Kuongezeka kwa matukio ya Ubakaji, Chanzo ni nini ?

HadithiZaRuvuly

JF-Expert Member
Apr 16, 2014
369
114
Tatizo la ubakaji linazidi kukua kila siku watoto wenye umri mdogo wanabakwa na watu wazima tatizo huwa ni nini ?
369493798165c4fa8f862900ce212fc3.jpg
 
Sijui hao wabakaji wanakua wagonjwa wa akili au laana zao tuu,manake wanawake walojaa tele unakwendaje kumbaka mtoto wa mwenzio bila ridhaa yake?
 
Ndumba. Mganga anampa masharti magumu mteja wake baada ya kumpiga mpunga wa kutosha. So anamwambia kambake mtoto mdogo ukifanikiwa hilo utajiri upo mlangoni. Kumbe ndio anaingia mlango wa jela.
 
Chanzo kikubwa cha ubakaji ni social inferiority ya mbakaji.

Mwanaume anapokuwa kwenye rank ya chini kwenye jamii anakuwa na nafasi ndogo ya kuwa genes donor.

Atakapohitaji mwenza obviously atakumbana na rejections nyingi kuliko kawaida, ndipo atakapofanya vitendo vya ubakaji.

Social inferiority inasababisha watu masikini wajihusishe na vitendo vya kiuhalifu kujipatia mali ili wasawazishe gap baina yao na wenye navyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom