Kupanda ghafla kwa bei ya saruji

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Bei ya saruji kwa siku za karibuni imepanda mpaka wananchi wamebaki kushangaa ni kwa sababu gani hali hii imetokea na juzi tu ndo tumeipigia CCM kura za kishindo. Walitaka tuwapigie kura kwanza ndo bei ya saruji ipande?. Tungejua mapema tusingeipigia CCM kura za kishindo. Athari za kupanda kwa saruji ni haya yafuatayo:-

(1) Wananchi waliokuwa wanajenga sasa hivi ujenzi umesimama.

(2) Wenye magari yanayosomba mchanga sasa hivi magari karibu yote yamesimama.

(3) Wauzaji wa matofali hawana wateja.

(4) Wauzaji wa jumla biashara yao imekuwa taratibu sana.

(5) Machinga wanaotegemea kupata mapato kwa kuteremsha mifuko ya sementi sasa hawana kazi.

(6) Machinga wanaotegemea kupakia mchanga kwenye magari sasa hawana kazi tena.

(7) Serikali inaendelea kukosa kodi kutokana na kuadimika kwa saruji. Kutokana na sababu nilizozieleza hapo juu ni wakati muafaka kutueleza sisi wananchi ni kwa sababu gani saruji imepanda ghafla hivyo na iweze kuchukua hatua za haraka sana kurekebisha kasoro hiyo.
 
Machinga anajulikana Kama mfanyabiashara ndogo ndogo, either kwa kutembeza mtaani au kukaa sehemu moja
Huyo unaemdhamilia hapo ni mkuli au mbeba mizigo
 
Saruji haijapandishwa na CCM bali imepanda baada ya kwa kiwanda cha Dangote kufungwa kwa ajili ya ukarabati bila kutoa taarifa kwenye mamlaka husika....




Cc: mahondaw
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom