Kupata kura 1 kituo cha Mgombea na mwenzi wake...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929
Jamani hivi ndoa hii iko salama kweli. Wameenda kwa shangwe kupiga kura ya udiwani, kura zimehesabiwa kura ya mama iko moja tu ya kwake, mumewe hakumpigia kura! Ndoa iko salama au ni siasa tu?
 
Atasema wamechakachua kura kama yaliyowahi kumsibu Lyatonga na Mzee wa Mapesa !
 
Jamani hivi ndoa hii iko salama kweli. Wameenda kwa shangwe kupiga kura ya udiwani, kura zimehesabiwa kura ya mama iko moja tu ya kwake, mumewe hakumpigia kura! Ndoa iko salama au ni siasa tu?

Mzee:: Jimbo la Ubungo :: Kituo cha Sinza (Int'n School)?
 
Ashukuru mungu hata hiyo moja kaipata,ndugu zetu CCM wazanzibar wanaiba hata kura uliyojipigia mwenyewe ili utoke na sifuri kabisa.
 
Kama hutaweza kuthibitisha kwamba kuna uchakachuzi, ndoa inaota mbawa fasta...
 
hehehehe mambo juu ya mambo uchaguzi mwaka huu burudni tupu
kuhesabu kura kumekosa demokrasia kabisa hii ni kwa kuwa watendaji wa tume wanateuliwa na raisi hii si sawa kabisa na huko mbele lazima amani itatoweka kama tume haitabadilisha hili.
 
Kwa jinsi kinamama tulivyo,atasamehewa tu kama anajua jinsi ya kushawishi. Manake huyo baba hakufikiria hata kusaidia kulinda kura za mkewe? Hawakuhamasisha hata housegal! Siasa ngumu sana..
 
Jamani hivi ndoa hii iko salama kweli. Wameenda kwa shangwe kupiga kura ya udiwani, kura zimehesabiwa kura ya mama iko moja tu ya kwake, mumewe hakumpigia kura! Ndoa iko salama au ni siasa tu?

Mkuu salamu sana
Hatimaye tumemaliza uchaguzi. Kuna siku ulituambia hapa hakuna kitu kama kuibiwa kura. Una yapi ya kusema kutokana na uchaguzi wa mwaka huu kaka yangu mpendwa. Ukiwa kama watu ambao nawaheshimu sana hapa JF tathmini yako ikoje kwa sasa?
 
Jamani hivi ndoa hii iko salama kweli. Wameenda kwa shangwe kupiga kura ya udiwani, kura zimehesabiwa kura ya mama iko moja tu ya kwake, mumewe hakumpigia kura! Ndoa iko salama au ni siasa tu?
Mwanakijiji....nakuhakikishia hii ndoa iko salama kabisa hapa mama ataeleweshwa na atakubali kushindwa na atarudi nyumbani na kuendelea kumpenda mumewe.......tatizo lingekuwepo iwapo mgombea angekuwa ni baba ....kisha mkewe amnyime kura........
 
Well said kajukuu....

Baioloji itaota mbawa hakika. Ananinyima kura, namnyima baioloji:yield::yield::yield::yield:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom