Kupambana na Serikali kwa maneno ya kuzusha ni dalili ya upinzani kukosa hoja

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Tangu kuingia Madarakani kwa Serikali ya Awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Vyama vya upinzani hususan chama kikuu cha Upinzani cha CHADEMA kimetoa maelekezo kwa vijana wake walioko katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuandika taarifa za uongo dhidi ya serikali.

Maelekezo yenye lengo la kudhoofisha kasi ya utendaji kazi wa serikali ya Magufuli yamekuja baada ya Upinzani kukosa hoja za msingi za kuuwezesha kujijenga.

Baadhi ya Uzushi ambao kwa makusudi uliandaliwa na vijana hao kwa maelekezo ya viongozi wao ni pamoja na:

1. Kwamba Makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan aliandika barua ya kujiuzulu kwa sababu eti hakuwa na maelewano na rais Magufuli

2. Kwamba Makamu wa Rais aliiagiza mamlaka husika kuzima internet kuanzia asubuhi hadi jioni ili kuwezesha watumishi kufanyakazi

3. Kwamba Rais, Dkt. Magufuli alitengua uteuzi wa RC wa Arusha, Mrisho Gambo

4. Kwamba kiwanda cha Saruji cha DANGOTE kimesitisha uzalishaji kutokana na kupanda kwa gharama za uzalishaji wakati kumbe ni kutokana na tatizo la kiufundi

5. Kwamba Benki ya CRDB itafunga matawi yake yote nchini kuanzia mwezi januari 2017 ili kupunguza gharama za uendeshaji za benki hiyo

6. Kwamba Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi, Prof. Joyce Ndalichako atangaza kuwa Walimu wote wangeshonewa sare za kuvaa wawapo kazini

7. Kwamba Kifaru cha jeshi kiliuzwa

Huo ni baadhi tu ya uzushi ambao umekuwa ukienezwa na vijana hawa ambao wamekuwa tegemeo la propaganda za wanasiasa baada ya Serikali ya awamu ya tano kuonekana kufanyakazi kwa umakini zaidi na hivyo upinzani kukosa hoja za kupanda nazo kwenye majukwaa ya kisiasa.

Mytake: Ni wakati sasa serikali iubaini mtandao huu wa kutengeneza uzushi na kuuchukulia hatua za kisheria. Aidha Wananchi na sisi tujiepushe na uongo wa aina hii na tumuunge mkono rais bila kujali itikadi za vyama, dini na makabila yetu kwani kazi anayoifanya ni ngumu, ina vikwazo na hujuma nyingi zikiwemo hizi za kutaka kuidhoofisha serikali yake kwa maneno ya uongo.
 
Wapinzani wa Tanzania ni pasua kichwa. Uelewa wao ni mdogo na sijui walipataje hizo nyadhifa walizonazo kwenye vyama vyao

Mlitaka wawe kama Makonda kutwa kutukana watendaji hadharani??Ila kimoja kikubwa uongo wa mpita njia si ukweli wa mwenye nyumba.Pole
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tangu kuingia Madarakani kwa Serikali ya Awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Vyama vya upinzani hususan chama kikuu cha Upinzani cha CHADEMA kimetoa maelekezo kwa vijana wake walioko katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuandika taarifa za uongo dhidi ya serikali. Maelekezo yenye lengo la kudhoofisha kasi ya utendaji kazi wa serikali ya Magufuli yamekuja baada ya Upinzani kukosa hoja za msingi za kuuwezesha kujijenga.
Baadhi ya Uzushi ambao kwa makusudi uliandaliwa na vijana hao kwa maelekezo ya viongozi wao ni pamoja na:
1. Kwamba Makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan aliandika barua ya kujiuzulu kwa sababu eti hakuwa na maelewano na rais Magufuli
2. Kwamba Makamu wa Rais aliiagiza mamlaka husika kuzima internet kuanzia asubuhi hadi jioni ili kuwezesha watumishi kufanyakazi
3. Kwamba Rais, Dkt. Magufuli alitengua uteuzi wa RC wa Arusha, Mrisho Gambo
4. Kwamba kiwanda cha Saruji cha DANGOTE kimesitisha uzalishaji kutokana na kupanda kwa gharama za uzalishaji wakati kumbe ni kutokana na tatizo la kiufundi
5. Kwamba Benki ya CRDB itafunga matawi yake yote nchini kuanzia mwezi januari 2017 ili kupunguza gharama za uendeshaji za benki hiyo
6. Kwamba Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi, Prof. Joyce Ndalichako atangaza kuwa Walimu wote wangeshonewa sare za kuvaa wawapo kazini
7. Kwamba Kifaru cha jeshi kiliuzwa
Huo ni baadhi tu ya uzushi ambao umekuwa ukienezwa na vijana hawa ambao wamekuwa tegemeo la propaganda za wanasiasa baada ya Serikali ya awamu ya tano kuonekana kufanyakazi kwa umakini zaidi na hivyo upinzani kukosa hoja za kupanda nazo kwenye majukwaa ya kisiasa.
Mytake: Ni wakati sasa serikali iubaini mtandao huu wa kutengeneza uzushi na kuuchukulia hatua za kisheria. Aidha Wananchi na sisi tujiepushe na uongo wa aina hii na tumuunge mkono rais bila kujali itikadi za vyama, dini na makabila yetu kwani kazi anayoifanya ni ngumu, ina vikwazo na hujuma nyingi zikiwemo hizi za kutaka kuidhoofisha serikali yake kwa maneno ya uongo.
Wazee walisema kisemwacho kipo kama hakipo kipo nyuma chaja.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi kunaupinzani tanzania tena? Kama ni hawa waliochukua wagombea kutoka ccm, siwa amini tena. Hata wanainchi walisha wapuuza mda mrefu.
 
Awamu hii ni kuambiana ukweli, subirini 2025 mtakapompata dhaifu mwingine kutoka CCM au Upinzani. Awamu ya tano nyeusi ni nyeusi na nyekundu ni nyekundu

Hakuna aliyejuu ya sheria.SIku yakija kukukuta ndipo utajua.Toka kuanza kwangu kazi sijawahi kumsikia kiongozi akimwambia mtumishi mwingine ...'UTAJUTA KUZALIWA"Kama Rais anabariki mpaka huu uendawazimu basi kama Taifa hatuna viongozi labda kuna neno lingine ambalo naweza nikalitumia
 
Kuna watu wanakera sana. Ningekuwa mimi ningeongea kwa maneno makali sana kuliko yale ya Makonda. Ardhi Kinondoni ni miongoni mwa taasisi zinazofanya vibaya sana
 
Tatizo na wewe mleta mada umejaa majungu mdomo wako mrefu kama bata.

Wewe kazi yako kukashifu wapinzani hiyo ndiyo tabia yenu wote.

Mimi binafsi naona JPM anafanya kazi kubwa hadi nawaza huyu mzee wetu anapata usingizi kweli? Nchi hii imejaa matatizo lukuki na naamini Magu angependa ayapunguze.....hususani corruption na uzembe kazini.

Wewe unayejiita Tata Madiba post nyingi unaandika chuki tu.....wala huonekani mwenye mchango wa maana na hicho chama chako CCM.

Pengine nyie mnaopiga domo hapa daily mnafurahi mkienda kusimulia friends zenu kwamba nyie ni hodari kubishana JF.

Acheni mambo ya ujuha vijana wa CCM na CHADEMA.....fanyeni kazi.
 
Nakushukuru tu kwa vile umerealize kuwa Rais wetu anafanya kazi kubwa. Mengine uliyoandika ni upuuzi mtupu
 
Back
Top Bottom