Kupata utajiri siyo suala la bahati, ni sayansi kama zilivyo sayansi nyingine

Kupata utajiri siyo swala la bahati au ujanja ujanja, bali ni sayansi, kama zilivyo sayansi nyingine. Ili moto uwake unahitaji kupata hewa ya oksijeni, hiyo ni sayansi, kadhalika kuna vitu vinahitajika ili mtu uweze kupata utajiri, hiyo pia ni sayansi.Sayansi ina sheria na kanuni zake, ambazo zikifuatwa basi matokeo yanakuja sawa wakati wote.

Hivyo utajiri pia una sheria na kanuni zake, ambazo mtu akizifuata ataweza kupata utajiri bila ya kushindwa. Uzuri wa sayansi ni kwamba hakuna kubahatisha, ukiweka kitu sahihi na utapata matokeo sahihi, ukiweka kitu ambacho siyo sahihi na matokeo yatakuja ambayo siyo sahihi, Kwa wale mliosoma masomo ya sayansi natumai mnanielewa vizuri.

Watu wengi wamekuwa wakifikiri kupata utajiri ni bahati, na hivyo kushiriki michezo ya kubahatisha na kamari wakiamini ipo siku yao. Rafiki, huwezi kupata utajiri wa uhakika na wa kudumu kupitia michezo ya kubahatisha, usijaribu kufanya hivyo na kama umewahi kufanya basi acha mara moja. Michezo ya kubahatisha siyo kanuni sahihi ya utajiri. Imeandikiwa Utajiri unatengenezwa na vitu viwili vikubwa;

NAMNA YA KUFIKIRI

Kuna namna ya kufikiri ambayo matajiri wanaitumia. Matajiri wana fikra chanya kuhusu fedha na utajiri, hufikiri kuhusu uwezekano na wanajua kuna utele wa chochote wanachokitaka kwenye dunia hii .Matajiri Wanajua dunia ina rasilimali za kutosha na haziwezi kuisha kamwe.

Kwa upande wa pili, masikini wana namna ya kufikiri ambayo inawaweka kwenye umasikini maisha yao yote. Kwanza wanaamini utajiri siyo kitu kizuri, wanajiambia umasikini ndiyo bora.

Pia wanaamini kwenye uhaba,kwamba dunia ina uchache na wachache pekee ndiyo wanaoweza kunufaika na rasilimali chache zilizopo. Kwa kuwa na mtazamo huu, masikini hufikiri ili wao wapate lazima wengine wakose, masikini wengi wao tena ni watu wenye nguvu wasiokuwa na ulemavu wowote ule hutumia andiko hili Kama silaha yao ya kujilinda.

NAMNA YA KUTENDA

Kiungo cha pili cha sayansi ya utajiri ni namna ya kutenda. Wale wanaotajirika wana namna ya kufanya mambo yao ambayo yanawaletea matokeo makubwa na mazuri sana. Wakishapanga kitu cha kufanya, wanachukua hatua mara moja, hawaahirishi kitu na hawaruhusu usumbufu wowote ujitokeze na uwatoe kwenye kile wanachofanya. Watu hawa wana vipaumbele ambavyo wanavisimamia na kufanyia kazi. Na chochote wanachofanya, wanakifanya kwa ubora wa hali ya juu sana. Kwa maana Imeandikiwa

Kwa upande wa pili, masikini wana namna yao ya kutenda mambo ambayo inawafanya waendelee kuwa masikini kwa maisha yao yote. Kwanza kabisa hawajui wanataka nini, hivyo muda wote wako ‘bize’ harakati zao hazina tofauti sana na harakati za Inzi lakini hakuna matokeo makubwa wanayopata kutokana na ubize wao.

Pili Masikini ni wazuri sana kwenye kuahirisha mambo, wanapanga wenyewe vitu vya kufanya lakini unapofika wakati
wa kufanya utasikia wanajiambia Nitafanya kesho. Imeandikiwa masikini wamezungukwa na kila aina ya usumbufu na hawataki kupitwa na jambo lolote katika maisha yao, hali hii inawachosha hata kabla hawajafanya kazi. Na hata pale wanapofanya kazi, wanaifanya kwa ukawaida sana, kama vile hawataki. Kwa tabia hii utajiri kwao wataendelea kuusoma kwenye magazeti na kuuona kwenye TV.

Nakubaliana naww kwene utajiri ni sayansi!!!…
mfano tu nchi tajiri n ulaya!! … wao wanaamini sayansi tu
huku tunakoamini ndumba na ushirikina bado ni fukara
 
Hii yaweza kuwa kubwa sana kwa wengi hapa na ukiwaambia hii ni sayansi wanachanganyikiwa.

Labda tuseme ni hesabu, mfano ukifanya 1+1=2. Hii ni kanuni na ndivyo ilivyo katika uhalisia wa kusaka utajiri ni lazima uzijue kanuni kama vile kijiti kimoja kikiwekwa pamoja na kijiti kingine lazima upate vijiti viwili.

Shida inakuja katika kuzijua hizo sheria au kanuni na namna ya kuzitumia.

Ninchoweza kuwaambia hiyo elimu inayofundishwa mashuleni hadi vyuo vyenu vikuu hakuna kanuni za utajiri zinafundishwa.

Ndiposa wengi wanaoingia mtaani kujifunza kwa waliofanikiwa hufanikiwa na pengine wengine hurithishwa kanuni hizo toka wazazi kama Wahindi au familia za matajiri. Kuna wengine huamua kujifunza kama akina Ben Zen Tarot
 
Huwa mnaelewa sayansi ni nini kweli??
Kila kitu sasa hivi mnaita ni sayansi!
Dr. Mihogo alisema siasa ni sayansi
Wengine nimewasikia wakisema mpira nao ni sayansi
 
Kwani sayansi ni nini ndugu...

Nijuavyo mimi Sayansi ni pale unapotumia au kufuatilia jambo kwa kuzingatia au kuegemea mbinu, kanuni au ushahidi thabiti wa jambo hilo lilivyofanyika au linavyofanyika na kukupatia matokeo sahihi bila chenga kama ulivyokusudia.

Ndio maana 1+1=2. Na kama mtu akikupatia kanuni au mbinu thabiti aliyoijaribu mara nyingi na anafikia malengo sio kwa kubahatisha. Basi hiyo ni Sayansi,

Labda sijui wewe unaifikiriaje sayansi ndugu tuzidi kueleweshana.
 
Vipi wale waliopata utajiri kwa urithi,au
Kwenye madini hawa walitumia sayansi gani
4. kuna watu wana bahati au nuksi. maana yangu ni kwamba kuna watu ambao kila wanachogusa katika biashara au ajira fulan wanafanikiwa. kinyume chake ni sawa, kuna watu wana nuksi. anafuata kanuni zote na sayansi za mtoa mada lakini hakuna kitu anafanikisha.
 
kwa hio una maanisha maskini wote hawafuti hizo njia hapo au. Vivyo hivyo matajiri hufuata njia hizo hapo?
 
Kupata utajiri siyo swala la bahati au ujanja ujanja, bali ni sayansi, kama zilivyo sayansi nyingine. Ili moto uwake unahitaji kupata hewa ya oksijeni, hiyo ni sayansi, kadhalika kuna vitu vinahitajika ili mtu uweze kupata utajiri, hiyo pia ni sayansi. Sayansi ina sheria na kanuni zake, ambazo zikifuatwa basi matokeo yanakuja sawa wakati wote.

Hivyo utajiri pia una sheria na kanuni zake, ambazo mtu akizifuata ataweza kupata utajiri bila ya kushindwa. Uzuri wa sayansi ni kwamba hakuna kubahatisha, ukiweka kitu sahihi na utapata matokeo sahihi, ukiweka kitu ambacho siyo sahihi na matokeo yatakuja ambayo siyo sahihi, Kwa wale mliosoma masomo ya sayansi natumai mnanielewa vizuri.

Watu wengi wamekuwa wakifikiri kupata utajiri ni bahati, na hivyo kushiriki michezo ya kubahatisha na kamari wakiamini ipo siku yao. Rafiki, huwezi kupata utajiri wa uhakika na wa kudumu kupitia michezo ya kubahatisha, usijaribu kufanya hivyo na kama umewahi kufanya basi acha mara moja. Michezo ya kubahatisha siyo kanuni sahihi ya utajiri. Imeandikiwa Utajiri unatengenezwa na vitu viwili vikubwa;

NAMNA YA KUFIKIRI

Kuna namna ya kufikiri ambayo matajiri wanaitumia. Matajiri wana fikra chanya kuhusu fedha na utajiri, hufikiri kuhusu uwezekano na wanajua kuna utele wa chochote wanachokitaka kwenye dunia hii. Matajiri Wanajua dunia ina rasilimali za kutosha na haziwezi kuisha kamwe.

Kwa upande wa pili, masikini wana namna ya kufikiri ambayo inawaweka kwenye umasikini maisha yao yote. Kwanza wanaamini utajiri siyo kitu kizuri, wanajiambia umasikini ndiyo bora.

Pia wanaamini kwenye uhaba,kwamba dunia ina uchache na wachache pekee ndiyo wanaoweza kunufaika na rasilimali chache zilizopo. Kwa kuwa na mtazamo huu, masikini hufikiri ili wao wapate lazima wengine wakose, masikini wengi wao tena ni watu wenye nguvu wasiokuwa na ulemavu wowote ule hutumia andiko hili Kama silaha yao ya kujilinda.

NAMNA YA KUTENDA

Kiungo cha pili cha sayansi ya utajiri ni namna ya kutenda. Wale wanaotajirika wana namna ya kufanya mambo yao ambayo yanawaletea matokeo makubwa na mazuri sana. Wakishapanga kitu cha kufanya, wanachukua hatua mara moja, hawaahirishi kitu na hawaruhusu usumbufu wowote ujitokeze na uwatoe kwenye kile wanachofanya. Watu hawa wana vipaumbele ambavyo wanavisimamia na kufanyia kazi. Na chochote wanachofanya, wanakifanya kwa ubora wa hali ya juu sana. Kwa maana Imeandikiwa

Kwa upande wa pili, masikini wana namna yao ya kutenda mambo ambayo inawafanya waendelee kuwa masikini kwa maisha yao yote. Kwanza kabisa hawajui wanataka nini, hivyo muda wote wako ‘bize’ harakati zao hazina tofauti sana na harakati za Inzi lakini hakuna matokeo makubwa wanayopata kutokana na ubize wao.

Pili Masikini ni wazuri sana kwenye kuahirisha mambo, wanapanga wenyewe vitu vya kufanya lakini unapofika wakati wa kufanya utasikia wanajiambia Nitafanya kesho.

Imeandikiwa masikini wamezungukwa na kila aina ya usumbufu na hawataki kupitwa na jambo lolote katika maisha yao, hali hii inawachosha hata kabla hawajafanya kazi. Na hata pale wanapofanya kazi, wanaifanya kwa ukawaida sana, kama vile hawataki.

Kwa tabia hii utajiri kwao wataendelea kuusoma kwenye magazeti na kuuona kwenye TV.

Uko sahihi kabisa
 
Tajiri kuingia mbinguni ni nafuu ya ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.

Imeandikwa.
unajua kuwa matajiri ndio wanaoendesha ulimwengu na kuwalipa mishahara maskini.

Hebu fikiria dunia hii bila matajiri, tungemwabudu Mungu kwa vibanda vya nyasi😂

Yaani mfalme Suleiman alieandika kitabu cha Zabur, mithali, na vingine, mwenye hekima na tajiri mkubwa enz hizo ashindwe kutinga mbinguni. Acha hizo bhana.

Achana na fikra nzito, umaskini unaosemwa hapo ni akili. Unaweza ukawa tajiri wa fikra potofu na ovu.

Niishie hapo, kwani hata nikiandika maandishi kujaa JF zote hutokaa uelewe. Chagua umaskini, mimi nachagua utajiri man na mbinguni utanikuta kwani nina uhakika. Ninagonga maisha hapa na mbinguni pia kisha narud hapa kiendeleza maisha. Raha ilioje
 
How comes unahubiri kwa Mungu kila jambo linawezekana halafu unakuja kwangu kupiga mzinga
 
Hii sayansi ni muda muafaka sasa ikaingizwa kwenye mitaala yetu mashuleni, maana hali zetu ni tete.
Sahau, hilo halitakaa litokee milele. Labda uingize mwenyewe mitaala ya nyumbani kwako. Shulen ni rahisi kuingiza mitaala ya ushoga kuliko hilo na misaada ya vitabu na vyoo na mabafu shuleni mkapewa. KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI🤣
 
Back
Top Bottom