Kupata vibali vya ujenzi manispaa ya Kinondoni ni rushwa tupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupata vibali vya ujenzi manispaa ya Kinondoni ni rushwa tupu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwanza, Sep 13, 2011.

1. m

mwanza JF-Expert Member

#1
Sep 13, 2011
Joined: May 7, 2009
Messages: 508
Likes Received: 176
Trophy Points: 60
jamani nimejaribu kufuata utaratibu wa kupata kibali cha ujenzi wa nyumba kutoka manispaa ya Kinondoni ila sasa ni mwaka mmoja tangu niombe ila ni usumbufu na rushwa imejaa mpaka sasa sijapata kibali.
Nikifuatilia mwanzoni walikuwa wanasema kikao bado hakijakaa kupitisha vibali na na nilipofuatilia toka mwezi wa tatu wakaniambia madiwani mpaka wakague kiwanja. Yaani sasa imekuwa ni usumbufu kila municipal engineer ananiambia atanisaidia na kuvuta hela akisema ni kwa ajili ya kuwalainisha mabosi lakini wapi mpaka leo naenda ila natoka patupu.
Nimafuatilia mainjinia wote wanataka rushwa na nimejaribu kumwona municipal director bila mafanikio.
Jamani naomba msaada wa mawazo ili nijue hatua za kuchukua

2. Chakaza

Chakaza JF-Expert Member

#2
Sep 13, 2011
Joined: Mar 10, 2007
Messages: 23,668
Likes Received: 21,901
Trophy Points: 280
Ujenzi holela ndani ya miji mingi ikiwema Mwanza na Arusha na kwingineko unatokana na ukiritimba na rushwa iliyokisiri katika Halmashauri za miji na majiji hapa nchini. Watanzania wa kawaida hawezi kupata pesa ya kujengea halafu ukaahirisha kumuidhinishia kujenga zaidi ya mwaka na bado akaendelea kuwa na hizo fedha zake hivyo apatapo usumbufu kama huo anaona heri ajijengee tuu liwalo na liwe huko mbeleni. Sasa inapofika suala la kubomolewa ndio ujue serikali inapochangia umasikini wa raia wake kwa kuruhusu watendaji watumie ofisi za umma kukwamisha mambo kwa manufaa binafsi.

3. zumbemkuu

zumbemkuu JF Bronze Member

#3
Sep 13, 2011
Joined: Sep 11, 2010
Messages: 9,004
Likes Received: 585
Trophy Points: 280
mkuu asaivi vikao vya kupitia michoro na kutoa vibali hufanyika mara 2 kwa mwz kwenye municipal zote za jiji la DSM, diwani hahusiki na kikao cha kupitisha kibali cha ujenzi coz hiyo inahusu zaidi watalaam, kama ofisa mipango miji, mhandisi na msanifu majengo, madiwani wao wanakaa vikao vya kuamua matumizi ya ardhi kama sikosei lakini sio kupitisha ramani, huo ni uhuni tu wanakufanyia.

4. M

Mbopo JF-Expert Member

#4
Sep 13, 2011
Joined: Jan 29, 2008
Messages: 2,532
Likes Received: 8
Trophy Points: 0
There is nothing political in this thread! Mods please do something about this misplacement.

5. zumbemkuu

zumbemkuu JF Bronze Member

#5
Sep 13, 2011
Joined: Sep 11, 2010
Messages: 9,004
Likes Received: 585
Trophy Points: 280
ili upate kibali cha ujenzi unapaswa kuwa na ramani ya jengo unalokusudia kujenga, pia ramani ya jengo lazima iendane na matumizi ya eneo husika. (residential, commercial residential...etc) sasa huo ukiritimba wa kusema madiwani pia wanatakiwa wawepo kwenye kikao cha kupata kibali ni uhuni tu huo.

6. kiroba

kiroba JF-Expert Member

#6
Sep 13, 2011
Joined: Sep 10, 2011
Messages: 324
Likes Received: 2
Trophy Points: 35
Ni kweli kabisa mkuu. Hili suala ni kwa manispaa zote tu, huwezi kupata kibali hata kama una documents zote zinazostahili. Utazungushwa hadi utaamua kukata tamaa. Pole sana mwananchi mwenzangu, lakini wana JF hili ni tatizo kubwa sana linalokabili taifa letu. Nawaomba wana JF kwa sauti ya pamoja tupaze ili tujaribu kuondoa suala kama hili katika manispaa zetu.

SALAMU KWA WAZIRI WA ARDHI (PROF ANNA TIBAIJUKA)
Hapa muheshimiwa una kazi kubwa sana, ila mimi binafsi nina imani sana na huyu mama. Ameonyesha uthubutu katika hili, tumpe muda na pia tumtie moyo huyu mama jasiri. Hapa muheshimiwa kwa kweli unatakiwa uwe na msimamo wa kweli vinginevyo utaadhirika katika hili.

7. m

mwanza JF-Expert Member

#7
Sep 14, 2011
Joined: May 7, 2009
Messages: 508
Likes Received: 176
Trophy Points: 60

Wataalamu akiwemo municipal engineer na municipal architect walishapitia michoro yangu na wakaniambia haina tatizo ila jambo lingine ni kuwa si jukumu la mwananchi wa kawaida kufuatilia ilitakiwa nikisha submit documents zangu wao wazipitishe kwa wahusika kwa muda unaotakiwa na either waniambie hiyo nyumba haifai kujengwa au wanipe kibali si kusubiri zaidi ya mwaka bila majibu

8. m

mwanza JF-Expert Member

#8
Sep 14, 2011
Joined: May 7, 2009
Messages: 508
Likes Received: 176
Trophy Points: 60

Labda ndugu yangu Mbopo haujaelewa pale municipal nimejaribu kuongea na baadhi ya wafanyakazi wanasema tatizo pale lipo kati ya technical staff na wanasiasa ndio maana madiwani ambao ni wana siasa wanaweza kumkataa mkurugenzi nahili la kutoa vibali nalo linawahusu madiwani kwa sababu wanashiriki kwenye vikao.
Tatizo lingine ni rushwa ambayo wenye nafasi kubwa ya kutusaidia sisi wananchi wa kawaida ni wanasiasa tuliowachagua likiwemo hili la kuwajulisha taabu tunayoipata kwenye vibali vya ujenzi

9. Bishanga

Bishanga JF-Expert Member

#9
Sep 14, 2011
Joined: Jun 29, 2008
Messages: 15,347
Likes Received: 47
Trophy Points: 0
Mkuu nakushauri umpigie simu meya wa manispaa Hon Mwenda,mpe malalamiko yako,namba yake ni 0754441335

10. Who Cares?

Who Cares? JF-Expert Member

#10
Sep 14, 2011
Joined: Jul 11, 2008
Messages: 3,465
Likes Received: 1,950
Trophy Points: 280
mkuu nakushauri anza ujenzi fastaaa...cha msingi uwe na risiti uliyotumia kulipia maombi ya kibali cha ujenzi.

kuna sheria inasema zikipita siku 90 toka ulipoomba kibali cha ujenzi na hujapewa sababu ya kutopewa kibali cha ujenzi unaweza kuanza ujenzi na lawama au matatizo yatayojitokeza yatabebwa na municipal husika
...ipo ngoja niingie library nikutafutie.

watanzania tujifunze kujua haki zetu ndogondogo za msingi kabsaaa...nawasilisha hoja

11. m

mwanza JF-Expert Member

#11
Sep 14, 2011
Joined: May 7, 2009
Messages: 508
Likes Received: 176
Trophy Points: 60

Nitashukuru sana ukinisaidia hicho kipengele cha sheria na mimi naanza fasta ujenzi

12. k

kakolo Senior Member

#12
Sep 14, 2011
Joined: Jul 7, 2011
Messages: 176
Likes Received: 31
Trophy Points: 45
Mimi niliweka file langu hapo swala likakaa muda mrefu wakati nafuatilia nikaambiwa mara afisa Mipango yupo ktk kikao mara
Nikaambiwa yuko Dodoma bungeni sasa hapo ndio niligombana nao hadi nikagundua lile file liko kwa masecretary na ndio waliokwamisha mizunguko yote. Niligombana nao sana baada ya mwezi nikapata kibali. Hiyo ni golofa kama ni nyumba ya chini
Anza kujenga tu.
Nilichachamaa shida hakuna pa kushitaki masekretary vigeuvigeu na mayor haonekani vikao daily. Nikagundua pia vikao ndio
Vinawapatia posho siyo kuwa hapo ofisini.
Nashukuru kwa hiyo namba ila sijui kama atapokea yy au secretary.

Loading...