Jamani, nimejaribu kufuata utaratibu wa kupata kibali cha ujenzi wa nyumba kutoka manispaa ya Kinondoni ila sasa ni mwaka mmoja tangu niombe ila ni usumbufu na rushwa imejaa mpaka sasa sijapata kibali.
Nikifuatilia mwanzoni walikuwa wanasema kikao bado hakijakaa kupitisha vibali na na nilipofuatilia toka mwezi wa tatu wakaniambia madiwani mpaka wakague kiwanja. Yaani sasa imekuwa ni usumbufu kila municipal engineer ananiambia atanisaidia na kuvuta hela akisema ni kwa ajili ya kuwalainisha mabosi lakini wapi mpaka leo naenda ila natoka patupu.
Nimafuatilia mainjinia wote wanataka rushwa na nimejaribu kumwona municipal director bila mafanikio.
Jamani naomba msaada wa mawazo ili nijue hatua za kuchukuwa.