Kuonyesha upendo sio lazima ukae na wazazi wako milele

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,738
3,198
Nimepatwa na mawazo juu ya wenzetu wanaopenda kuishi na wazazi wao popote anapokaa/kuishi baada ya kupata kazi na kuanza maisha.Naongelea wale waliooa/kuolewa bado wanawakaribisha wazazi wao wawezi kuishi pamoja nao kama familia ili kulipa fadhila kwa wazazi kwa kukulea na kukuzaa.

Hili swala lipo saana katika Jamii zetu kwakuwa mara nyingi mzazi baada ya kukuzaa na kukusomesha uchumi wake anakuwa amewekeza kwa mtoto wake.hivyo mtoto anawajibika kumlea mzazi wake katika kipindi fulani.

Tatizo liko katika kulipa fadhila/kufanya wajibu wako kwa wazazi, kuna wengine wanaleta shida katika ndoa zao kwa kutaka kuambatana na wazazi bila kujari nature kuwa kuna kipindi unapaswa ukae peke yako na familia yako uingoze na kutoa maamuzi,wazazi wako wajibika kwa njia uliyoipanga wakiwa mbali na wewe.japo kuna wazazi nao huwaganda watoto wao jama ruba!

Hakuna asiyewapenda wazazi wake lakini kuna kipindi utawaacha na kubaliana na hilo agizo la Mungu.ukikaidi usilete lawama humu jf.
 
nikweli alafu mi hiyo habari ya kuwekeza nije nilipe fadhila kwangu haipo aisee eti nilkulea utoton nami nilee uzeen duh,,,,,, my signature inajpambanua hapo chini, habari ya maugomvi yasiyo na tija sitaki,,,,,,,,. kama pesa itatumwa na huduma nyingine hukohuko,.
 
Back
Top Bottom