Kuongezeka kwa matukio ya UBAKAJI Nchini, tatizo ni nini? Tujadiliane tuokoe taifa letu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,302
5,439
Mimi ni mmoja wa watu ambao wamekuwepo kwenye ulimwengu wa habari kwa muda mrefu, siyo mkongwe lakini nakaribia kwenye Dunia ya wanahabari wakongwe.

Moja kati ya nyakati ambazo zimekuwa zikitawaliwa na matukio ya ukatili kwa binadamu hasa ubakaji, ulawiti na udhalilishaji kwa Wanawake na watoto ni miaka ya hivi karibuni.

Kila unaposikia kesi za matukio hayo huwa kunakuwa na sababu ambazo wazi unaona hazina kichwa wala miguu, sijui dunia inaelekea wapi!

Inashangaza sana, matukio ya ubakaji ndio kabisa yamezidi kuwa mengi, bado najiuliza kuongezeka kwa matukio kama hayo, je ni utandawazi, tabia tu zimebadilika au ni nini hasa ndugu zangu, tujadiliane ili tuokoe kizazi chetu ndugu zangu, TATIZO NI NINI UBAKAJI KUSHIKA KASI NCHINI?

faa98c72dafd590a4cd7e3eb9aedcf136b214cfd.png


=======================

Kwanini matukio ya ubakaji yanaongezeka?

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa amesema kuongezeka kwa makosa ya ubakaji, inasababishwa na vyombo vya habari kuzipa kipaumbele habari hizo na watu wamekuwa na mwamko wa kutoa taarifa za ubakaji katika vyombo vya dola.

“Huenda sasa hivi utoaji taarifa dhidi ya vitendo hivyo ni mkubwa kuliko zamani. Siyo ajabu ukakuta zamani watu walikuwa wakibakwa sana kuliko hata sasa,” amesema Ole Ngurumwa.

Baadhi ya tafiti zinaeleza kuwa mmomonyoko wa maadili kwenye jamii, matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, wazazi/ walezi kukosa muda wa kutosha wa kukaa na watoto kuwafundisha maadili mema na mila potofu kwa baadhi ya makabila kuona kuwa mwanamke ni chombo kinachoweza kutumika kwa namna yeyote ile ni baadhi ya vitu vinavyochochea ubakaji.


Pia soma:
~Kesi 42 udhalilishaji kwa Wanafunzi zaripotiwa Pemba, kuna ubakaji, ulawiti na mimba
~Serikali: Ripoti ya kesi za ukatili kwa watoto, Ubakaji 5,899, mimba 1,677, ulawiti 1,114
~Mbunge: Ubakaji umeongezeka sasa sababu wanaume wanashindwa kununua mapenzi, mapenzi ni bidhaa
 
Wimbi la watu wengi sana wanaangalia porno sijui kwanini serikali iliziachia tna lilikuwa maamuzi sahihi sana Kwa kizazi chetu
 
Utelezi umekuwa wa gharama sana na watu hawana vipato vya kuwawezesha kupata starehe pendwa
 
Back
Top Bottom