Mroojr
Member
- Nov 15, 2010
- 65
- 8
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na EWURA ni kwamba wamewakubalia Tanesco kupandisha gharama za matumizi ya umeme kwa 18.5%. Hebu tujiulize je kutabadilika nini? Wameshawahi kupandisha gharama hizi mara chungu nzima lakini hakuna badiliko lolote, mgawo uko pale pale,hakuna umeme wa uhakika,bado twaendelea kutegemea maji ya mvua hafifu kutupa umeme, hawana programme zozote za kuondokana na kutegemea umeme wa maji usio wa uhakika. Sasa je hizi gharama tunazoongezewa zinafanya kazi gani? Tunanufaika nini? Au ni kuwalipa Dowans?