Kupambana na Serikali kwa maneno ya kuzusha ni dalili ya upinzani kukosa hoja

Suala la dangote sio tatizo la kiufundi, wewe ndo unaleta propaganda hapa
2016-11-30 12.54.50.png
 
Mbona Makonda nilishamshinda siku nyingi sana!
1.Hawezi kuwa bright kama mimi
2.Hawezi kuwa na proper management skills kama zangu
3.Hawezi kupata kazi kwa kuzingatia weledi na performance.
4.Sikuajiriwa kwa kupiga Waziri Mkuu.
5.Nimefanikiwa kwa kutumia elimu niliyonayo,uwezo wangu na kuheshimu wakubwa na wadogo.
6.Sijazoe kuropoka hovyo mikutanoni.
7.Nina weledi unafaa kuigwa na jamii yangu.
8.Ninajitambua kwa asilimi 100
9.Ninajua haki zangu kama raia na mfanyakazi.
10.Ninamuogopa sana Mungu aliyenipa uhai.
Na mengine mengi ambayo nina uhakika kwa asilimia 100 nimemzidi Makonda sana tu
Wewe siyo size ya Makonda mkuu. Chuki zako binafsi dhidi yake unapoteza muda. Hata hivyo unatupoteza muda kama unataka anzisha mada yako na Makonda, hapa siyo mahali pake. Mapovu kibao yanayokutoka hayatasaidia kitu, Makonda ni RC wewe na njaa zako utakufa bure na pressure jambo la msingi jipange tu na wewe mkono upate kwenda kinywani. Kama mlisoma wote, wewe kuwa mpole tu ndo umeshapigwa gepu hivyo.
 
Wewe siyo size ya Makonda mkuu. Chuki zako binafsi dhidi yake unapoteza muda. Hata hivyo unatupoteza muda kama unataka anzisha mada yako na Makonda, hapa siyo mahali pake. Mapovu kibao yanayokutoka hayatasaida, Makonda ni RC wewe na njaa zako utakufa bure na pressure. Kama mlisoma wote, wewe kuwa mpole tu ndo umeshapigwa gepu hivyo.

Na siwezi kuwa size ya Makonda,sababu ninahekima busara na uwezo wa kuongoza kuliko Makonda.Hivyo asilani siwezi kuwa kama huyo mropokaji wenu.Ni bahati nzuri sikusoma na mtu asiye na uwezo kama yeye
 
Tunataka serikali ya viwanda mliyoahidi... acheni maneno ya uongo uongo kila mnapopewa nafasi ya kuongoza. Mmekuwa mkitumia mbinu hizo hizo kwa miaka zaidi ya 50 huku nchi yetu ikiendelea kutopea kwenye umaskini.
 
kwamba serikali imekula rambirambi za wana kagera, kwamba serikali imefuta ajira, kwamba serikali imefuta mikopo elimu ya juu, kwamba serikali imefuta mikutano ya kisiasa, kwamba serikali imefuta bunge live, kwamba hospitalini hakuna madawa na chanjo,kwamba serikali imefirisika, kwamba ni dikteta uchwara..........................
 
Tangu kuingia Madarakani kwa Serikali ya Awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Vyama vya upinzani hususan chama kikuu cha Upinzani cha CHADEMA kimetoa maelekezo kwa vijana wake walioko katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuandika taarifa za uongo dhidi ya serikali.

Maelekezo yenye lengo la kudhoofisha kasi ya utendaji kazi wa serikali ya Magufuli yamekuja baada ya Upinzani kukosa hoja za msingi za kuuwezesha kujijenga.

Baadhi ya Uzushi ambao kwa makusudi uliandaliwa na vijana hao kwa maelekezo ya viongozi wao ni pamoja na:

1. Kwamba Makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan aliandika barua ya kujiuzulu kwa sababu eti hakuwa na maelewano na rais Magufuli

2. Kwamba Makamu wa Rais aliiagiza mamlaka husika kuzima internet kuanzia asubuhi hadi jioni ili kuwezesha watumishi kufanyakazi

3. Kwamba Rais, Dkt. Magufuli alitengua uteuzi wa RC wa Arusha, Mrisho Gambo

4. Kwamba kiwanda cha Saruji cha DANGOTE kimesitisha uzalishaji kutokana na kupanda kwa gharama za uzalishaji wakati kumbe ni kutokana na tatizo la kiufundi

5. Kwamba Benki ya CRDB itafunga matawi yake yote nchini kuanzia mwezi januari 2017 ili kupunguza gharama za uendeshaji za benki hiyo

6. Kwamba Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi, Prof. Joyce Ndalichako atangaza kuwa Walimu wote wangeshonewa sare za kuvaa wawapo kazini

7. Kwamba Kifaru cha jeshi kiliuzwa

Huo ni baadhi tu ya uzushi ambao umekuwa ukienezwa na vijana hawa ambao wamekuwa tegemeo la propaganda za wanasiasa baada ya Serikali ya awamu ya tano kuonekana kufanyakazi kwa umakini zaidi na hivyo upinzani kukosa hoja za kupanda nazo kwenye majukwaa ya kisiasa.

Mytake: Ni wakati sasa serikali iubaini mtandao huu wa kutengeneza uzushi na kuuchukulia hatua za kisheria. Aidha Wananchi na sisi tujiepushe na uongo wa aina hii na tumuunge mkono rais bila kujali itikadi za vyama, dini na makabila yetu kwani kazi anayoifanya ni ngumu, ina vikwazo na hujuma nyingi zikiwemo hizi za kutaka kuidhoofisha serikali yake kwa maneno ya uongo.

Nitaongelea namba 5 katika orodha yako; suala la CRDB,hakuna aliyesema matawi yake yote, na kama kuna mtu atasema matawi yake yote basi haelewi anachokisema na haitaji kujibiwa! Nikweli CRDB ni benki kubwa kabisa hapa nchini na kwa bahati nzuri inaongozwa kwa kiwango kikubwa na watanzania lakini ukweli utabaki pale pale, kwamba uwezekano wa CRDB siku moja kupunza matawi yake hapa nchini ni mkubwa sana. Ikizembea kuanza kuyapunguza matawi yake itakuja kufa kifo cha mende.

CRDB ikiyumba haitakuwa imesababishwa na Rais wa nchi au utawala wake, yatakuwa ni matatizo ndani ya CRDB yenyewe. Ukiangalia matawi iliyonayo na uchumi wa sasa, inaonekana dhahiri kuwa kuna tatizo la msingi. CRDB wakati fulani imekuwa ikikiuka tarabu za kibenki kwa nia ya kujiongezea kipato. Kwa mfano CRDB ndiyo benki pekee hapa nchini iliyotakatisha fedha za EPA miaka ya mwisho ya utawala Mheshimiwa Mkapa.

Angalia mikopo, mikubwa iliyozihusisha Halmashauri za miji, wilaya na majiji, kama jiji la Mbeya, imejaa mazingira hatarishi. Kwa utawala wa sasa, hatutegemei biashara ya kiujanja ujanja, hali itakuwa mbaya bila shaka. Kwa hiyo matatizo ya CRDB hayawezi kuhusishwa na utawala wa sasa.
Mwisho, naomba nikuelimishe, kuukosoa utawala wa Rais wa sasa sio UCHADEMA na kuutetea utawala wa sasa sio UCCM kama unavyotaka kutuaminisha. Tuukosoe utawala kwa hoja za kisayansi na kuutetea kwa hoja za kisayansi na sio itikadi na rangi za vyama vyetu.
 
Tatizo na wewe mleta mada umejaa majungu mdomo wako mrefu kama bata.

Wewe kazi yako kukashifu wapinzani hiyo ndiyo tabia yenu wote.

Mimi binafsi naona JPM anafanya kazi kubwa hadi nawaza huyu mzee wetu anapata usingizi kweli? Nchi hii imejaa matatizo lukuki na naamini Magu angependa ayapunguze.....hususani corruption na uzembe kazini.

Wewe unayejiita Tata Madiba post nyingi unaandika chuki tu.....wala huonekani mwenye mchango wa maana na hicho chama chako CCM.

Pengine nyie mnaopiga domo hapa daily mnafurahi mkienda kusimulia friends zenu kwamba nyie ni hodari kubishana JF.

Acheni mambo ya ujuha vijana wa CCM na CHADEMA.....fanyeni kazi.
Umesema kweli
 
Walizusha kwamba Wabunge wa CCM wamehongwa milioni 10

walizusha kwamba hospitalini hakuna dawa wala chanjo

walizusha kwamba wanafunzi wa elimu ya juu wamekosa mikopo

walizusha kwamba Shigongo anaidai CCM

walizusha kwamba CCM imeshindwa kuwalipa wafanyakazi wake ktk kampuni ya uhuru

Jipeni matumaini na kuita kila kitu uzushi.............
 
Wacheni Sera za kibabe kwenye uchumi mtaiharibu nchi. Haya mambo ya kusingizia wapinzani ni kutapatapa tu. Dangote kwa mfano wanahusika nini na upinzani?
 
Tangu kuingia Madarakani kwa Serikali ya Awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Vyama vya upinzani hususan chama kikuu cha Upinzani cha CHADEMA kimetoa maelekezo kwa vijana wake walioko katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuandika taarifa za uongo dhidi ya serikali.

Maelekezo yenye lengo la kudhoofisha kasi ya utendaji kazi wa serikali ya Magufuli yamekuja baada ya Upinzani kukosa hoja za msingi za kuuwezesha kujijenga.

Baadhi ya Uzushi ambao kwa makusudi uliandaliwa na vijana hao kwa maelekezo ya viongozi wao ni pamoja na:

1. Kwamba Makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan aliandika barua ya kujiuzulu kwa sababu eti hakuwa na maelewano na rais Magufuli

2. Kwamba Makamu wa Rais aliiagiza mamlaka husika kuzima internet kuanzia asubuhi hadi jioni ili kuwezesha watumishi kufanyakazi

3. Kwamba Rais, Dkt. Magufuli alitengua uteuzi wa RC wa Arusha, Mrisho Gambo

4. Kwamba kiwanda cha Saruji cha DANGOTE kimesitisha uzalishaji kutokana na kupanda kwa gharama za uzalishaji wakati kumbe ni kutokana na tatizo la kiufundi

5. Kwamba Benki ya CRDB itafunga matawi yake yote nchini kuanzia mwezi januari 2017 ili kupunguza gharama za uendeshaji za benki hiyo

6. Kwamba Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi, Prof. Joyce Ndalichako atangaza kuwa Walimu wote wangeshonewa sare za kuvaa wawapo kazini

7. Kwamba Kifaru cha jeshi kiliuzwa

Huo ni baadhi tu ya uzushi ambao umekuwa ukienezwa na vijana hawa ambao wamekuwa tegemeo la propaganda za wanasiasa baada ya Serikali ya awamu ya tano kuonekana kufanyakazi kwa umakini zaidi na hivyo upinzani kukosa hoja za kupanda nazo kwenye majukwaa ya kisiasa.

Mytake: Ni wakati sasa serikali iubaini mtandao huu wa kutengeneza uzushi na kuuchukulia hatua za kisheria. Aidha Wananchi na sisi tujiepushe na uongo wa aina hii na tumuunge mkono rais bila kujali itikadi za vyama, dini na makabila yetu kwani kazi anayoifanya ni ngumu, ina vikwazo na hujuma nyingi zikiwemo hizi za kutaka kuidhoofisha serikali yake kwa maneno ya uongo.
Kwamba mikutano ya kisiasa yanje marufuku, kwamba bunge live marufuku, mikopo ya wanafunzi marufuku mbn hujayasema haya.
 
Back
Top Bottom