Uchaguzi 2020 Kupanda bei ya sukari na uhaba wa mafuta kuelekea Uchaguzi Mkuu

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
14,923
19,614
Wakati ikijulikana wazi mwezi wa nne viwanda vya sukari vitasimamisha uzalishaji kulitokea uhaba mkubwa wa sukari ambao ulisababisha bei kupanda pamoja na juhudi za serikali ikiwa ni pamoja na kuagiza sukari Uganda na kutoa bei elekezi bado bei haijashuka.

Jana tumesikia malalamiko ya wafanyabiashara wa ifakara kukosa mafuta wanapoenda kununua mafuta kipindi hiki hali inayopelekea uhaba wa mafuta na bei kupanda

Kwanini hali hii inahusishwa na uchaguzi, akiba ya mafuta inajulikana pia kuna vyombo kama ewura ambao ni kazi yao kusimamia bei na kufatilia bei elekezi ila kwanini wafanyabiashara wanapata ujasili wa kuficha bidhaa na kupandisha bei.

Ukiangalia kwa jicho la tatu haya mambo yana uhusiano mkubwa na uchaguzi mkuu tafakari.
 
Factors ni nyingi moja pia wafanyabiashara uogopa kuweka hela zao kwenye mzunguko kuhofia risk yeyeto sababu Siasa za afrika hazitabiriki
 
ngoja nipite maana me mfanyabiashara nikichangha itakula kwangu hebu tuendelee kuisifia awamu ya tano kwa kutuleta hapa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom