Ukitaka kumtambua kiongozi mzuri, ni wakati wa matatizo. Ukitaka kumtambua dereva mzuri, angalia atafanya nini pale ambapo ajali ni dhahiri.
Kuna.mambo, kama nchi, huna uwezo wa kuyabadilisha bali unahitajika kuonesha weledi na ujuzi wa pekee, namna ya kukabiliana na yale usiyo na uwezo wa kuyabadilisha.
Hakuna asiyejua kuwa bei ya mafuta imepanda kwenye soko la Dunia. Wala wananchi hawahitaji kubiwa hilo, kwa dababu wanafahamu. Wanachotaka kubiwa ni je, Serikali inafanya nini ili kukabiliana ja hali hiyo. Hapo ndipo weledi wa uongozi unapotakiwa kupimwa.
Kipindi hiki ni vha janga, na majanga yanahitaji skills za ziada kukabiliana na hali. Kukitokea janga au changamoto, ukibweteke, unateketea moja kwa moja, uktafuta suluhisho sahihi, unaweza kutoka, tena ukiwa imara zaidi kuzidi hata ulivyokuwa mwanzo. Matatizo huikomaza nchi, hasa yanapotafutiwa suluhisho sahihi.
Kubweteka na kubakia kusema eti mbona Duniani kote bei za mafuta zimepnda, ni dalili ya kuishiwa maarifa na ufahamu wa namna ya kukabiliana na tatizo la upandaji bei ya mafuta.
Kuna kodi zaidi ya 10 kwenye mafuta, zote hizi zinaongeza mzigo wa bei ya mafuta, ambao tayari ni mzito kupindukia kutokana na bei kubwa ya mafuta kwenye soko la Dunia.
Kubakia tunasema eti mbona nanchi nyingina yamepanda, kama vile, kusema vile ndiyo utatuzi wa tatizo ni kukosa uongozi wenye maarifa.
Mazingira ya uchumi ya nchi moja na nyingine, yanatofautiana sana.
Kwa mfano, mataifa yaliyoendelea, mizigo mingi inasafirishwa kwa treni zinazotumia umeme, hivyo ongezeko la bei ya mafuta, haliwezi kuwa na athari kubwa ya moja kwa moja kwenye upanfldaji wa bei za bidhaa zote. Kuna nchi sahizi, zina kiasi kikubwa cha magari yanayotumia umeme/betri badala ya mafuta, lakini pia kuna yale ya hybrid, yanatumia mafuta kidogo, umeme zaidi. Hawa wote, kwao athari ya upandaji bei ya mafuta, japo ipo, lakini siyo ya kiwango kikubwa kama hapa kwetu.
Tanzania, kila kitu kinasafirishwa kwa mafuta. Kupanda kwa bei ya mafuta, ni kupanda kwa bei ya kila kitu.
Nilishangaa sana siku moja kumsikia Waziri Mkuu, akiuliza kwa nini bidhaa zinazozalishwa hapa hapa nchini nazo zipande bei!! Loh, kweli nchi ina ombwe la uongozi. Hivi kweli Majaliwa, hana uwezo wa kutambua kuwa unapopandisha gharama za usafirishaji maana yake umepandisha bei ya kila siku? Hivi mchele kutoka Mbeya kuusafirisha mpaka Dar, unabebwa vichwani au kwenye matumbo ya watu?
Ili kukabiliana na hali mbaya ya bei ya mafuta Duniani, Serikali ifute kodi zote kwenye mafuta. Mapato ya Serikali yatashuka, na baadhi ya miradi itasimama, lakini ni afadhali kutokee hayo kuliko uchumi wa nchi na maisha ya watu yaparanganyike.
NOTE:
Kuna mambo yanatia aibu. Wasaidizi wa Rais wanasema kuwa ile kauli ya Rais kuwa bei ya mafuta Marekani ipo juu sana kuliko Tanzania, ni kwa vile Rais alishindwa kutofautisha kati ya galoni na lita. Vituo vingi vya mafuta US, bei zilizoandikwa ni kwa gallon na siyo kwa lita. Ifahamike kuwa gallon 1 ni sawa na 3.785.