Kuongezwa muda wa Urais: Askofu Emmaus Bandekile awaonya Rais Magufuli na Spika Ndugai

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Nimemsikia Mbunge mmoja akiongea Bungeni akitaka Bunge libadilishe Katiba ya Nchi ili kumfanya Rais Magufuli aendelee kutawala hata baada ya kumaliza kipindi chake cha kikatiba cha miaka 10. Kama hilo halitoshi, Spika Ndugai amesikika akimhakikishia Mbunge husika kuwa kazi hiyo ya kubadilisha kipengere cha Katiba kinachoweka ukomo wa Rais kuwa miaka 10 itafanywa na wao wote [Wabunge] katika Bunge lijalo. [Spika anaonekana kuwa na uhakika kuwa Rais Magufuli na wao wenyewe watachaguliwa tena katika Uchaguzi wa Mwaka huu].

Ninapenda niwalejeze Spika Ndugai, Wabunge, na Watanzania wote kwa ujumla kuhusu habari ya Mfalme Darius na Bunge lake katika Dola ya Uajemi (Persia) na Umedi (Mede) yapata miaka 2500 iliyopita.

Mfalme Darius aliunda Baraza (Bunge) lake lenye Wajumbe 120 aliowateua yeye wenyewe. Katika hali ya kutaka kumkomoa Danieli ambaye alionekana kuwa na uwezo mkubwa wa kiuongozi kuwazidi wao, Wabunge wenye nia ovu walianzisha mikakati ya siri ya kutaka kumnyamazisha Danieli.

Mikakati yote iliposhindwa, waliamua kutunga sheria ambayo walijua kuwa itamfurahisha Mfalme Darius lakini huku ikiwa na lengo lililojificha la kumnyamazisha kabisa Danieli kwani walijua kuwa hatima ya sheria ile ilikuwa ni kifo cha Danieli. Walitunga sheria ya kutukuza mawazo ya Mfalme kwa kusifu na kuabudu mradi au sanamu aliyoitengeneza Mfalme.

Walimshawishi Mfalme aitie muhuri au aisaini sheria ile. Wakapitisha Azimio la Ki-Bunge la kuzuia mtu ye yote au mamlaka ye yote kutangua sheria ile. Hata hivyo, Mungu hakuruhusu uovu ule na akaingilia kati. Wabunge wote waliopitisha Azimio lile waliuawa pamoja na wake zao na watoto wao lakini Danieli alipona na aliendelea kustawi zaidi. Kwa uelewa zaidi kuhusu habari hii someni Biblia Takatifu katika Kitabu cha Danieli 6:1-28.

Tunapenda kuwaonya na kuwatahadharisha Wabunge na watu wote wanaofanya mikakati ya kutaka kutunga Sheria mbalimbali zenye hila mtambuka ikiwemo kutaka kumfurahisha Rais aliyeko madarakani lakini lengo kuu lililojificha likiwa ni kulinda matakwa yao binafsi kwa njia ya kuwazuia au kuwanyamazisha watu wengine wanaoonekana kuwa ni tishio kwa nafasi zao na matakwa yao! Mungu anatoa onyo kali kwa watu na viongozi wa namna hiyo (Isaya 10:1-4).

Ushauri wangu kwa Rais Magufuli ni kuwa awe makini sana na watu ambao kila kukicha wanapenda kumsifia tu pasipo hata kumtahadharisha. Akiwafuata watu wa namna hiyo, basi ajue kuwa anaikaribisha hasira ya Mungu kwake mwenyewe na kizazi chake!

Ninamshukuru Mungu mwenye rehema nyingi kwa kunipa ujasiri wa kuyaandika haya (Ezekieli 33:1-20).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
 
Ilianza kama story ila sasa tunapoelekea naona hili swala lishapita na lazima litokee hivi mimi naomba nikuulize ndugai na CCM yako hivi mmefikiria umbali kiasi gani? au nyie mnawaza maisha yenu tu ya watoto wenu na wajukuu wenu hamuyawazii?

Haiingii akilini kabisa mtu anaongea kwamba hatuwezi pata mtu kama JPM tena! hivi mko serious kweli nyie? kweli hii nchi yenye watu milioni 60+ asipatikane mtu kama kama yeye?

Kama mnaajenda zenu binafsi mseme lakini hoja hizo hazina mashiko, hivi mkiweka ukomo wa Rais maybe ikawa ni mihula minne hivi mnajua huko mbeleni mtakuja kuongozwa na Rais gani? mfano Rais aongoze kwa mihula minne hivi ikitokea akaja akapatikana Rais mbovu hii nchi itawekwa kwenye hali gani?

mimi ninaamini hata JPM mwenyewe hawezi kukubali lazima ataiheshimu katiba!

Hii nchi imeongozwa hata kabla yake na itaendelea hata baada yake, sisi wananchi hatukuwatuma hivyo, hayo ni maoni yenu binafsi sio ya wananchi mnaowawakilisha!

Hivi Spika Ndugai wanakongwa ndio wamekutuma hivyo? mpo bungeni kuwakilisha mawazo ya wananchi wenu waliyowaagiza sio kuwakilisha mawazo yenu msijisahau


Kweli JPM anafanya kazi nzuri sana lakini kwa swala la kuongezewa muda hapana kwakweli
 
Kwa awamu hii hakuna litamkwalo pasi kujulikana na mshika hatamu wa sasa. Ukiona watu kama vile wanaropoka elewa kuwa kuropoka huko kuna kila baraka za mtajwaji mkuu. Hatuna ujasiri wa kudai katiba mpya hivyo tujiandae kisaikolojia kuwa kama Uganda tu.

Tatizo la Wadanganyika tuko vizuri sana kwenye kuandika na kuzungumza nyuma ya pazia lakini sio watendaji wa kudai kile tunachoandika na kuzungumza. Hivyo tukubali hatma yetu na maisha yaendelee.
 
Nimekuwa mnazi sana wa awamu hii, lakini kasi ya kuisha ymuhula wa mheshimiwa imekuwa kubwa, yaani kama kuna mkono wa mtu, kufumba na kufumbua 2015-2020 imeisha,tunajua 2020-2025 ndio kabisa itapita kama upepo.

Watoto bado wanasoma,kakibanda hakajaisha, sijui itakuwaje yaani

Kwa kweli katiba ibadilishwe tuendelee kula na kumalizia majukumu mawili matatu
 
Nimekuwa mnazi sana wa awamu hii, lakini kasi ya kuisha ymuhula wa mheshimiwa imekuwa kubwa, yaani kama kuna mkono wa mtu, kufumba na kufumbua 2015-2020 imeisha,tunajua 2020-2025 ndio kabisa itapita kama upepo.

Watoto bado wanasoma,kakibanda hakajaisha, sijui itakuwaje yaani

Kwa kweli katiba ibadilishwe tuendelee kula na kumalizia majukumu mawili matatu
Umesahau kuweka namba ya simu
 
Nimekuwa mnazi sana wa awamu hii, lakini kasi ya kuisha ymuhula wa mheshimiwa imekuwa kubwa, yaani kama kuna mkono wa mtu, kufumba na kufumbua 2015-2020 imeisha,tunajua 2020-2025 ndio kabisa itapita kama upepo.

Watoto bado wanasoma,kakibanda hakajaisha, sijui itakuwaje yaani

Kwa kweli katiba ibadilishwe tuendelee kula na kumalizia majukumu mawili matatu
Kumbe!!!

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Tulimuomba Mungu aondoe COVID-19,tutamuomba MUNGU huyo huyo washindwe kwa njia yoyote kuongeza muda..kama wanafikiri Mubgu alisikia maombi ya ya COVID-19 na mengine hatasikia wanajidanganya
 
Magufuli aliposema omba kwa ajili ya janga la corona ulimkejeli.
Sasa hivi unajifanya kumjua sana Mungu na kunukuu maandio!

Mpka oktoba lazima nguo za ndani mvae kichwani.
 
Kila Mtanzania kwa nafasi yake na imani yake akemee huu ujinga.
 
Wasijaribu kucheza na katiba ita tugarimu miaka mingi. Ila na uhakika raisi hawezi fata ushauri wa hao viongozi wasio jielewa
 
Back
Top Bottom