Kuongezeka kwa Wanawake wenye ndevu, Tatizo nini?

Page 94

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
5,204
15,198
Salaam Wakuu.

Zamani tukiwa wadogo, ndevu kwa wanawake zilikua nadra sana. Ni wanawake wachache sana hasa wa Kichaga (wamachame na Wakibosho),hasa wafanyabiashara ndiyo waliokuwa na ndevu mbili tatu kwenye videvu vyao. Lakini, kwa sasa wanawake wengi wana ndevu nyingi tu kama wanaume au hata zaidi.

Nimekua nikistaajabu kadri siku zinavyoenda ndivyo wanawake wenye ndevu wamekuwa wengi sana tofauti na miaka ya nyuma.

Kimsingi, ndevu ni sehemu ya ukuaji kwa mwanaume (siyo wote lazima waote ndevu). Kama ambavyo mwanaume hubadilika sauti na kuwa nzito, kupanuka kifua na mambo mengine, kuota ndevu ni sehemu pia ya ukuaji. Ndevu huzalishwa na hormone iitwayo androgenic hormone. Homoni hii i zaidi kwa wanaume na si ajabu wala haishangazi kumkuta mwanaume na ndevu.

Lakini, huwa nashtushwa sana nikimkuta mwanamke na ndevu nyingi haswa. Nyingi sana. Yaani, unakuta kidevu kimejaa ndevu, ukichanganyia na sura ya baba yake unaweza kudhani ni dume.

Nimekuwa nikistaajabu sana. Je, kuongezeka huku kwa wanawake wenye ndevu husababishwa na nini? Je, ni vyakula tunavyokula? Je, wanakuwa na homoni za kiume nyingi?

Vipi, wapenzi wao? Hivi, mnajisikia amani kuwa nao kwenye gemu? Ndevu haziwabugudhi katika zoezi zima la kulana mate?
Afu wengi wao ni wanene kama Miss fulani humu jukwaani.

Je, nini kifanyike ili kuzuia au kupunguza ongezeko hili la wanawake wenye ndevu?

Nawasilisha.
 
Duu! Eti kuimarika kiuchumi. Hapo kitu hormones mwilini inazalishwa isivyo. Matokeo ndo mojawapo videvu kwa m/Ke na matiti kwa mme.
 
Dr, unataka kumaanisha hizo ndevu zinatoa fedha? Je, mwenye ndevu nyingi ndiye mwenye pesa nyingi? Je, wasiyo nazo hawapo vizuri kiuchumi?
No dear jibu langu halihusiani na sayansi kabisa, nimeongelea kuhusu uwezo wa kiuchumi kwa kuwa, zamani wanawake wanalitegemea wanaume ki-uchumi na kuolewa ilikuwa ni sehemu ya ajira au vacation kwa mwanamke. Sikuhizi wanawake wengi wanajiweza ki-uchumi. I am not a Dr, mimi ni kapuku tu mkuu.
 
Binafsi sijawai kutana na mwanamke mwenye ndevu kabisa zaidi ya wale wenye tunywele tuwili tutatu kidevuni...
Nadhani vyakula tunavyokula miaka ya sasa vinavuruga mgawanyo wa hormones kwa watoto. Matokeo yake msichana anakua na hormones nyingi za kiume kupelekea kuota kwa ndevu. Ni maoni yangu tu, sio scientifically proven.
 
Wapo wengi Mkuu. Mimi nimeshakutana nao wengi sana. Zaidi hata ya 20, huku kwenye jiji la Makonda. Hata mimi nilikua naona kawaida kwa wenye tunywele tuwili tutatu.
 
Binafsi sijawai kutana na mwanamke mwenye ndevu kabisa zaidi ya wale wenye tunywele tuwili tutatu kidevuni...
Nadhani vyakula tunavyokula miaka ya sasa vinavuruga mgawanyo wa hormones kwa watoto. Matokeo yake msichana anakua na hormones nyingi za kiume kupelekea kuota kwa ndevu. Ni maoni yangu tu, sio scientifically proven.
Wapo wanaonyoa kabisa mkuu baada ya hapo ndiyo cream to powder ya fashion fair inahusu.
 
mabadiliko ya tabia ya nchi ndio yanapelekea hiyo hali.... btw si huwa wanasema we are equal!? basi maombi yao Mungu kayasikia
 
Binafsi sijawai kutana na mwanamke mwenye ndevu kabisa zaidi ya wale wenye tunywele tuwili tutatu kidevuni...
Nadhani vyakula tunavyokula miaka ya sasa vinavuruga mgawanyo wa hormones kwa watoto. Matokeo yake msichana anakua na hormones nyingi za kiume kupelekea kuota kwa ndevu. Ni maoni yangu tu, sio scientifically proven.
55de18e095c2f0f7f988eb6090499afe.jpg
54471a0cc52aeb8eb10a3bf833716b1a.jpg
 
Back
Top Bottom