Kupandishwa umeme na kodi za kikatili kwa watanzania ni kifungu kipi cha ilani ya uchaguzi ya ccm

Pakawapakawa

Senior Member
Nov 19, 2012
110
170
Wapendwa wanachama wenzangu na hasa Mhe. Nape na Mwigulu, tujuze ni vipengele vipi ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM vinaruhusu kupandishwa umeme kwa asilimia 85 na kutozwa kodi wananchi kwa kiwango tunachoshudia sasa. Ukweli tunanyanyasika mitaa kwa kuambiwa ni matokeo ya Ilani ya Chama chenu. Je kuna ukweli wowote?. Ninauliza swali hili baada ya kuona ziara zote za Katibu mkuu na nyie mlioambatana naye hakuwai kukemia masuala yaha!.
 

Gwankaja Gwakilingo

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
1,991
2,000
Tumeyataka maana tuliambiwa tukashupaza shingo zetu wacha tukione cha moto sasa......ndo shida ya kuongozwa na mizigo
 

blueray

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
2,217
0
Waulize kwanza Ufisadi upo kipengele gani cha ilani halafu utafakari mwishowe utajua
 

Erwin Rommel

JF-Expert Member
Dec 1, 2013
429
195
Pia waulize CCM ile opresheni yao ya mauaji ya wananchi ilikuwa katika kipengele gani cha ilani hiyo ya CCM?
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,536
2,000
CCM ni wavivu wa kufikiri, wavivu wa kubuni njia mpya. Wanajua njia kuu mbili tatu baasi. Bia na sigara, kodi ya PAYE. Mengine ni kukisia tu bila kuyafanyia utafiti wowote.
Wawekezaji, wanatamani walipe kodi kama kule kwao lakini sisi tunawaambia watufichie kuleeeee uswiss. Wale tunao wakamua kodi, kwa vile ni wachache haitoshelezi hivyo vyanzo mbadala tuna warudia wale wale walala hoi. Tunaongeza bei ya mafuta na umeme. Kwani waliwahi kusema hawawezi kulipa? Viongozi pamoja na hayo ma allowance s kibao lakini pia mafuta ya bure na hata chakula nyumbani bure. Atajua kweli mlala hoi? Fikiria vizuri
 

Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,562
2,000
Wacha bei ipandishwe ifike sh 1,000/ kwa unit moja , maana bado Watanzania wamelala usingizi labda wanaweza kuzinduka kwa hili.Wapinzani wakiwatetea wao wanaziba masikio.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom