Kupaa kwa ethiopia airlines (boeing 767) toka arusha airport

Kaduguda

JF-Expert Member
Aug 1, 2008
724
641
Hebu shuhudia namna ambavyo Boeing 767 ilivyoweza kupaa toka uwanja wa ndege wa Arusha. Japo ulikuwa mdogo bado kitu kiliweza kuinuka bila hata kumaliza runway!


GONGA HAPA ILI KUWEZA KUIONA



Karibu wataalamu wetu kwa comments sasa

 
Kaokoa roho za watu wakati wa kuland na wameitoa ndege kwa usalama. Bravoooooo
 
Nyie watu mnachekesha sana. Huwezi kupewa mashine kama ile na BOENG wakuruhusu uipaishe bila kuwa hujapewa shule ya kutosha. Kuna shule kubwa sana huwa wanapewa na haya mazoezi yote huwa wanafanya kwa kitu wanachoita Flight Simulator ambalo humo ndani unaweza ku-simulate mambo mengi sana sana yanayoweza kutokea kwa Rubani au ndege kama Moto, kutua majini, Engine kuzimika, upepo mkali mbele, nyuma au pembeni, kuruka nakupaa katika sehemu fupi, ardhi mbaya, nk nk. Huyo alichofanya ni moja ya mazoezi ambayo si ajabu huyo rubani alifanya kabla hajaja leo hapo Arusha.

Nina imani kabisa wakati nyie mnashika roho juu, yeye alikuwa akicheka tu kwani alijua umahiri wa Ndege hiyo na uzuri wa Engine zake ambazo zinaweza kufanya maajabu. Hii ndege lazima nikiri imenifungua macho sana kujua Engine yake inafanya kazi nyingi sana. Nilikuwa nashangaa kwa nini Pipa hilo gharama yake ni Mamilioni ya Dola, sasa nimeelewa. Ukiangalia ni kuwa kabla ya kurusha, kuna upepo mkali sana inarusha kabla haija-take off. Kilichotokea ni ndege kupaa hata kabla ya Uwanja kufika nusu yake. Haikuwa Bahati nzuri, ni shule tupu na Uzuri wa Engine.



Boeing 747-400 very early rotation ! 600 meter take-off run of a Boeing 747. Emirates Sky Cargo - YouTube
 
Last edited by a moderator:
daaa huyo ruban anaoneka yuko na passion na kitu anacho kifanya hajal yupo katk mazingira yap anaamini uwezo wake
 
InJamaa kahakikisha kaichochea moto injini wakati dude bado limesimama, lilivyoingia kwenye mwendo hata halikuhitaji kwenda sana kwani engine ilishapata momentum ya kutosha, na kama hamna upepo sana kitu kinang'oka kama unapaisha helicopter.

Inabidi niiangalie tena hii, hii ni sayansi na sanaa.

Kids don't try this at home.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom