Kwanza napenda bila unafiki wowote kumpa sifa kubwa sana Mwenyekiti wa CCM kaka yetu JK. Aliongoza nchi hii kwa umakini mkubwa sana. Anahitaji kila aina ya sifa kutoka kwa yeyote mzalendo wa nchi hii. Alitumia hekima na busara kubwa. Hii ilifanya nchi ikatulia vizuri sana
Inanifanya niamini kuwa, uongozi wa nchi siyo lazima kiongozi awe na elimu kubwa sana. Kama kuna wakati nchi hii iliwahi kupitia ktk changamoto nyingi, basi ni kipindi cha JK.
Kwanza ndiyo wakati demokrasia ilishika kasi mno. Lakini sikuwahi kumsikia kaka yetu akipiga marufuku mkutano wa mtu au chama chochote.na nchi ikaendelea kutulia Kama maji ya mtungi.
Kipindi chake kila mtu alikuwa na furaha akifuhia amani na kila aina ya uhuru. Mungu akujaalie maisha marefu na yenye baraka Mwenyekiti wetu.
Sasa hivi hali ni tofauti kabisa. Kiongozi aliyepo anaaza kuigawa nchi vipande vipande.watu wa itikadi tofauti hawasalimiani, hawazikani. Zanzibar ndiyo mfano halisi. Mfano mwingine ni bunge letu na vyama vyetu vyote vya siasa kwa ujumla. Hali ni mbaya. Mlio karibu naye mwambieni ukweli kuwa hali ni mbaya. Msisifie kila kitu.
Sasa hivi kuna hatari kubwa sana nchi hii ikaingia ktk machafuko makubwa kabisa kuwahi kutokea. Hili kila mtu analiona.na yanaweza kuanzia Dodoma na yakasambaa nchi nchi nzima.
Ushauri wangu, mkuu wa nchi aite mkutano wa vyama vyote wakae pamoja watafute muafaka. Kinga ni bora kuliko tiba.