Kupanda kwa bei ya vinywaji vya coca cola company

Ally Msangi

JF-Expert Member
Jun 29, 2010
608
120
Hapo jani katika pita pita yangu mtaani nimekuwa nikiskia tetesi kuhusu kupandishwa ghafla bei za vinywaji vya kampuni ya coca cola, tetesi hizi zimenishtusha zaidi baada ya kuona matangazo na posterz nyingi asubuhi hii huku mitaani zikiashiria kupanda huku kwa bei, ambapo kwa sasa soda aina ya coca cola, fanta, sprite, na stone tangawizi zitauzwa kwa bei ya sh 500/=,

swali ni kwamba, bunge la bajeti ndio hupanga bei mpya za bidhaa, sasa iweje bei zinapandishwa kinyemela na wakati bunge la bajet lilisha pitisha bei za bidhaa.
 
Bunge Halipangi bei Bwana...... kazi ya bunge ni kupitisha bajeti. mtu akiamua kupandisha bidhaa yake bei at
any time anaweza kufanya hivyo kwani kunywa soda sio lazima (sio necessity commodity ).
 
Hii post ni ya Mwaka gani? mbona bei hiyo ni miaka miwili sasa tunanunua soda shs 500/-
 
Lazima ipande, kwani serikali siiiliongeza kodi kwenye vinywaji???

Kweli kabisa, kreti imetokea 7300-9100, Gesi kg 15 33,000-42000, umeme hakuna, mkaa hakuna??? je uwiano wa kodi na mfumuko wa bei vinaendana?
 
Hiyo shilingi mia tano ni kwenu huko mjini............huku soda ni shilingi 700 toka wiki iliyopita, kabla ilikuwa 600/=
 
Bei iliyokuwa imependekezwa awali kwa vinywaji vya jamii ya Coca-Cola ilikuwa ni TZS 400, ila kwa kuwa sisi watanzania tunaona ukiuziwa ghali basi wewe ni matawi ndio maana sehemu nyingi haswa uswazi kwa kuwa soda nianasa ndio zikawa zinauzwa TZS 500.

Lakini kwa sasa kampuni ya Kwanza Bottlers wamesema wamepandisha bei kuwa TZS 500 kutokana na kushuka kwa thamani ya shillingi pamoja na kupanda kwa gharama za uagizaji ikiwa pamoja na sukari na gesi ya Carbon Dioxide.

Poleni sana mnaopenda soda na kuwalea walanguzi ndio maana mnauziwa soda kwa bei ya juu mitaani bila majumuisho ya kodi zingine kama Luxury Tax inayokuwa imewekwa kwenye mahoteli.

Ushauri wangu, agiza soda kunywa, toa jero, tambaa... moto nkawashiane polisi post.
 
Hiyo shilingi mia tano ni kwenu huko mjini............huku soda ni shilingi 700 toka wiki iliyopita, kabla ilikuwa 600/=
huku mjini imepanda toka 500/= hadi 600/=......... tangu last week. JK HOYEEEEEEEEEEE.............MALARIA SUGU HOYEEEEEEEEEE................. DSM HOYEEEEEEEE
 
kupanda kwa gharama za uagizaji ikiwa pamoja na sukari na gesi ya Carbon Dioxide.
Ushauri wangu, agiza soda kunywa, toa jero, tambaa... moto nkawashiane polisi.

Kumbe hii gas tunayoipumua(Co2) inaagizwa kutoka nje!!

Wabongo hawakufikishi polisi.watakunyoosha papo hapo.usijaribu utaumia!
 
Ndizi mbivu 1 sh 150
tango sh 300
chungwa sh 150

kuleni matunda wadau. Acheni hizo chemicals. Hivi mnayajua madhara ya peps na coca lakn?
 
Hii post ni ya Mwaka gani? mbona bei hiyo ni miaka miwili sasa tunanunua soda shs 500/-

huko ulipo kuwa ukiuziwa 500 ilikuwa either ni ktk bar au hotels, ila kwa wauzaji wa rejareja mtaani bei kianzilishi ilikuwa ni 400, mpaka hapo jana ambapo imepanda rasmi kuwa 500, sasa huko ulipokuwa ukiuziwa 500 awali sasa itakuwa 600
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom