Kupaka rangi nyumba kunahitaji kibali. Nani wanatunga Sheria hizi?

drilling

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
4,658
4,747
Sheria zilizotungwa zinatuumiza.

Nilikuwa napiga rangi nyumba yangu nikakamatwa sina kibali cha ujenzi.

Hivi hata kupiga rangi tu kibali? Na kuna sheria ya ku-park gari pembeni ya barabara umewasha hazard unakamatwa hata kama imeharibika.

Watunga sheria hizi ni kina nani?
 
Kwa hiyo lengo ni kuwajua watunga sheria si ndio? Halafu?

Hiyo ya kupaka rangi ni ya Bunge.

Hiyo ya parking ni halmashauri
 
Hii ndio naisikia kwako aiseeh, kibali cha ujenzi sawa na siyo ukamatwe bali unazuiwa mpaka utakapokamilisha taratibu za ujenzi lakini kwenye kupaka rangi sijawahi kusikia
 
Hii ndio naisikia kwako aiseeh, kibali cha ujenzi sawa na siyo ukamatwe bali unazuiwa mpaka utakapokamilisha taratibu za ujenzi lakini kwenye kupaka rangi sijawahi kusikia
Hata mimi ndio nasikia saiv. Yani unafanya kaukarabati chako cha rangi mpaka kibali. Too much kwakweli
 
Labda kama sheria ya kulazimisha kupaka rangi hapo sawa. Hii ya kuzuia kupaka rangi ni ya mwaka gani?

Sheria zingine zimetungwa kwa malengo yake ya wakati mahsusi na yafaa zifanyiwe marekebisho au zifutwe kabisa kufuatana na mahitaji ya wakati.

Ianze na katiba ya zamani isiyokidhi mahitaji ya wakati huu.
 
Hii hapa mpaka nili laminate hii document for future ...use
IMG_20210622_214944_8~2.jpg
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom