kupata mimba

millionroses

Member
Nov 12, 2012
19
2
habari jf doctor...nilianza kubleed tarehe 24/11/2012 na nikamaliza tarehe 28/11/2012...je ni siku gani ambayo ningeweza kupata mimba..msaada
 
habari jf doctor...nilianza kubleed tarehe 24/11/2012 na nikamaliza tarehe 28/11/2012...je ni siku gani ambayo ningeweza kupata mimba..msaada
ni rahisu ndugu yangu ongeza siku 14 tangu umeanza siku zako kwa mtoto wa kiume, na siku 15 kwa mtoto wa kike. kwa maelezo yako ya mwezi huu tegemea kupata siku ya tarehe 7- 9/12/2012
 
ni rahisu ndugu yangu ongeza siku 14 tangu umeanza siku zako kwa mtoto wa kiume, na siku 15 kwa mtoto wa kike. kwa maelezo yako ya mwezi huu tegemea kupata siku ya tarehe 7- 9/12/2012
Si sahihi kuhusu tarehe za mtoto wa kike na kiume. Kumbuke mbegu ya mtoto wa kiume (y) ina speed kubwa kuingia ukeni lakini inakufa mapema, lakini ya mtoto wa kike (x) ina mwendo mdogo lakini inaishi muda mrefu. Kwa hiyo kama yai litatoka siku ya 14, na akakutana na mwanaume siku hiyohiyo, uwezekano mkubwa ni kupata mtoto wa kiume. Lakini kama atakutana na mwanaume siku moja kabla, uwezekano ni mkubwa wa kupata mtoto wa kike.
Lakini hii mara nyingi ni bahati nasibu tu. Kwa kuwa hakuna fixed day ya yai kutoka. Unaweza kuwa na mzunguko wa siku 28, yet yai likachelewa au kuwahi zaidi. Kwahiyo mpango wa mtoto wa kiume au wa kike huwa si perfect siku zote.
 
nashukuru kwa ushauri kidogo napata faraja maana hizo siku niliwajibika ipasavyo.....
Tafuta kifaa kinaitwa ovulation predictor kit kitakusaidia katika kujua siku nzuri za kupata mimba vifaa hivi kwa sasa vinapatikana kwenye Pharmacy nyingi za hapa mjini.Kifaa hiki ni mkombozi kwa akinadada ambao wanahitaji kupata mimba na hawajui utaratibu wa siku zao au siku zao huwa zinabadilika mara kwa mara.
 
hata kama ulijitahidi ipasavyo ww, je huyo mwanaume alikuwa anaproduce matured sperms, kama alikuwa anafanya kila cku sperms znakomaa muda gan? mimba inatungwa kwa condition flan kutoka kwa mwaume na mwanamke pia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom