Kupanda kwa bei za bidhaa muhimu na gharama ya maisha; Sababu ni zipi na nini kifanyike kukabiliana na hali

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,469
46,000
Kumekuwepo na malalamiko ya muda mrefu sasa bei za bidhaa muhimu kama mafuta ya kula, nishati, vifaa vya ujenzi zimepanda sana katika kipindi cha muda mfupi.

Sababu za kupanda sana kwa bei za bidhaa ni zipi? Kiuchumi

1. Matatizo ya umeme yanaathiri uzalishaji wa ndani kwa kiasi kikubwa?

2. Kodi/tozo ni kubwa na nyingi katika bidhaa nyingi muhimu?

3. Vita vya Urusi na Ukraine ?

4. Uingizaji wa bidhaa kutoka nje una changamoto?

5. Mishahara/ vipato ni kidogo sana?

6. Uzalishaji Viwandani umepungua?


Kwa wabobezi wa uchumi hatua gani za muda mfupi na za haraka zinaweza kuchukuliwa kukabiliana na kupanda kwa bei?

1. Kodi/tozo katika bidhaa fulani ziondolewe au kupunguzwa? Vipi kuhusu mapato ya serikali?

2. Mishahara ipandishwe ? Vipi kuhusu mfumuko wa bei?

3. Uingizwaji wa bidhaa kutoka nje upungiziwe vikwazo?

4. Viongozi watoe matamko na amri kwa wafanyabiashara washushe bei au wasipandishe?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom