekea
Hivyo askari kukaguliwa mgodini si kosa maana wakati mwingine wamekuwa wakitumika katika vitendo vya udokozi
 
Umetoa elimu nzuri saana!Unapaswa pewa pongezi!!Hii ndio inatakiwa siku zote ndugu
 
Back
Top Bottom