Kupanda kwa bei za dhahabu katika soko la dunia, masiha magumu na kuuawa kwa watanzania

WATANABE

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
1,092
466

Mwaka 2009/10, Dhahabu ya Tanzania iliyouzwa nje ni Tani 38 za dhahabu. Katika soko la dunia wakia moja (Troy Ounce) ya dhahabu inanunuliwa kwa Dola 1526. Wakia 1 (Troy Ounce) ni sawa na Gramu 31.1 za dhahabu. Kilo 1 (Moja) ya dhahabu ina wakia 32.1 zenye thamani ya Dola 49,068.00.

Hivyo tani 1 (Moja) ya Dhahabu ina thamani ya Dola 1,526,000.00, hivyo ni sahihi kusema kuwa Tanzania iliuza nje Dhahabu yenye thamani ya Dola za Kimarekani 73,248,000.00 sawa na Shilingi za Kitanzania 113,168,160,000/=. Kutokana na mikataba ya kifisadi Tanzania inapata mrahaba wa 3% tu kutokana na mazuzo ya dhahabu hivyo kati ya Dola 73,248,000.00 zinzotokana na mazuo ya dhahabu Serikali ya Tanzania itapata Dola 2,197,440.00 ambazo ni sawa na Shilingi za Kitanzania 3,395,044,800/=.

Ikumbukwe kuwa dhahabu hii ya Tanzania husafirishwa na kuuzwa nje ya nchi na wawekezaji ambao wamewekwa na Serikali za CCM. Vile vile Serikali za CCM zimewasamehe wawekezaji hawa kulipa kodi mbali mbali zitokanazo na mauzo ya dhabau kama inavyoonyeshwa hapo juu, hivyo kuzidi kuikosesha nchi mapato.

Cha kustaajabisha zaidi Serikali za CCM ziliwasamehe na zinaendelea kuwasamehe wawekezaji hawa hivyo hawalipi kodi ya kuingiza malighafi wanazotumia katika uchimbaji wa madini ikiwemo mitambo, mafuta n.k. Hali hii inazidi kiukosesha nchi mapato ukiachai mbali mapato yanayopotea katika mauzo ya dhahabu nje kama inavyoonyeshwa hapo juu na hivyo kuzidi kuifanya ishindwe kuwapatia wananchi huduma mbali mbali za kijaii, watanzania kukosa ajira kutokana na mzunguko wa fedha hapa nchini kuwa mdogo sana usioweza kuihimili mahataji ya watanzania na hivyo kuchochea umaskini.

Ni katika kutambua hilo, wakazi wa Nyamongo mkoani Mara wameanza kupambana na wawekezaji hawa wanyonyaji ili angalau Serikali za CCM zitambue kuwa watanzania wanaumia sana na hali ngumu ya maisha ili hatiamye wazinduke katika lindi hili la ufisadi ili raslimali za taifa ziweze kutumika kwa manufaa ya nchi na watu wake.

Nchi kama Botswana pamoja na kuchukua mrahaba wa juu zaidi ya Tanzania huiwalazimisha wawekezaji kuipatia nchi hiyo hisa katika shughuli za uchimbaji wa madini, vitu ambavyo kwa pamaoja vinaongeza mapato ya nchi hiyo kutokana na madini.

Badala ya Serikali za CCM kutumia Polisi kuua watanzania wanaoumizwa na hali ngumu ya maisha na umaskini, kwanini isikubali kukaa chini na wananchi na kukubali kutazama upya utaratibu wa matumizi ya raslimali za taifa. Botswana ilifiikia hatua ya kuvunja mikataba iliyokuwepo na wawekezaji wanyonyaji na hawakuthubutu kuondoka.


Buriani Mashujaa wqa Nyamongo, Hongera CHADEMA kwa kuwa wananyamongo katia kipindi hiki kigumu!!!!
 
Back
Top Bottom