Kupata kiongozi kama Rais Magufuli anayetumikia na kutumika kwa ajili ya kila mtu ni Baraka na Bahati

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,600
Viongozi wengi wanapopata madaraka ya juu ya uongozi, ugeuka na kuwafanya watu watumishi wao badala ya wao kuwa watumishi wa watu. Wengi wa viongozi hao uingiwa tamaa ya mali za umma bila kujali maslahi ya wengi na hivyo kushindwa kuwatumikia vyema watu wake. Viongozi wa nchi hizo maranyingi wanageuka na kuwa maadui wa watu.

Hali ni tofauti kwa Tanzania, Rais Magufuli ni tofauti sana. Ni kiongozi mnyenyekevu kwa watu anaowaongoza. Ni kiongozi aliyetayari kutumika kwa ajili ya watu wake na kuwatumikia watu wake bila kujali tofauti zao. Ni kiongozi mwenye kila sababu ya sisi kumuita mtumishi wetu. Tumemtuma atutumikie na anatutumikia vyema kwa kadiri ya uwezo wake.

Ni ajabu kuona mtu anahoji uongozi wa Rais Magufuli hasa pale anapojitoa kututumikia na kutumika kwa ajili yetu. Rais Magufuli yupo ikulu, mahali ambapo anaweza kula atakavyo na kufanya atakacho na asifanye kazi yeyote kwa miaka mitano na baada ya miaka mitano anaacha zake na agombanii tena ila Rais Magufuli anasema hapana lazima deni la kuwatumikia na kutumika kwa ajili ya Tanzania alilipe. Mifano ipo mingi ya viongozi waliogeuka mizigo ndani ya nchi zao ila Rais Magufuli kabeba mizigo ya watanzania kwa kuwatumikia.

Kama akitaka, kwa miaka yote mitano ya Urais wake anaweza asifanye ziara yeyote mikoani badala yake anafanya ziara za Dar es salaam tu. Ila akasema hapana watanzania wananidai na wakati wa kampeni ameona wanayomdai na kuahidi kutekeleza. Anatekeleza kwa kwenda kukagua alivyoahidi huko mikoani . Hii ni Baraka kuwa na Rais anayetumikia watu wake wote.

Rais anayejinasibu kwa vitendo si maneno matupu kama Rais wa wanyonge ni Baraka na bahati kubwa kumpata . Kiongozi aliyejitoa kutumika na kuwatumikia wanyonge wote ni Baraka. Ni nchi chache zenye viongozi ambao wapo kulinda maslahi ya wanyonge dhidi ya matajiri na wanyonyaji, Tanzania kama miongoni mwa nchi hizo ni jambo zuri sana. tumemtuma anatutumikia vyema
 
Kila Kiongozi utumika kwa ajili ya kila mtu, kutumika inaweza kuwa in a positive way or negative one,
 
kwa hicho ulichokiandika hapo juu "tittle" napata mashaka kuwa huenda ukawa na utindi wa ubongo

#na kama vipi ifanye hiyo bahati iwe ya ndugu zako/ukoo wenu.
 
Jiwe akijirekebisha kidogo tu baadhi ya TABIA zake atakuwa Rais bora zaidi kuwahi kutokea TZ na Afrika kwa ujumla
Hivi hizi Ngonjera mtaacha lini? Maana kila mtu ujikomba kwa rais anyedhani ndiye, ukimuuliza faiza foxy atakwambia kikwete ndo Bora wakati mohamed anasema Mwinyi, kwa BAK anaamini Nyerere ndo bora , Tuache haya mambo
 
Acha kumpamba huyo nduli na MUUAJI wewe!

Viongozi wengi wanapopata madaraka ya juu ya uongozi, ugeuka na kuwafanya watu watumishi wao badala ya wao kuwa watumishi wa watu. Wengi wa viongozi hao uingiwa tamaa ya mali za umma bila kujali maslahi ya wengi na hivyo kushindwa kuwatumikia vyema watu wake. Viongozi wa nchi hizo maranyingi wanageuka na kuwa maadui wa watu.

Hali ni tofauti kwa Tanzania, Rais Magufuli ni tofauti sana. Ni kiongozi mnyenyekevu kwa watu anaowaongoza. Ni kiongozi aliyetayari kutumika kwa ajili ya watu wake na kuwatumikia watu wake bila kujali tofauti zao. Ni kiongozi mwenye kila sababu ya sisi kumuita mtumishi wetu. Tumemtuma atutumikie na anatutumikia vyema kwa kadiri ya uwezo wake.

Ni ajabu kuona mtu anahoji uongozi wa Rais Magufuli hasa pale anapojitoa kututumikia na kutumika kwa ajili yetu. Rais Magufuli yupo ikulu, mahali ambapo anaweza kula atakavyo na kufanya atakacho na asifanye kazi yeyote kwa miaka mitano na baada ya miaka mitano anaacha zake na agombanii tena ila Rais Magufuli anasema hapana lazima deni la kuwatumikia na kutumika kwa ajili ya Tanzania alilipe. Mifano ipo mingi ya viongozi waliogeuka mizigo ndani ya nchi zao ila Rais Magufuli kabeba mizigo ya watanzania kwa kuwatumikia.

Kama akitaka, kwa miaka yote mitano ya Urais wake anaweza asifanye ziara yeyote mikoani badala yake anafanya ziara za Dar es salaam tu. Ila akasema hapana watanzania wananidai na wakati wa kampeni ameona wanayomdai na kuahidi kutekeleza. Anatekeleza kwa kwenda kukagua alivyoahidi huko mikoani . Hii ni Baraka kuwa na Rais anayetumikia watu wake wote.

Rais anayejinasibu kwa vitendo si maneno matupu kama Rais wa wanyonge ni Baraka na bahati kubwa kumpata . Kiongozi aliyejitoa kutumika na kuwatumikia wanyonge wote ni Baraka. Ni nchi chache zenye viongozi ambao wapo kulinda maslahi ya wanyonge dhidi ya matajiri na wanyonyaji, Tanzania kama miongoni mwa nchi hizo ni jambo zuri sana. tumemtuma anatutumikia vyema
 
kwa hicho ulichokiandika hapo juu "tittle" napata mashaka kuwa huenda ukawa na utindi wa ubongo

#na kama vipi ifanye hiyo bahati iwe ya ndugu zako/ukoo wenu.
hii ni bahati ya Tanzania, sina mamlaka ya kufanya bahati ya umma, yangu binafsi
 
Jpm ni rais mzuri saana isipokua ana mapungufu yake kama vile KUKURUPUKA TU NA KUFANYA JAMBO BILA KUJALI NI ATHARI GANI YATAKAYO TOKEA MBELENI kwa Mfano-UNUNUZI WA KOROSHO NA MENGINEYO,,na kingine zaidi ni UTEKWAJI WA WATU hili swala la waru kutekwa kwa kweli linampunguzia asilimia kubwa saaana ya sifa za uongozi wake
Angejirekebisha na hayo tu kwa kweli angependeka kwa %99‍♂️
 
Chema chajiuza kibaya chajitembeza ,vipi ndugu mbona unahangaika sana kumpamba asiyepambika ,Jiwe kiongozi mnyenyekevu sawa kabisa kama ambavyo alivyotoa hotuba yake ya unyenyekevu kwa wahanga wa tetemeko la kagera au vipi ?akawaambia ukimwi nyinyi ,katerero nyinyi ,tetemeko nyinyi ,Mimi Siva let's tetemeko .Tabora akawaambia kwa unyenyekevu hayo mabango yenu mkayalalie na wake zenu ,DSM mtu atakayefikisha mwezi wa saba DSM atakuwa mwanaume kweli kweli mziandaa suruali zenu za zamani msizitupe ,Msaliti hawezi kusavaivu ,wafukuze huko bungeni halafu Mimi niwashughulikie huku ,watalimia meno ,wasioweza kulipia mia mbili wapige mbizi ,wanaotaka rami wapake kinyesi hizo ni baadhi ya kauli zake za unyenyekevu kabisa mtoa Uzi hongera sana Lumumba kwa kujitoa ufahamu .Hapo sijaenda kwenye utekaji ,mauaji na uchumi .
 
Nawaza Waziri wa Ujenzi katika awamu hii arnde jimboni kwake akajenge traffic lights nini kitamtokea
 
Magufuli is a great leader.

Kuamua kutokuwa mateka wa wazungu si kitu kidogo. Utapigwa vita vya akili. Mataifa ya magharibi ya najua kuna wajinga wengi dunia yetu. Wanawachezea akili na wanaimba na kuicheza nyimbo wasizozijua.

Kwa wasomi, viongozi wa dini, wafanyabiashara, wananchi wa chini, yeye ni jembe. Kumbuka mikutano ya Rais na wasomi UDSM, Mikutano na wafanyabiashara, mikutano na wadau wa madini, nk. Ndiyo mana upinzani baada ya makundi hayo kumkubali, waliamua kuyachafua kwa kampeni za mitandaoni. Eti viongozi viongozi wa dini wamenunuliwa, wanajipendekeza. Wafanyabiashara wanaogopa kutozwa kodi na wanajipendekeza, nk.

Kwa hakika tumepata bahati kumpata huyu. Campaign za kumchafua ndiyo maana bado Zina Impact ndogo.

Waliobaki kumshambulia Magufuli ni majina Yale Yale ya kwenye mitandao, JF ukiongoza.
 
Back
Top Bottom