Kupanda kwa thamani ya Tsh. dhidi ya Us. dola kunaashiria nini? (kutoka 1800---1584 within a month) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupanda kwa thamani ya Tsh. dhidi ya Us. dola kunaashiria nini? (kutoka 1800---1584 within a month)

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by ngwendu, Dec 22, 2011.

 1. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka shilingi ya tanzania ilishuka nakufikia thamani ya 1800 kwa dola moja ya Us na sasa imepanda na imefikia 1584 leo. hii inaashiria nini? kipindi ikishuka thamani kila siku zilikuwa zinakuja threads mpya kuripoti hilo lakini mbona sasa wale maripota wetu hatuwaoni? tunawashauri pia wendelee kuripori kama walivyokuwa wakifanya hapo awali.
  Na mwishi kabisa ambalo ndo lengo la thread hii, ni kuwa inaashiria nini? wataalamu wa uchumi hebu tusaidieni sisi wauza machungwa huku mtaani.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Source???

  Ngoja Niangalie online«»XE currency
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Du Ebwana kweli,Tsh imepanda zidi ya USD ni 1584
   
 4. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,227
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Mkuu Hiki ni kipindi cha mapunziko, biashara nyingi zinafunga hadi January, so no much use of foreign currency this month. kwa sababu hiyo lazima foreign currecies zitapungua thamani kwa sasa lakini haimaanishi Tsh imepanda thamani. Kuthibitisha hilo angalia bei ya vitu soko la ndani je na vyenyewe vimeshuka bei au la? hapo ndo utajua kama shilingi bado inaporomoka au inainuka.

  Kitu kingine subiri ikifika januari 15 na kuendelea wakati biashara nyingi zinafunguliwa tena, utaona kama Dola itabaki hapo pa 15xx au la.

  conclusion: Shilingi haijapanda thamani hata kidogo, with comparison na Local market, Dola haijashuka thamani ila kwa mwezi huu wa mapumziko watumiaji wa Dola hawapo.

  Kama una Tsh zisizokuwa na kazi huu ni wakati wako mazuri wa kuwekeza kwenye Dola, Mwezi wa pili mwakani utakuwa na faida sana ukiziuza.
   
 5. K

  KyelaBoy JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 9, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukienda madukani kununua vitu kama computer wenyewe huuza kwa dola,dola 1 ni sawa na Tsh 1640 kwa hiyo mambo baado yako palepale huo unafuu haupo
   
 6. Dero

  Dero JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 324
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kinachotokea ni kwamba Serikali kupitia BoT ime-release fresh dollars sokoni, kawaida BoT huwauzia bank na bank huwauzia individuals na makampuni, lakini kinachofanyika sasa BoT in awauzia individuals like Bureau de change kwa rate ya chini mno, mwisho wa siku bank nao wanalazimika kushusha rate (function of supply nad demand). Lakini hiki kinachofanyika si measurement nzuri ya ku-control exchange rate kwani mara nyingi haidumu, kwani BoT ina maximum foreign reserve haiwezi kuuza USD kila siku, at the same time kati ya wale wanouziwa kwa bei rahishi kuna wengine wanazifadhi wakisubiri BoT itakopoacha kurelease more USD wao wauze kwa bei ya juu. Serikali inatakiwa imaimarishe uuzaji nje bidhaa , yaani tuwe na more export than import, hii ni njia nzuri ya ku-control exchange rate.
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Thanks, ila nasubiri hiyo tarehe 15 january uliyosema. ila kitu kingine ambacho ungenisaidia, mbona watu hawarepoti kama kipindi sh ikishuka? au sisi tunaombeana mabaya tu? mbona naona kama jambo la aibu kwetu waTZ? au mnaonaje?
   
 8. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  Wanasema ukiona mgonjwa mahututi kapata nafuu kaa chonjo...! tafakari
   
 9. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #9
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kimsingi kupanda thamani dhidi ya $ kuna mambo mengi yanaweza yakajitokeza. Hiyo ni njia mojawapo ya kupunguza mfumuko wa bei(Inflation). Je mfumuko wa bei umepungua kutoka kipindi hicho unachozungumzia cha miezi mitatu?. Kama bado basi njia waliotumia kupunguza mfumuko wa bei sio mbadala na mathara yake yataendelea kuzoofisha uchumi wa nchi zaidi ya hapo mwanzo. Kwa kipindi kirefu (in a long run) kijacho Uwezekano ni mkubwa wawekezaji wa ndani wakashindwa kuendesha shughuli zao-hii ni kutokana na gharama za uzalishaji kuongezeka -Riba( Interest rate ) kuwa juu. Pia kushuka kwa mauzo ya bidhaa nje ya nchi (decrease in exports).Pia ukumbuke na ufunguke macho kuwa Tsh haijapanda thamani kutokana na uzalishaji ama exports .Mfano Ksh imepanda thamani dhidi ya $ kutokana na kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa zao nje ya nchi hususani mazao ya kilimo.Kwa hiyo nchini Kenya hali ya uchumi inazidi kuimarika tofauti na nchini Tanzania ambako kuna ongezeko la thamani ya Tsh dhidi ya $ lakini uchumi unazidi kuzorota.
   
 10. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Si kweli kuwa shilingi inapanda. Ukweli ni kwamba Dolla inashuka thamani
   
 11. estson22

  estson22 Senior Member

  #11
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Dah mkuu uko fiti hata kama sikuoni lakini maneno uliyoyaandika mtu anaweza akaakonvisika,thanks you open my mind
  :eyebrows::eyebrows::A S embarassed::shock:
   
 12. estson22

  estson22 Senior Member

  #12
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Teteta hoja yako iwe na mashiko mkubwa
  :A S embarassed:
   
 13. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Noted with thanx.
   
 14. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu lakini umeangalia thamani ya dola juu ya currency nyingine kwa miezi miwili iliyopita kama vile Euro na Pound? Better ungekuwa na data. internet siunayo hebu bofya ndo utoe data zako hizo.
   
 15. R

  Rutatinisibwa Senior Member

  #15
  Dec 22, 2011
  Joined: Aug 22, 2011
  Messages: 105
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Ebi bishuba omu kipindi eki ila Endeleea yagamba amazima umu kipindi eki!
   
 16. R

  Rutatinisibwa Senior Member

  #16
  Dec 22, 2011
  Joined: Aug 22, 2011
  Messages: 105
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Aga mazima omukipindi eki! ninkusima muno!
   
 17. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Gwendu hakuna mwenye wajibu wa kumpasha mwenzie habari. Hii thread uloleta wewe inatosha pia.

  kuhusu tshs yetu kama haikuwa na nguvu kipindi cha msimu wa mazao (pamba,korosho,kahawa n.k hiki unachokiona sasa ni sanaa zo benki kuu tu, tujipe muda.
   
 18. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Ni kweli kiongozi. Mgonjwa akipata nafuu ata omba na uji mwingi siku hiyo lakini baadaye kibao kinageuka!
   
 19. F

  Fideline JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Katika wote walotoa maelezo hapo Dero ndo yuko right.Nadhani kitaaluma Dero utakuwa mchumi.Sababu zilizotolewa za watu kwenda Xmass hazina mashiko.Tuache siasa kwenye mambo tusoyajua.Naomba kuwakilisha!!
   
 20. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wakuu simungeenda kule kwenye private? kwani mpaka muandike hapa kitu ambacho wengi hatukielewi? Ni vizuri kutumia busara kwa kila ulifanyalo.
   
Loading...