Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,561
- 19,056
Kumekua na kawaida kwa watu wanopandisha majini au mashetani au maruhani au mizimu kudai au kudaiwa kua na uwezo wa kuzungumza lugha ngeni isiyofahamika na yule mtu ambae jini linapanda kichwani mwake na kumposes kwa muda flani wenyewe wakimwita kiti. Kwamba utakuta mtu hajawahi kujifunza labda kimasai au hata kiingereza lakini akipandisha huyo jini au mzimu wenye asili ya kizungu au kimasai utakuta eti na yeye anaongea lugha hizo.
Kwa utafiti nilioufanya jambo hilo sio kweli. Katika hili kuna mambo mawili tu. Ama huyo kiti anafahamu hiyo lugha ambayo jini anaitumia, au kama kiti hajui kabisa lugha husika basi ataongea makorokocho kwa lafudhi ya lugha hiyo na watasema hiyo ndio lugha yenyewe, hasa kama katika wasikilizaji hakuna mtu anayeijua. Kwa mfano kama kiti anafahamu kuongea kiingereza broken basi huyo jini ataongea pia kiingereza broken
Hapa sipingi taarifa wanazozitoa kama ni sahihi au sio sahihi (maana kwa utafiti wangu wengine hutoa taarifa sahihi ya mambo yaliyotokea bila ya kua wameelezwa au kuyajua kabda). Ninachokisema na kutoa changamoto ni kwamba lugha watakayoitumia ni ile ambayo kiti anaijua kwa ufasaha na kama anijua kwa kubabaisha na jini ataongea kwa kubabaisha. Natoa changamoto kama kuna mtu anaweza kutoa ushuhuda tofauti na aka prove laki moja ya krismass kutoka kwangu inamsubiri