Kupata mtoto kabla ya ndoa sio mwisho wa maisha

Status
Not open for further replies.

Peter Stephano 809

Senior Member
Feb 29, 2020
120
162
Enzi za mababu na mabibi zetu ilikua ni lazima mwanamke apate mchumba aolewe kisha azae watoto na ajenge familia akiwa nyumbani kwa mume wake.

Kwa jamii ya leo si jambo geni kusikia mwanamke amepata ujauzito kabla ya ndoa akiwa shuleni au nyumbani kwao.

Hii ni kutokana na mabadiliko ya kisayansi, utandawazi na mambo mengine ya maadili katika maisha.

Dhana ya mwanamke kupata mtoto kabla ya ndoa ni miongoni mwa ajenda inayo itofautisha jamii kimtazamo kwa Sasa.

Kumekuwa na mawazo mseto juu ya uhalali wa tabia ya mwanamke anaepata mtoto kabla ya ndoa.

Mpaka kupelekea baadhi ya watu kuona mwanamke aliyepata mtoto kabla ya ndoa hafai kuoelewa na mwanaume mwingine iwapo hatopata bahati ya kuolewa na yule aliyezaa nae.

Aidha wanao amini kwenye msingi huu hutetea hoja yao kuwa mwanamke aliyepata mtoto kabla ya ndoa si mwanamke wa kuoa kwani anaweza kuwa na changamoto nyingi kisa ambacho kinapelekea ashindwe kuolewa na mwanaume aliyezaa nae huyo mtoto au watoto.

Wengine huenda mbali zaidi kwa kumchukulia mwanamke aliyepata mtoto kabla ya ndoa kuwa malaya asie na Subira na mwenye kutofuata maadili ya dini, mila na tamaduni za kijamii.

Kwa upande wa kundi lingine la kijamii huchukulia hali hii Kama changamoto ya kijamii kwa kueleza kuwa kitendo cha mwanamke kupata ujauzito kabla ya ndoa si cha kujitakia wala kuendekeza bali hutokana na sababu mbalimbali.

Uhaba wa Elimu ya uzazi miongoni mwa wasichana wadogo, mabadiliko ya kimwili na kulubuniwa ni miongoni mwa sababu zinazotajwa.

Kadharika tabia ya Wanaume wakubwa kwa wadogo kuwarubuni wanawake kuwa baada ya kuzaa nao watawaoa kisha kuwatelekeza.

Watetezi wa dhana hii wanasema kuwa wanawake wengi wanaweza kuwa wamelelewa kwenye Maadili mema ila huingia kwenye Uhusiano na Wanaume wasio na malengo nao kimaisha jambo ambalo hupelekea mimba kabla ya ndoa.

Na inaelezwa kuwa wanawake wengi baada ya kuzalishwa watoto pasipo matakwa yao hujiona walio chafuliwa hivyo kuwachukia Wanaume wao na kutotaka kabisa mahusiano baada ya kupata mtoto Jambo ambalo hukatisha mipango ya kufunga ndoa.

Pia dhana ya hii ya utetezi inabainisha kuwa Wanaume ndio chanzo kikubwa cha tatizo kwa kuendekeza tamaa pasipo kuwa na malengo wala mipango ya ndoa baada ya kupata mtoto.

Kitendo hiki hukatisha tamaa wanawake walio zàa nao na kujikuta wanatengana kabisa kila mtu kuanza Maisha yake ya tofauti.

Lakini je ukweli ni upi juu ya mawazo haya mseto ya jamii kuhusu mwanamke aliyepata mtoto kabla ya ndoa.

Jambo la kwanza ni kutambua kuwa kupata mtoto ni majaliwa ya mwenyezi mungu Kama ilivyo elezwa kwenye vitabu vya dini.

Kadharika mwanamke au mwanaume aliyepata mtoto kabla ya ndoa hapaswi kujiona mwenye uovu mkubwa kupita uovu wote duniani bali anapaswa kutimiza wajibu na matakwa ya kimaadili kwa kumuoa au kuolewa na yule aliyezaa nae.

Mwanamke aliyepata mtoto kabla ya ndoa iwe kwa bahati mbaya ama kwa maksudi anapaswa kutambua mtoto ni baraka na si haramu mbele ya Mungu.

Wanawake wengi huvunjika moyo na kukata tamaa juu ya maisha na kujiona hawana thamani yoyote kwenye jamii jambo ambalo sio kweli na hudumaza ustawi na utu wao kwenye jamii.

Mwanamke aliyepata mtoto kabla ya ndoa anapaswa kusimama imara kwa kutimiza wajibu wake kwa mtoto, kuendelea Kufuata mila na tamaduni za jamii pamoja na kujali maisha yake ili mambo mengine yaendelee.

Jamii pia inapaswa kubadilika kwa kutokuwa na mawazo hasi juu ya mwanamke anaepata mtoto kabla ya ndoa kwani kuna mambo mengi humkumba mwanamke katika maisha Kama ilivyoelezwa hapo mwanzo.

Wanaume wanapaswa kubadilika kuachana na tabia ya kuwarubuni wanawake kisha kuwatelekeza pia wanapaswa kuachana na Imani potofu juu ya mwanamke anaepata mtoto kabla ya ndoa.

(Picha kwa Msaada wa Internet Mnmtanzania.com)

Peter Mwaihola kitaaluma Ni Mwandishi wa habari na mchambuzi wa masuala ya siasa na jamii.
 
Mada nzuri, ila changamoto ni kwamba umebase kwenye upande mmoja kuonesha kuwa wanaume pekee ndo tunafanya makosa kwa wanawake zetu, ila ukiangalia pia upande wa pili hata wao wanatukosea na mifano ipo mingi tu, ila kwetu sisi baadhi ya wanaume tunakubaliana na hali.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom