Kupata hedhi baada ya kujifungua

Ms mol

JF-Expert Member
Mar 31, 2017
1,960
2,336
Wasalaaam.

Ni miezi 9 sasa toka nijifungue mtoto wangu. Sasa sijawahi kubleed kabisa. Na nimeishia Hofu nisije nikapata mimba jamani maana naendelea kukutana na mwenzangu kwa tendo la ndoa kila Mara.

Je, mimba haiwezi kujitungia ndani kwa ndani jamani!

Asante
 
dimaa, Hata sasa hivi sina mimba jamani ila tu nina hofu yai lisijepevuka mimba ikanasa
 
Dr alimuambia ni lactating annorhea ila sikupata nafasi ya kumuuliza swali km kuna uwezekano wa kupata mimba kabla sijaiona hiyo bleed. I'm mean ni yai likikomaa likarutubishwa. Kamwene kamwene,
 
Dr alimuambia ni lactating annorhea ila sikupata nafasi ya kumuuliza swali km kuna uwezekano wa kupata mimba kabla sijaiona hiyo bleed... I'm mean ni yai likikomaa likarutubishwa.
tumia uzazi wa mpango tu uwe salama
 
king otaligamba asante japo nina kahofu eti yai likipevuka na kukutana na mbegu ya kiume ndani kwa ndani si nitapata mimba au vipi daktari wangu.


Mie sio mtaalam lakini nakuelewa sana hofu yako. Kwamba siku hiyo yai ndio limeanza kukomaa na kupevuka ili ndio iwe mwanzo wa kuona siku zako ikatokea likakutana na mbegu za kiume si ndio tayari itakua umekamata mimba? Naona wadau wanasema lazima upate siku kwanza ndio uweze kukamata mimba kana kwamba yai la mara ya kwanza haliwezi kutunga mimba.

Kuhusu kuchelewa kuona siku, kama unanyonyesha vizuri, wengine wanaenda hadi mwaka bila kuona siku, hiyo isikutie hofu.
 
Asante kwa kunielewa barabara The Monk ngoja niwaulize vizuri ten a nielewe Dada Sky Eclat na kaka KING oligamba yai la kwanza halitungishi mimba?
Mie sio mtaalam lakini nakuelewa sana hofu yako. Kwamba siku hiyo yai ndio limeanza kukomaa na kupevuka ili ndio iwe mwanzo wa kuona siku zako ikatokea likakutana na mbegu za kiume si ndio tayari itakua umekamata mimba? Naona wadau wanasema lazima upate siku kwanza ndio uweze kukamata mimba kana kwsmba yai la mara ya kwanza haliwezi kutunga mimba.

Kuhusu kuchelewa kuona siku, kama unanyonyesha vizuri, wengine wanaenda hadi mwaka bila kuona siku, hiyo isikutie hofu.
 
Ni Kwamba hakuna yai linaloweza kupevuka kabla ya kuona siku zako tangu ulipojifungua. Hakuna mechanism hivyo.

Tusaidie na siye tusio na uelewa wa haya mambo Mkuu. Unaposema kuona siku zako baada ya kujifungua si inamaanisha mchakato mzima wa kutengenezwa yai, kupevuka na kutoka kama damu baada ya kukosa kirutubisho?

Swali ni Je, hilo yai la mara ya kwanza haliwezi kutunga mimba?
 
Tusaidie na sie tusio na uelewa wa haya mambo mkuu. Unposema kuona siku zako baada ya kujifungua si inamaanisha mchakato mzima wa kutengenezwa yai, kupevuka na kutoka kama damu baada ya kukosa kirutubisho?

Swali ni Je, hilo yai la mara ya kwanza haliwezi kutunga mimba?
Nikwambie tu. Hedhi haitokani na yai kuharibika. Ila tu Kama yai litakuwa limekuja likakosa mbegu za kurutubisha basi litaharibika baadaye litatoka Kama damu pamoja na hedhi.
 
Nikwambie tu. Hedhi haitokani na yai kuharibika. Ila tu Kama yai litakuwa limekuja likakosa mbegu za kurutubisha basi litaharibika baadaye litatoka Kama damu pamoja na hedhi.

Bado tunaongea lugha moja hadi hapo, swali ni Je, hilo yai la mara ya kwanza baada ya kujifungua anaweza kupata ujauzito?
 
Back
Top Bottom