Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!

Wanasema baba ndio kichwa cha familia, familia isiyokuwa na uwelekeo wakimaendeleo baba ndio tatizo.

Pascal Mayalla wana ccm nyie ndio baba wa taifa hili nini shida kwenye hili la kilimo
Msema kweli ni Mpenzi wa Mungu, ni kweli pale mwanzo Baba alikuwa tatizo, na baadhi ya akina sisi watoto, hilo tuliliona, hatuku kaa kimya kwa kunyamaza, tulipaaza sauti zetu kulisema

Huyu Baba wa sasa aliyepo, (japo kijinsia ni mwanamke), ili asifanye makosa kama ya Baba aliyemtangulia anahitaji kusaidiwa kuonyeshwa tatizo ni sisi Watanzania wenyewe kwenye Upangaji wa Vipaumbele Vyetu, baadhi ya sisi Watanzania wazalendo tumeisha libaini hili na tumejitolea kujitokeza kumsaidia kupitia sauti zetu (TV Program ya "Kwa Maslahi ya Taifa" ), au kupitia makala za magazetini "Kwa Maslahi ya Taifa" na huku kwenye mitandao ya Jamii ikiwemo JF, na mfano mzuri ni Makala yangu hii

Tanzania bado tuna tatizo la upangaji vipaumbele vyetu, baada ya Elimu, Afya na kilimo, ilipaswa ije nishati!. Ni aibu na hatari kupikia kuni na mkaa!

Makala hiyo iliandamana na kipindi cha TV kwenye ITV na TBC. Sasa kama Mzee Baba (Mama Babaa) na lile jicho lake (japo limeregea lakini linaona sana), litakuwa limeona, hata kama sio yeye mwenyewe in person, lakini lile jicho lake jingine by proxy linaloona kila mahali , kila kona hadi uvunguni, litakuwa limeona, hivyo Mimi kama raia mwema wa taifa langu, nitakuwa nimetimiza wajibu wangu kwa nchi yangu.

P.
 
What are Priorities Zetu, Tanzania?. Nini ni Vipaumbele Vyetu? .
Taifa linakabiliwa la viongozi wasio na vision hivyo kukosa mission to accomplish, we seriously lack visionary leaders ndio maana karibu kila kitu ni mpaka rais aje!. Je nini vipaumbele vyetu?, Tanzania kama nchi inayotaka maenddeleo ya kweli, tunatakiwa tujue ni nini tunataka na tutapataje. Kama hujui unachotaka, huwezi kutafuta maana hujui utafute nini!. Ukiishajua unataka nini, ndipo unajipanga utapataje hicho unachokitaka na njia za kukitafutia ili ukipate!. Ukiisha kosa vision, huwezi kuwa na mission to accomplish ya unatekeleza nini, hivyo tumekuwa ni nchi ya kuendeshwa na matukio.

Ushauri wa A Way Forward and What to do.
Serikali yetu, kila wizara, kila idara na kila wakala, lazima ziwe na mission na vision statements, accompanied by a list ya Strategic Objectives ambazo ziko SMART (Specific, Measurable, Attainable, Realistic, Timely). Pia ziwepo timeline strategy ya utekelezaji hizo smart objectives, hivyo viongozi wajitokeze kutueleza na kutuonyesha achievements ya utekelezaji malengo kusudiwa na sio kutufanyia dramas na maonesho ya kuita media na kutoa maagizo na maelekezo kwa kusema tutafanya hiki au kile, lakini hatuoni, utekelezaji.

Tuanze ku demand kuonyeshwa results oriented events nini kilichofanyika na sio kututengenezea maigizo ya matukio. Kila siku tunaonyeshwa jinsi viongozi wetu wakizindua miradi, Viwanda, etc, lakini hatupewi mrejesho wowote hiyo miradi imeleta faida gani kwa wananchi na maendeleo ya taifa. Badala ya kuonyeshea viongozi wanasema nini na wanafanya nini, tuonyeshwe matokeo, results oriented actions.

Nakamilisha taratibu za kurusha Vipindi Maalum vya TV vitakavyoitwa "Kwa Maslahi ya Taifa" ambavyo vitaangazia nini kimefanyika, nini kifanyike kuitoa Tanzania hapa ilipo kwenda kwenye Tanzania tunayoitaka.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Hiki nilichozungumza hapa, ndicho kitu Gwajima alichokisema leo Bungeni. Visionary leadership, viongozi wenye maono.

P.
 
Wanabodi,
Sisi Wana mitandao tumeshauriwa kuitumia mitandao kulisaidia taifa letu kuendelea, hivyo huu ni ushauri wangu.

Ili Tanzania tuendelee kwa kupata maendeleo ya kweli, na sio maendeleo kiini macho, tunahitaji kujenga taasisi Imara ( strong institutions), zenye mifumo imara, ( an effective systems) ambayo inakuwa automated, ikitokea kuna jambo lolote haliko sawa, the system itself, will detect na hapo hapo kuwa ejected out of system, straight away, hakutakuwa na haja ya tumbua tumbua, mtu akienda kinyume cha mfumo, ni mfumo ndio utamuondoa, na sio kumsubiria rais kumtumbua!. Rais anapofanya ziara mbalimbali, kusema ukweli kuna vitu vinaibuka ambayo ni vya kawaida sana, sio mpaka rais aje ndio viwe detected. Sio kila kitu ni mpaka rais!.

Tanzania hatuhitaji sanaa za maonyesho ya drama na ze comedy za one man shows kuonyeshea maigizo ya uchapa kazi na utawala bora kwa maonyesho na ziara za kushtukiza, ili baadae kurushiwa matukio kwenye mitandao ya Jamii, jioni kutokelezea kwenye TV na runinga zetu, na kesho yake kutokea kwenye magazeti ili tuu kuwaonyeshea watu, Watanzania waone jinsi viongozi wetu, wanavyochapa kazi kwa bidii kuleta maendeleo by, just to make believe something is being done na rais wetu!, tena siku hizi karibu kila anachofanya rais, kinarushwa live na TV zile zile ambazo hazina fedha za kurusha live Bunge la wananchi, lakini live za rais, wanaweza!.

Ziara za Kushtukiza Vs Maigizo ya Ziara za Kushtukiza.
Kuna ziara za kweli za kushtukiza na kuna maigizo ya ziara za kushtukiza. Ziara za kweli za kushtukiza hufanyika kwa kushutikiza kiukweli kweli, no one knows, except the inner circle, hata media ni ile tuu ya rais, lakini maigizo za ziara za kustukiza ni pale wahusika wote wakuu wanaarifiwa ikiwemo media inaambiwa na kualikwa ili iwepo mahali husika patakaposhtukizwa ili warekodi tukio hilo la kustukiza, turushiwe kwenye breaking News za mitandao ya kijamii na jioni watu waje waone kwenye TV na kesho yake kwenye magazeti !.

Mfano mzuri ni kontena zimekamatwa siku nyingi nyuma, scanner zimeonyesha kilichomo ndani containers hizo, mhusika mwenye kontena ametafutwa, amepatikana na amekamatwa yuko kwenye selo ya polisi, containers zimefunguliwa mbele yake kujiridhisha na contents za kilichomo, kisha mhusika anasweka selo, conteiners hizo zinafungwa na zinawekwa seals mpya as if hazijafunguliwa, kisha rais anaarifiwa atafute muda aje kufanya ziara ya kushtukiza, muda ukipatikana, media zinaarifiwa, kuwa rais atafanya ziara ya kushutukiza bandarini, hadi muda wa ziara hiyo, kisha rais anafanya ziara, anapelekwa straight eneo zilipo conteiners hizo, likiwepo kundi kubwa la media iko standby kusubiria ziara ya kushukiza, rais anaonyeshwa conteiners hizo zikiwa zimefungwa na seal as if hazijawahi kufunguliwa!, kisha conteiners hizo zinafunguliwa mbele ya rais huku media ikilirekodi tukio zima, na baada ya kufunguliwa ndipo watu kujifanya kushangaa kilichomo na media kutengeneza a big story ya " Rais Magufuli Afanya Ziara ya Kushukiza Bandarini, Abaini...

Igizo la Ziara ya Kushtukiza Jana Pale Bandarini.
Ni wajinga tuu na wale wasiofahamu process za usafirishaji makontena bandarini ndio wataamini kuwa jana rais Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza Bandarini Dar, na katika ziara hivyo amebaini contena 26 za mchanga wa dhahabu na contena 2 zilizoficha magari ya kifahari ili tuu kuonyesha rais wetu ni mchapa kazi, ameokoa tusiibiwe kwa ziara ya kushukiza Bandarini, and he is doing something!.

Kilichotokea.
Kusafirisha containers is a process, by the time rais anapiga marufuku kusafirishwa mchanga wa dhahabu, tayari consignment ya huo mchanga unaodaiwa kukamatwa, tayari iliishakuwa processed on transit na kuna sehemu ya mizigo iliishafika bandarini siku nyingi kabla ya marufuku ya rais, na kwenye ICDs, hapo bandarini, hivyo kupitia tangazo la marufuku ya rais, likapelekea hizo consignment zote zisimamishwe na kuzuiliwa bandarini. Sasa kuita media na kumuita rais kujidai kukamata kitu kilichohifadhiwa na kuzuiliwa kihalali kabisa hapo Bandarini kwa kujifanya kumebainishwa na ziara ya kushutukiza ya rais, ni usanii wa sanaa za maigizo!.

Containers za Mitumba Kumbe Magari!.
Zile contena za magari zilizoandikwa mitumba, zote ziliwasili nchini toka mwezi November mwaka jana, na zilipitishwa kwenye scanners na kuona kilichomo ndani ni tofauti na kilicho kuwa declared kwenye the bills of landing. Mmiliki wa mzigo huo ni Ramadhani Mussa Hamisi Ukwaju ambaye, masikini wa watu ni clearing agent tuu, by chance mimi namfahamu mtu mwenye mzigo huo, hivyo clearing agent huyo ameisha kamatwa siku nyingi, tangu Mwezi February, containers zikafunguliwa mbele yake, na yuko kwenye mahabusu ya Polisi Bandari tangu tarehe 4 ya mwezi huo wa February kwa kosa la kuhusika na mzigo wa magari ya kifahari yaliyoingizwa nchini kinyemela kama nguo za mtumba, na toka alipokamatwa hiyo tarehe 4 mpaka leo, bado hajafikishwa mahakani ili tuu kusubiria mpaka rais apate nafasi ya kuja kufanya ziara ya kushtukiza bandarini, huku mhusika akiozoea selo!. Standard time ya mtu kukaa mahabusu bila kufikishwa mahakamani ni 24 hrs! . Mtu kukamatwa tangu tarehe 4 February hadi leo bila kufikishwa mahakamani ili kutengeneza igizo la kukamatwa hizo containers!. Kisha rais anakuja, wanaweka seal nyingine na kufungua upya ili tuu kuwaonyeshea Watanzania jinsi rais wetu alivyo mchapa kazi.

Ni Mchanga Au Makinikia?
Scanners zimeishaonyesha contents ya mchanga kwenye conteiners za Acacia, ambao jina lake halisi ni makinikia, containers hizo zilipokelewa bandarini siku nyingi nyuma kabla ya marufuku ya rais kusafirisha mchanga nje ya nchi, na process iliisha anza kabla ya katazo la rais, hivyo rais kuelezwa ni mzigo mpya, ni kumdanganya!. Yaani kila kitu kinajulikana kabla, kisha rais wetu anaitwa kuja kushtukiza akiandamana na media, ili kesho yake ndio iwe headlines, hili ni igizo la ziara ya kushtukiza!, but very unfortunately kwa this time around, igizo la jana limebuma ku attract the intended much needed attention ya front page kuonyeshea uchapakazi wa rais wetu, kwa sababu kulitokea tukio kubwa zaidi kihabari, that was more news worth kuliko igizo hili!.

Drama na Igizo za Ziara ya Kushtukiza.
Baada ya hayo kubainika, daily report ilionyesha lakini ikaamuliwa kusichukuliwe hatua zozote bali mkuu wa nchi aarifiwe kwanza, kisha ipangwe ziara ya kushtukiza halafu ndipo hayo yaonekane yamebainishwa na ziara hiyo ya kushtukiza ili ionekana kama ni ziara ya kushukiza ya rais ndio imebaini hayo!. Everything was a premeditated moves, although it was well staged kuonekana ni issue kubwa, lakini ndio hivyo tena, sometimes hata sterling kwenye movie huwa ana bugi step na hulazimika kufanya take two or take three!. Jana kwenye media Nape ndio alikuwa sterling!.

Shows za Ze Comedy.
Kumuita Mkuu wa nchi kufanya ziara za kushtukiza katika tukio lililopangwa na kisha kufungua zile seals za yale makontena mbele ya rais huku akishuhudia na ku act kushangaa, kuwa ndio wamebaini hayo magari ya kifahari, ili tuu kuuaminisha umma kuwa ni ziara hiyo ndio imeibua hayo, ni kupoteza muda wa thamani wa rais wetu. Hivi sio vitu vya kulisaidia taifa letu. Tusifanye vitu tuu ili watu waone!. Viongozi wetu wasitumie media kufanyia maonyesho ya maigizo ya utendaji kazi, au utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku!.

What are Priorities Zetu, Tanzania?. Nini ni Vipaumbele Vyetu? .
Taifa linakabiliwa la viongozi wasio na vision hivyo kukosa mission to accomplish, we seriously lack visionary leaders ndio maana karibu kila kitu ni mpaka rais aje!. Je nini vipaumbele vyetu?, Tanzania kama nchi inayotaka maenddeleo ya kweli, tunatakiwa tujue ni nini tunataka na tutapataje. Kama hujui unachotaka, huwezi kutafuta maana hujui utafute nini!. Ukiishajua unataka nini, ndipo unajipanga utapataje hicho unachokitaka na njia za kukitafutia ili ukipate!. Ukiisha kosa vision, huwezi kuwa na mission to accomplish ya unatekeleza nini, hivyo tumekuwa ni nchi ya kuendeshwa na matukio.

Nchi inakabiliwa na sitofahamu nyingi, kuna kiongozi amefoji vyeti, kuna kiongozi amefanya tukio la uhalifu wa uvamizi wa media, kuna waziri muadilifu anatimiza wajibu wake kikamilifu tena kwa waledi wa hali ya juu, badala ya mhalifu kutumbuliwa, anatumbuliwa Waziri muadilifu na kama haitoshi, mjinga fulani anamtolea na kumtishia bastola, mbele ya media live, halafu Mkuu wetu wa nchi anakwenda kufanya igizo ziara ya kushtukiza bandarini!.

Ushauri wa A Way Forward and What to do.
Serikali yetu, kila wizara, kila idara na kila wakala, lazima ziwe na mission na vision statements, accompanied by a list ya Strategic Objectives ambazo ziko SMART (Specific, Measurable, Attainable, Realistic, Timely). Pia ziwepo timeline strategy ya utekelezaji hizo smart objectives, hivyo viongozi wajitokeze kutueleza na kutuonyesha achievements ya utekelezaji malengo kusudiwa na sio kutufanyia dramas na maonesho ya kuita media na kutoa maagizo na maelekezo kwa kusema tutafanya hiki au kile, lakini hatuoni, utekelezaji.

Mfano tunapo hubiri kuhusu Tanzania ya viwanda, where is the blue print ya Tanzania ya viwanda?, zenye smart objectives zenye malengo ya short term, medium term na long term strategies?. Ili tuwe na Tanzania ya viwanda tunahitaji land, where is the land set out kwa Tanzania ya Viwanda?. Tunahitaji labor, nguvu kazi ya Tanzania ya viwanda jee tumeishajua tutajenga viwanda gani na vya kuzalisha nini ili hiyo mainpower na labor force kuvihudumia hivyo viwanda itayarishwe?. Tunahitaji capital ya kuanzisha hivyo viwanda, kuna strategies gani kuwawezesha Watanzania kuimiliki Tanzania ya Viwanda?, au tunataka kujenga Tanzania ya viwanda lakini viwanda ni vya wawekezaji wageni, vya Mchina, Mhindi na Mzungu?, na Mtanzania kuja kuwa ni kibarua tuu kwenye hiyo,Tanzania ya Viwanda kama ilivyo kwenye Uchumi wa Gesi?.

Tanzania ya viwanda itahitaji malighafi ya viwanda, uchumi wa Tanzania unategemea kilimo, hivyo the biggest industries za Tanzania ya Viwanda zinapaswa kuwa ni agro processing industries, jee tuna mikakati gani ya kuinua sekta ya kilimo, ili izalishe malighafi ya viwanda?, au tunajenga Tanzania ya viwanda vya assembling imported components, or processing imported semi processed raw materials kama viwanda vya Bhakressa, vinatengeneza juices na kusaga unga wa ngano, lakini malighafi zote ni imported products, zinatoka nje!, hadi pulp ya mango juice tuna import, huku maembe ya Unyanyembe na Lushoto yakiozea mitini!. Tangu tumeanza kuhubiri wimbo wa Tanzania ya Viwanda, where is the blue print?, what is the plan?, tuko wapi, tumefanikisha nini? , tumekwama wapi and what is a way forward? .

Badala ya kuwahimiza ma bullies, impersonators, impostors na forgerist kuchapa kazi, tupewe matokeo ya hizo kazi zinazochwapwa, watu wanataka matokeo, na sio tuu kupokea maagizo na maelekezo tuu,kwa vitendo vya kuona sifa kutokelezea tuu kwenye TV huku wakitoa maagizo, maelekezo, na kuandikwa magazetini, sasa tujikite kwenye utendaji unaozingatia matokeo, na sifa zisiwe katika kutoa maagizo, bali ziwe katika matokeo ya utekelezaji wa maagizo hayo.

Tuanze ku demand kuonyeshwa results oriented events nini kilichofanyika na sio kututengenezea maigizo ya matukio. Kila siku tunaonyeshwa jinsi viongozi wetu wakizindua miradi, Viwanda, etc, lakini hatupewi mrejesho wowote hiyo miradi imeleta faida gani kwa wananchi na maendeleo ya taifa. Badala ya kuonyeshea viongozi wanasema nini na wanafanya nini, tuonyeshwe matokeo, results oriented actions.

Nakamilisha taratibu za kurusha Vipindi Maalum vya TV vitakavyoitwa "Kwa Maslahi ya Taifa" ambavyo vitaangazia nini kimefanyika, nini kifanyike kuitoa Tanzania hapa ilipo kwenda kwenye Tanzania tunayoitaka.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Hapa Pascal ulijilipua kama vile Magufuli hayupo. Umeongea ukweli mtupu ambao utaishi milele. Hongera.
 
Wanabodi,

Leo siku ya Machi 17 ndio siku Taifa tulipotangaziwa kifo cha Shujaa wetu JPM, hivyo katika kumkumbuka, na kumuenzi, mnaonaje tukijikumbusha baadhi ya mabandiko ambayo tulimshauri JPM na ushauri huo ukafanyiwa kazi, kwa kutaja Bandiko, ulishauri nini, na nini kilikuja kufanyika kwa ushauri huo, na jee kulisaidia JPM? Kulisaidia nini?

Kwa vile JPM alikuwa ni mbabe kwa kufanya baadhi ya mambo kibabe, hadi kutafsiriwa ni dikiteta, hivyo baadhi ya ushauri kwa JPM pia ulitolewa kibabe kwa kumpiga Spana za kutosha, ila tukubali tukatae, Spana za JF zilimsaidia sana JPM na kulisaidia taifa.

Kumuenzi JPM, naomba tujikumbushe baadhi ya mabandiko, tuliwahi kushauri nini kwa kuandika nini na kutoa ushauri wa nini kifanyike, na kufuatia ushauri huo, nini kilifanyika na jee kilimsaidia JPM?kilimsaidia kivipi?. Jee kililisaidia taifa?, kililisaidia kivipi?

Hili ni moja ya mabadiliko hayo ambalo limemsaidia sana na kulisaidia taifa.

Na mwisho kwa vile sasa Samia ndie Rais wetu, JF tunapaswa kuendelea kutimiza wajibu wetu kwa kumsaidia Samia, kwa vile JPM alikuwa ni rais mbabe vivyo hivyo ushauri ulitolewa kibabe, lakini Samia no Mtaratibu, mstaarabu, jee licha ya utaribu na ustaarabu, Mama Nate tumpige Spana kama za JPM? au twende naye taratibu kama alivyo, kwa Mama iwe ni kumkuna tuu, na tusimpare kama alivyo shauri mwenyewe, kuwa ukinikuna vizuri nitakukuna ila ukinipara, nitakuparua?

Mabandiko mengi ya kuwakumbuka marehemu huishia kwa RIP kumuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi kwavile wanakuwa hawajui marehemu yuko wapi,, lakini mimi kwa vile tayari nimeisha kulishwa JPM yuko wapi Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani bado kuna haja ya kuendelea kumuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi huku tayari najua yuko peponi?.

Pumzika Magufuli Pumzika! Tutakukumbuka Daima!

Paskali!
 
Mimi nilikuwa nakosoa na kushauri Swali kwa Viongozi/Wanasiasa Wetu: Kama Waliuona Udhalimu wa Awamu Iliyopita, na Wakaunyamazia, Is it Right Kuusema Sasa au Waendelee Kunyamaza?.
Pascal tumia akili kama msomi. Ulitaka waseme wauawe, wapotezwe, wabambikiwe kesi za uongo? Tumia akili!

Nipe thread yako yoyote uliyomkosoa Magufuli Kwa ukali
Utamkosoaje bosi wako kwa ukali?.
na kumpa ukweli kama Ben saanane alivyofanya kuhusu PhD ya mchongo.
Kuna wengi humu wanadhani kupotea kwa Ben Saanane ni shauri ya issue ya Ph.D ya mchongo!. Not necessarily!.
Ben alikuwa na computer program ya kufanya election tallying verification.
Baada ya matokeo ya uchaguzi, akafanya verification kutumia matokeo ya kura za urais, akajumlisha kura zote valid, plus invalid akapata total votes counted, kisha akatoa idadi ya waliojitokeza, akapata idadi ya kura fake zililiongezwa!. Lile bandiko sijui kama bado lipo humu!.
Hii documentary evidence by computing ni very dangerous then PhD ya mchongo!.
Nawe ulikaa kimya na uliposema ulisifia kupata uteuzi
Kati ya watu ambao hatukuwahi kukaa kimya, mimi ni mmoja wao.
Japo ni kweli baadae Blaza wangu ali changes for the better na mimi nikawa namsifu genuinely
P
 
Wanabodi,
Sisi Wana mitandao tumeshauriwa kuitumia mitandao kulisaidia taifa letu kuendelea, hivyo huu ni ushauri wangu.

Ili Tanzania tuendelee kwa kupata maendeleo ya kweli, na sio maendeleo kiini macho, tunahitaji kujenga taasisi Imara ( strong institutions), zenye mifumo imara, ( an effective systems) ambayo inakuwa automated,

Nakamilisha taratibu za kurusha Vipindi Maalum vya TV vitakavyoitwa "Kwa Maslahi ya Taifa" ambavyo vitaangazia nini kimefanyika, nini kifanyike kuitoa Tanzania hapa ilipo kwenda kwenye Tanzania tunayoitaka.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Tanzania is amongst the most blessed countries in the world.
Mkuu DEU87 , kwanza asante sana kwa mada hii, naunga mkono hoja, Tanzania ni nchi iliyobarikiwa sana tuu, ila...
Karibu mitaa hii, hili tumelijadili sana humu Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows! na hapa Je, maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu au vitu? Wachumi tusaidieni, uchumi wa Awamu ya 5, unalisaidia Taifa au utaliangamiza?
Pia niliwahi kuuliza maswali haya humu Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya informed decision au tutachagua tuu? na swali hili Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya informed decision au tutachagua tuu? na hili Elections 2015 - Ikitokea CCM ishinde, Je ushindi huo ni kutokana kuwekeza kwenye Maendeleo au kwenye Ignorance?
Tunahitaji mjadala wa kitaifa, nchi yetu nimebarikiwa sana, tuna almost kila kitu!, tunakwama wapi?.
p
 
Wanabodi,

Ili Tanzania tuendelee kwa kupata maendeleo ya kweli, na sio maendeleo kiini macho, tunahitaji kujenga taasisi Imara ( strong institutions), zenye mifumo imara, ( an effective systems) ambayo inakuwa automated, ikitokea kuna jambo lolote haliko sawa, the system itself, will detect na hapo hapo kuwa ejected out of system, straight away,

What are Priorities Zetu, Tanzania?. Nini ni Vipaumbele Vyetu? .
Taifa linakabiliwa la viongozi wasio na vision hivyo kukosa mission to accomplish, we seriously lack visionary leaders ndio maana karibu kila kitu ni mpaka rais aje!. Je nini vipaumbele vyetu?, Tanzania kama nchi inayotaka maenddeleo ya kweli, tunatakiwa tujue ni nini tunataka na tutapataje. Kama hujui unachotaka, huwezi kutafuta maana hujui utafute nini!. Ukiishajua unataka nini, ndipo unajipanga utapataje hicho unachokitaka na njia za kukitafutia ili ukipate!. Ukiisha kosa vision, huwezi kuwa na mission to accomplish ya unatekeleza nini, hivyo tumekuwa ni nchi ya kuendeshwa na matukio.

Ushauri wa A Way Forward and What to do.
Serikali yetu, kila wizara, kila idara na kila wakala, lazima ziwe na mission na vision statements, accompanied by a list ya Strategic Objectives ambazo ziko SMART (Specific, Measurable, Attainable, Realistic, Timely). Pia ziwepo timeline strategy ya utekelezaji hizo smart objectives, hivyo viongozi wajitokeze kutueleza na kutuonyesha achievements ya utekelezaji malengo kusudiwa na sio kutufanyia dramas na maonesho ya kuita media na kutoa maagizo na maelekezo kwa kusema tutafanya hiki au kile, lakini hatuoni, utekelezaji.

Tuanze ku demand kuonyeshwa results oriented events nini kilichofanyika na sio kututengenezea maigizo ya matukio. Kila siku tunaonyeshwa jinsi viongozi wetu wakizindua miradi, Viwanda, etc, lakini hatupewi mrejesho wowote hiyo miradi imeleta faida gani kwa wananchi na maendeleo ya taifa. Badala ya kuonyeshea viongozi wanasema nini na wanafanya nini, tuonyeshwe matokeo, results oriented actions.

Nakamilisha taratibu za kurusha Vipindi Maalum vya TV vitakavyoitwa "Kwa Maslahi ya Taifa" ambavyo vitaangazia nini kimefanyika, nini kifanyike kuitoa Tanzania hapa ilipo kwenda kwenye Tanzania tunayoitaka.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
1. Kwanini sisi kama nchi tunashindwa kuendesha baadhi ya mambo yetu likiwemo la bandari linaloleta shida sasa?

2. Kama tulijiuliza, then tulipata sababu ni zipi? Na way forward ili kutoka hapa tulipo ni nini?

Kwa sababu mfumo wetu utawala wa nchi umejengwa katika msingi huu mbovu na WA hovyo kabisa...

Na kimsingi hili ndilo tatizo kubwa tulilonalo kama nchi na ndiyo msingi wa matatizo yote. Na Kamwe ishu siyo kuwa Watanzania hawezi kuendesha mambo yao kwa ufanisi na kuleta matokeo...

Bali wamefanywa hivi na mifumo yetu ya hovyo na dhaifu ya kisheria na kikatiba iliyozaa mfumo mbaya na wa hovyo na dhaifu wa utawala wa nchi yote...

SULUHISHO:

NI KATIBA MPYA itakayozaa MFUMO MPYA WA KISIASA na KIUTAWALA katika nchi na kutengeneza TAASISI IMARA..
Mkuu Uzima Tele , karibu pande hizi, tumeisha jiuliza sana haya mambo.
P
 
Mkuu Uzima Tele , karibu pande hizi, tumeisha jiuliza sana haya mambo.
P
Umesoma ukanielewa kweli?

Reference ya maswali nilyokuuliza ni article yako kwenye gazeti la Nipashe uliyoikopi na kuipest humu wewe mwenyewe..

Kwa hiyo, hiki ulichoandika hapa siyo jibu la maswali yangu..

Baada ya kujiuliza, ukapata sababu gani? Je, based on those reasons, unadhani suluhu ni hiki kinachofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na waziri wake Prof. Makame Mbarawa [wote Wazanzibari] kuwapa waarabu wa DP World [Dubai] bandari zote za bahari na maziwa na za mito za Tanganyika akiziacha za kwao Zanzibar?

Hizo za Zanzibar zinafanya vyema siyo? Na unajua kuwa ishu bandari ni jambo la kimuungano na linapaswa kuendeshwa, kusimamiwa na mamlaka moja ya muumgano?

Kama ni hivyo kwanini mambo yanakwenda hivi??
 
Back
Top Bottom