Kuongezeka kwa muda wa kubadilisha taarifa za wateja wa mabenki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuongezeka kwa muda wa kubadilisha taarifa za wateja wa mabenki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Maswa, Mar 14, 2012.

 1. M

  Maswa Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  WATEJA WAONGEZEWA MUDA KUREKEBISHA TAARIFA BENKI
  BENKI Kuu ya Tanzania imeongeza muda wa mwaka mmoja kwa wateja wa benki zote nchini kuboresha taarifa zao kuanzia kesho Machi 15, 2012 hadi Machi 14, 2013. Benki na taasisi zote za fedha zimejulishwa kuzingatia kikamilifu agizo hili. Agizo la awali lilitamka kwamba muda wa kuboresha taarifa za wateja wa benki ungelimalizika leo.Mwaka jana (2011) Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustafa Mkulo, alitoa kipindi cha muda wa mwaka mmoja kuanzia Machi 15, 2011 hadi Machi 14, 2012 kwa ajili ya zoezi hilo. Hii ilikuwa ni kuziwezesha benki zote kuzingatia kanuni zilizomo katika Sheria ya Kudhibiti Fedha Haramu.Wakati huo huo, Benki Kuu ya Tanzania inawataka wananchi na wateja wa benki nchini kutimiza wajibu wao kwa kujaza fomu za taarifa zao ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kwa kushindwa kutimiza sharti hilo la kisheria.
  Imetolewa na Idara ya Uhusiano na Itifaki
  BENKI KUU YA TANZANIA
  Machi 14, 2012

  PRESS RELEASE
  CUSTOMERS GIVEN MORE TIME TO UPDATE BANK RECORDS
  THE Bank of Tanzania (BoT) has extended the deadline for bank customers to update their bank data for a period of one year starting from tomorrow March 15, 2012 to March 14, 2013. Following this new development, all banks and financial institutions have been informed and asked to comply as the initial deadline issued last year was expected to end today. The extension follows consultations with the Ministry of Finance and Economic Affairs. The Minister for Finance and Economic Affairs, Mr. Mustafa Mkulo, granted a one-year moratorium (March 15, 2011 to March 14, 2012) for banks to comply with the Anti-Money Laundering Regulations, 2007 to enable banks to regularize/update all accounts opened prior to the coming into force of the Anti-Money Laundering Act. Meanwhile, the Bank of Tanzania urges members of the public to comply with the requirement in order to avoid inconveniences that could result from failure to adhere to the directive of updating their personal information.
  Issued by the Public Relations and Protocol Department
  BANK OF TANZANIA
  March 14, 2012
   
 2. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,350
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Pouwa !
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mimi ni peasant. Hayanihusu!
   
 4. M

  Maswa Member

  #4
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vizuri ila tambua kuwa peasant mzuri lazima awe na taarifa za nini kinaendelea katika nchi yake hasa ndiyo lengo la jumbe huu kuwekwa wana JF wajue! wewe kama hii taarifa haikuhusu uko primitive sana! Pole sana ndugu yangu....waache inayowahusu waendelee kuhabarishana!
   
 5. P

  Puza Senior Member

  #5
  Mar 14, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  shukran mkuu nadhani itakuwa ni fursa kwa walioshindwa kufanya hivyo kukamilisha ila je ac zitaendelea toa pesa kama kawaida kwa atm hili haswa ni kwa wale walio nje ya nchi wanategemea mastercard na viza ntaomba wanaofaham watujuze.
   
 6. d

  dav22 JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  du safi sana maana muda wenyewe wa kwenda bank ku-update hamna kabisa
   
 7. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Mi nilienda kwenye tawi langu la NMB kufanya hivyo,jamaa akasema sina haja ya kuhakiki,so sijui inakuwaje...
   
 8. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Ndio maana baadhi ya watu wanasema "Tz ni kichwa cha mwendawazimu". Kutokana na hiyo habari, je kuna haja ya kufanya utafiti ili kuthibitisha ukweli?????
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Heri yako wewe unayewaita wenzako primitive! Ngoja mimi nichukue jembe langu la mkono nikalime shambani.
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  kawaida, ikifika machi wataongeza miezi mingine mitatu.....
   
 11. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Thanks 4the info.
   
 12. b

  binti ashura Senior Member

  #12
  Mar 15, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0


  mie nilijuwa kuwa itakuwa hivyo kutokana na historia ya bongo ni kuwekana kwenye presha halafu inakuwa hivi. walisema usiposajiri simu mwisho tarehe furani walioitaja ilipofika wakaongeza muda na baadae kimyaaaaaaaaaaaa.
  wakaja na noti mpya ambazo walisema mwisho mwezi wa sita mwakajana kutumia noti za zamani lakini mpaka leo zinatumika. bongo yetu wanaweka msukumo pale ambapo serikali unachukua pesa kutoka kwa wananchi direct mfano kubadirisha reseni za magari, pass za kusafiria, kuanzisha vituo vya kukusanyia ushuru au kodi mbalimbali hata kama hapajakaa sawa watarazimisha watu waanze kulipia mfano kituo cha kukusanyia ushuru kwenye magari Irula na mengine mengi.
   
 13. NEXTLEVEL

  NEXTLEVEL JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 856
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 80
  Heeeh kumbe ilikuwa mwisho tarehe 14March2012 duh akaunti zangu zote nilikuwa zijaziupdate ingekula kwangu asante BOT nitafanya upesi.
   
 14. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Itapunguza kero ya foleni.
   
Loading...