Kupanda kwa bei ya umeme kuna athari gani kwa maisha ya mlala hoi????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupanda kwa bei ya umeme kuna athari gani kwa maisha ya mlala hoi?????

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babayah67, Dec 24, 2010.

 1. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Jana nimemsikia Waziri Ngeleja akiongelea juu ya ulazima wa kupandisha bei ya umeme wa Tanesco. Waziri alienda mbali zaidi kwa kuwashangaa watanzania kwa nini wanalalamika kupanda kwa bei ya umeme wakati kiasi kilichopanda ni kati ya sh 9 na 28 tu. Kiwango hiki kwa Ngeleja ni kiwango kidogo saana. Kitu kimoja hakukiongelea nafikiri kwa makusudi mazima. Nacho ni nini maana yake unaposema umepandisha bei kwa sh 9 hadi 28??

  Cha kwanza hapa tunatakiwa tujue kuwa hii ni ongezeko la bei kwa kila unit moja ya umeme. Kwa tulio wengi tunatumia umeme zaidi ya unit 50 kwa mwezi, hivyo ongezeko letu ni sh 28 kwa kila unit, sasa kama unatumia unit 250 kwa mwezi ni sawa na ongezeko la sh 7000/= kwa mwezi mmoja, hiki kwa Ngeleja ni kiwango kidogo saana. Hii ni DIRECT INCREASE ya gharama ya maisha kwa mlalahoi. Lakini pia kuna INDIRECT INCREASE ya gharama ambazo Ngeleja hakuzitaja kwa makusudi kabisa. Hapa inatokana na gharama zote zinazotokea kutokana na matumizi ya umeme mfano, ukienda kunyoa, saloon, ukinunua mkate, unga wa sembe, bei ya maji ya kunywa na kila huduma unayoijua kuwa inatumia umeme. Maana mwenye kutoa hiyo huduma atafidia ongezeko la bei ya umeme kwa kuongeza bei katika huduma zake. Hili tunaliona tayari mfano katika bei ya maji ya Uhai ya chupa kubwa ya lita 6, bei imepanda toka sh 1000/= hadi 1200/=. Ngeleja alitakiwa pia azungumzie vitu kama hivi.

  Akimalizia hiyo jana Ngeleja anawashangaa wote wanaotaka kuandamana ati kupinga ongezeko la umeme wakati kilicho ongezeka ni kiasi kidogo saana. Mi namwambia NGELEJA kiasi kilichopanda kwako ni kidogo saana kwetu ni kikuubwa saana. Yeye hapo alipo halipii chochote katika Umeme, Maji, Usafiri, Nyumba hata amewekewa mfanyakazi wa ndani kwa pesa ya walala hoi, hivyo hajui adha gani tulizonazo akina sie. Atuache tuandamane tuelezee machungu yetu tunayokabiliana nayo kutokana na adha hii.

  Ukiangalia kwa undani saana matatizo yaliyopo Tanesco yanatokana na kuidai pesa nyingi saana serikali, kama Tanesco wangeamua kuwabana Serikali iwalipe madeni yake yote leo hii kusingekuwa na ongezeko la bei wanayotaka kuiongeza. Fikiria ofisi za serikali zote, anzia mawizara, ikulu, magereza, mashule, hospital na majumba yote wanayokaa viongozi wa serikali kama mawaziri. Hawa wote wangelipa kama tunavyolipa kila kukicha akina sie tanesco hawatakuwa na shida ya pesa.:angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry:
   
 2. I

  Igwachanya Senior Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 142
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Asante kwa uchambuzi wako makini. Hivi hawa mawaziri wa Mkwere nafikiri DAWA wanazotumia ili waendelee kubakia madarakani nahisi zimewadhuru. Kauli zao si za watu
  wanaojiita viongozi kwani hawawakilishi mtazamo na ukweli tunaouhitaji kama watanzania

  We are paying the price of embracing ccm. Mind you, this is just gear no.1, how about gear no.5? I cant imagine how unbearable life will be!

  Dr Slaa once said, re-electing CCM is a disaster. His prophesy is undeniably featuring not only to pro-CDM, but thithi emu (CCM).

  Tutakaza mikanda hadi viuno vitukatike. Tutakonda hadi maumbile yetu yatafanana na "rock pedestal" kutokana na njaa na utapiamulo kwa makundi yote kwani kama hujawahi ona utapiamulo kwa watu wazima, kila mtu asubiri aone.
   
 3. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye nyekundu, yeye na familia yake halimhusu ndo maana anashabikia na hajui hali halisi ya maisha ya mtanzania wa kawaida.Yaaani ndugu yangu sijui nafuu ya mlalahoi itapatikana lini? kwa kweli inasikitisha saana.
   
 4. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hao ndiyo mawaziri wa JK bwana!!!!... Hiyo ndiyo Top cream ya CCM!!!! Hawajui hata kusoma alama za nyakati!!! Wanafikiri watanzania wa leo ndo walewale wa mwaka 47!!! Hawa watu wanachefua mfano hakuna!!!!!
   
 5. I

  Igwachanya Senior Member

  #5
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 142
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Also among academic institutions which should pay heavily the price for backing CCM is UDOM. I got surprised when I heard and saw students of UDOM boycotting, they played a tremendous role to enabling CCM retain its terrorism. Since then, the credibility of this politic university to many Tanzanians with good faith to their nation has dramatically gone down.

  My take; Police piga sana hawa kwani wanamdai nani matatizo yao kwani ujinga wao ndo unawaumiza
   
 6. d

  dotto JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  (1) Kunaongeza uwajibikaji

  (2) kunaongeza wawekezaji wa viwanda

  (3) Kila duka na nyumba inakuwa na Tanesco yake

  (4) Price per Unit inaongezeka.

  (5) Nguvu inaamia kwenye flyover

  (6) Watu wanakuwa wanawahi home toka makazini kwao bse hakuna umeme.

  (7) Environmental protection bse of Generator emissions inakuwa imezingatiwa maana Govt wako makini sana hasa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira.

  (8) Environmental Protection inakuwa imelindwa sana maana mkaa unakuwa wa maana sana mjini. Si lazima kupikia umeme mambo ya kizungu.

  (9) Tanesco inakuwa sasa inajikita kutengeneza miundo mbinu yake maana umeme utakuwa haupo kwa kipindi hicho chote.

  (10) IPTL, Dowans and Songas kama wawekezaji muhimu na aghali sana wanapata chao

  Nawasilisha!!
   
 7. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  umeme ukipanda mbona ni kasheshe kwa mlala hoi? machine za kusaga unga bei inaongezeka pia huku kwetu. haijalishi ni ya umeme au mafuta kwa kuwa hao wauza mafuta pump zao zatumia umeme. viwanda pia vitaongeza bei ya bidhaa zao kwa kuwa umeme kitakuwa chanzo. alieshiba hamkumbuki mwenye njaa guys
   
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kondom nazo zitapanda bei.......

  Ze Bingwa, Ze kili, Ze Konyagi, Ze Serengeti, Ze ndovu hata Ze Chibuku la kwetu nalo litakuwa halishikiki.....

  Airport Charge itapanda bei............ ahhhh, wengi hatupandi ndege.
   
 9. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  ....hii ndio tataizo la watanzania wachache wenye uwezo wa kubadilisha mambo wanapo-politicize mambo. wengi wetu tumeshakombolewa fikra kwa kumtambua adui wetu (CCM)..bado NEC, TISS, PFT (Police Force of Tanzania).
   
Loading...